Watanzania wengi mnatia huruma kwenye uandishi wa Kiswahili

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kuna uzi nilianzisha kuhusu taarifa za Kenya kuingia mkataba na Afrika Kusini ili kuwasaidia kuzindua elimu ya lugha ya Kiswahili kwenye mtaala wao. Kuna Watanzania wametiririka kwa povu za kiajabu huku wakijinadi kwamba wao ndio wamiliki wa hii lugha na hao ndio waliopaswa kualikwa wakaifunze, ila cha kushangaza, hao hao Watanzania ukisoma humo uandishi wao wa Kiswahili unatia huruma na ukihoji wanakuambia hawana haja ya kuzingatia Kiswahili sanifu.

Unakuta mtu anajisifu jinsi alivyoganda kwenye Kiswahili pekee na hataki kujiongeza kwenye lugha nyingine, ila hicho hicho Kiswahili hakitendei haki, anaandika upupu mtupu, Kiswahili kibovu kupita maelezo.

Watanzania mnatia huruma mjue, mnazembea hamtaki kujifunza Kingereza, pia lugha zenu za asili mumezitelekeza, madogo wengi hamzijui hata salamu, kazi yenu kuvaa milegezo na kushobokea wasanii mjini mjini, halafu Kiswahili hamtaki kujiboresha, uandishi wenu wa ovyoo, ni janga la taifa lakini kama mbuni mumefukia vichwa vyenu na kuanika maeneo mengine yote.

Watanzania wengi kazini ukiwaomba waandike taarifa/ripoti kwa Kingereza hawawezi, ukiwaagiza basi waandike kwa Kiswahili halafu utatafsiri mwenyewe hapo ndio utashangaa kitu watakachokuandikia, mtu hazingatii alama za uandishi, matumizi sahihi ya misamiati n.k. Kiswahili kibovu hadi kinatia hasira.

Sio kwamba najisifu wala kuwasifu Wakenya kuwa tunajua Kiswahili kuwazidi Watanzania, ila ni kwamba wengi tunapambana kujiboresha kila siku, kuyakubali mapungufu yetu na kuyafanyia kazi, mimi binafsi tangu nikiwa mdogo nilipenda sana kusoma gazeti la Taifa Leo ambalo huandikwa kwa Kiswahili, nia na lengo lilikua kujifunza jinsi ya kutumia hii lugha ipasavyo.
 
.....alisikika manzi mmoja wa Nairobi baada ya kupiga chupa kadhaa za keroro!
Hiyo ni lugha ya mtaani baina ya vijana, hata mimi niliitumia sana enzi zangu nikiwa kijana, nilikua nazungumza shen'g hadi basi, hata leo mtaani huwa nataniana na vijana wakiwemo wanangu kwa matumizi ya hiyo lugha, lakini pamoja na hayo ni kwamba huyo mtu ukimuagiza aandike taarifa/ripoti kwa Kiswahili au Kingereza, utafurahia uandishi wake ulionyooka.

Hapa Kenya tunatumia lugha nyingi, mwanangu hapa anapiga Kiswahili, Kingereza, Sheng, Kikikuyu, na Kiluhya kwa kiasi, na pia shuleni wanajifunza Kifaransa, hii inachangia uwezo wa kupanua ubongo na matumizi yake sio kuishi kama zezeta.
 
Naomba unieleze ufasaha wa hili neno lako " wameganda kwenye kiswahili" na kujiongeza kwenye lugha zingine, halafu ndio ukosoe watanzania kuhusu kukifahamu kiswahili fashion.
 
Eti wa Tanzania hawajui kiswahili na hawataki kujifunza English na kilugha, kila siku nasema unajitia hodari wa kuijua Tanzania kinaganaga kumbe huna ulijualo kuhusu hii nchi

Watanzania wasojua kikwao ni wachache sana, nafikiri less than 30% na wengi ni sababu ya kukulia mijini na wazazi wenye different ethnicity {by the way Tanzanians don't care ethnicity as the first acceptance in relationships like Kenya} japo huwezi kuta hawajui hata maneno machache upande wa baba au hata mama. Ndio maana JPM kwenye mikutano yake lazima asalimie watu kwa kilugha kwanza.

