MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kuna uzi nilianzisha kuhusu taarifa za Kenya kuingia mkataba na Afrika Kusini ili kuwasaidia kuzindua elimu ya lugha ya Kiswahili kwenye mtaala wao. Kuna Watanzania wametiririka kwa povu za kiajabu huku wakijinadi kwamba wao ndio wamiliki wa hii lugha na hao ndio waliopaswa kualikwa wakaifunze, ila cha kushangaza, hao hao Watanzania ukisoma humo uandishi wao wa Kiswahili unatia huruma na ukihoji wanakuambia hawana haja ya kuzingatia Kiswahili sanifu.
Unakuta mtu anajisifu jinsi alivyoganda kwenye Kiswahili pekee na hataki kujiongeza kwenye lugha nyingine, ila hicho hicho Kiswahili hakitendei haki, anaandika upupu mtupu, Kiswahili kibovu kupita maelezo.
Watanzania mnatia huruma mjue, mnazembea hamtaki kujifunza Kingereza, pia lugha zenu za asili mumezitelekeza, madogo wengi hamzijui hata salamu, kazi yenu kuvaa milegezo na kushobokea wasanii mjini mjini, halafu Kiswahili hamtaki kujiboresha, uandishi wenu wa ovyoo, ni janga la taifa lakini kama mbuni mumefukia vichwa vyenu na kuanika maeneo mengine yote.
Watanzania wengi kazini ukiwaomba waandike taarifa/ripoti kwa Kingereza hawawezi, ukiwaagiza basi waandike kwa Kiswahili halafu utatafsiri mwenyewe hapo ndio utashangaa kitu watakachokuandikia, mtu hazingatii alama za uandishi, matumizi sahihi ya misamiati n.k. Kiswahili kibovu hadi kinatia hasira.
Sio kwamba najisifu wala kuwasifu Wakenya kuwa tunajua Kiswahili kuwazidi Watanzania, ila ni kwamba wengi tunapambana kujiboresha kila siku, kuyakubali mapungufu yetu na kuyafanyia kazi, mimi binafsi tangu nikiwa mdogo nilipenda sana kusoma gazeti la Taifa Leo ambalo huandikwa kwa Kiswahili, nia na lengo lilikua kujifunza jinsi ya kutumia hii lugha ipasavyo.