Watanzania wengi hufa bila hata kumiliki Tsh 100M katika maisha yao. Wewe, ushawahi kumiliki ?

Na sisi tunaomiliki zaidi ya milioni 100 tutolee uzoefu wetu wapi?
 
Hapa duniani lazima uwe na focus, ipende biashara yako au kazi yako kwa moyo wako na usimwamgalie mtu aliye shindwa
Kaa na watu wenye positive thinking
Pesa ina watu wake walahi
Hiyo pesa unayo sema niliishika nikiwa shule Maana wengine tuna old money
Babu wa babu katengeneza pesa safi, bibi wa bibi naye katengeneza pesa swafiiii
Sisi tunaiendeleza!
Pesa inakuchagua na unaiheshimu
Namkumbuka Ndesamburo, Aikaeli Mbowe, Frank Mareale n.k. hawa kina babu walikuwa strict katika biashara zao, lakini watoto wao majanga matupu!
Kuwa na kiu ya kutengeneza pesa, hivi hivi hata ukipewa $20m utazipoteza zote kama ukiwa ni mtu wa mkosi!
 
nilikamata milioni 70 nikiwa na 25 niliipata baada ya kuuza eneo la heka mbili jamaa akajenga shell ndgu jamaa ilikuwa balaa nilifaidi kama40 tu
 
Cheza biko! hakuna kazi ya kukupa pesa hiyo kwa mara moja tanzania hii zaidi ya kamari😨😨😨😨
Unachekesha kweli
Hiyo mbona pesa ndogo sana
Tender moja tu ya kipumbavu inamuingizia mtu huo mpunga mara kwa mara
 
Hela yote hiyo nipeleke wapi? Mimi nikipata buku tano ya mboga inatosha mafweza mengi hayo kila mtu atanitolea machom

Sio sirikali - wasiofahamika, tiaraei..
Sio ndugu
Sio vicheche
Sio majambazi

Kila mmoja kwa wakati wake
 
Unachekesha kweli
Hiyo mbona pesa ndogo sana
Tender moja tu ya kipumbavu inamuingizia mtu huo mpunga mara kwa mara
Si kwa watanzania wengi sasa boss! Mfano tenda za barabara n.k wanamudu waTZ wachache.
 
Wale wa FOREX a.k.a wazee wa kudownload madolareee humu jf itakua wanapiga hayo mamiliion,teh teh
 
Ungesema kwa mkupuo ungeeleweka,lakini umesema sio lazima kwa mkupuo..je huoni kama total mishahara ya huyo mtumishi wa umma tangu aanze kazi,inafika 100 mil kwa miaka hata 20?
 
Aisee we jama hujui kwamba wapo wengi sana ambao wanamiliki hizo senti,ungesema Bilioni moja ningekuelewa ila cash flow ya milioni mia moja ni hela ndogo
 
Kama ni jumla ya mali zote Mil 100 ni ndogo sana mkuu,kama ni cash mkononi ni nyingi sana.
Mfano mafinga kuna vijana wana mbao zenye thamani zaidi ya mil 200,usukumani wafugaji wana ng'ombe zaidi ya 400,mashambani mbeya ndio usiseme.
Mil 100 ni ndogo
 
Nishawahi kupata Milion 50....niliipata kipindi nasoma bavaria katika chuo cha passau universty nilikuwa off campus ,

Nilipata kazi za ajabu ajabu kufanya but zilikuwa zianilipa sana .....baada ya kumaliza nilipata kazi ya muda katika kampuni ya GULO FILM Ya ujerumani ....ndipo nilipopata mpunga wa kutosha mpk leo ilishabaki story nasubiri labda pension yangu nitapiga M 200 BUT NI MWAKA 2048. ndiyo nastaff serikalin

sent from toyota Allex
 
Ungesema kwa mkupuo ungeeleweka,lakini umesema sio lazima kwa mkupuo..je huoni kama total mishahara ya huyo mtumishi wa umma tangu aanze kazi,inafika 100 mil kwa miaka hata 20?
Nataka hata kama kwa kudunduliza, uwe nayo tayari ushashika mkononi total 100M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…