Kingine Tanzania saivi secondary education is compulsory for every primary school leavers, kwa hiyo hiyo mantiki ya Watanzania hawataki kujifunza English inapata natural death hapo, by the way kama hujui all private schools in Tanzania 35% of total school count in the county are English medium schools, kwa hiyo wapo Watanzania kwa mamilioni ambao hawakusoma swahili medium schools {public schools} at all. Suala la French Tanzania kinafundishwa kila kona pamoja na International languages kibao

Lastly but not least, Tanzania tunapenda uafrika wetu na African identities sio katika kuenzi utamaduni wetu wa lugha ya kiswahili tu bali mpaka hata mavazi ya Watanzania ni ya kiafrika kuliko huko Kenya mlikokumbatia umagharibi, huwezi kukuta mavazi ya kitenge, bazee, batiki, khanga {African prints} huko Kenya na urembo wa culture, nyimbo, ngoma, hadithi za kitamaduni kwa hiyo huna legitimacy ya kutufundisha Watanzania kuthamini uafrika kikiwemo kiswahili chetu wakati nyinyi ni mfu kabisa kwenye hilo.
 
Naomba unieleze ufasaha wa hili neno lako " wameganda kwenye kiswahili" na kujiongeza kwenye lugha zingine, halafu ndio ukosoe watanzania kuhusu kukifahamu kiswahili fashion.

Hamna sehemu nimejisifia kukijua Kiswahili zaidi ya Watanzania, nimesema huwa napambana kujiboresha kila siku narekebisha mapungufu yangu, ila nyie mpo mpo tu, hamtaki kujiongeza wala kukosolewa.
 
Reactions: Ilu
sijkuelewa mkuu unachomaanisha.watanzania hatujui lugha yetu ya kiswahili au lugha za mataifa mengine?
 
We jamaa mara nyingi unapozungumzia Tanzania unakuwa na mtazamo hasi kabisa. Sababu haswa ni ipi?! Ni kipi mtazania akihitaji kutoka Kenya ili awe bora!! Jibu ni hakuna! Tabia za binadamu yeyote ni matokeo ya utamaduni uliomkuza, hivyo huwezi kumuhukumu mtanzania kwa kutoishi kama mkenya, uelewa na uwezo wako wa kuchambua masuala ya kijamii ni hafifu sana na umetawaliwa na ubinafsi, pengine kwa kuwa huko Kenya kuendekeza ukabila ni sehemu muhimu ya maisha yenu.

Ni kweli Kiswahili unakifahamu, tena kuna uwezekano mkubwa kuwa Kiswahili chako umejifunzia na kukizungumza sana ukiwa Tanzania unakokudhalilisha kila uchao. Kiswahili cha Kenya na Tanzania ni tofauti sana, japo kuna mfanano kiasi angalau kwa wakazi wa Mombasa.

Watanzania wanakifahamu Kiingereza vizuri sana ila hatuna matumizi ya mara kwa mara tuwapo hapa kwetu na haituathiri, hivyo unajua kuwa lugha isipotumika mara kwa mara ni rahisi kusahaulika ama kupoteza radha muhimu za lugha husika. Nakukumbusha kuwa kutokujua Kiingereza hakupunguzi uwezo wa akili hata chembe. Kwani wewe wafahamu Kichina!? Kiarabu je?! Kifaransa na Kireno!!! Au wewe upeo wako umegota kwenye Kiingereza na kujivunia lugha isiyo yako kwa asili!!

Nikuarifu kuwa Afrika Kusini wanawachukua wakenya kuwafundisha Kiswahili si kwa sababu Kenya ni wazuri katika Kiswahili kuliko Tanzania, bali kwa kuwa mna matumizi ya Kiingereza zaidi yetu, hivyo mnayo nafasi bora zaidi ya kukitumia Kiingereza kufundisha Kiswahili kile chepesi kabisa (Simple Swahili for foreign learners). Kiswahili cha kuombea maji ili usife kwa kiu. Kiswahili haswa kipo Tanzania, kikihitajika tutahitajika.
 
Ahsante mtungi wa hekima
 

Utakua umesoma mstari wa kwanza wa bandiko langu na kukimbilia kujibu kwa mihemko, tulia urudie taratibu nilichoandika, usome neno kwa neno na kutafakari, kisha uje tujadii kwa hekima.
 
Kwamba simu yako ina king'amuzi cha kuona macho yangu yalipoishia kusoma... Utakuwa na malaria wewe sio bure.
Utakua umesoma mstari wa kwanza wa bandiko langu na kukimbilia kujibu kwa mihemko, tulia urudie taratibu nilichoandika, usome neno kwa neno na kutafakari, kisha uje tujadii kwa hekima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…