Watanzania wengi mnatia huruma kwenye uandishi wa Kiswahili

Nimependa mada yako japo imekaa kichokozi ila yapo ya kweli ulitoyagusia hapo... Ila ukweli ulio uchi ni kuwa watanzania wanakijua kiswahili vizuri zaidi kuliko wakenya lakini Wakenya ni watafutaji (aggressive) sana wa nafasi kuliko watanza... So nyie mnapata sio kwa sababu ya kukijua bali kwa kufosi kingi
 
Una Kiswahili kizuri kweli kama sio mkenya.

Ila ni ukweli usiopingika kuwa lugha ni tatizo kwetu watanzania wengi. Kiingereza hatujui,lugha zetu za kikabila hatujui lakini pia kishwahili ni changamoto kuanzia kuzungumza hadi kuandika.
 
Sitaki kukuwekea wasiwadi juu ya uwezo wako wa kupambanua mambo na kujenga hoja KAMA ni MSOMI kikawaida shida ya matumizi R na L sio kosa la kiufundishajibnintatizo la kibioojia ulimi kushindwa kutamka herusi R na L
Naelewa hilo vizuri sana. Hata Kenya watu wana shida ya matamshi. Binafsi sijawahi zungumza kiswahili maana kutamka maneno ni shida.
Tatizo nyie mnaandika tu vile mnavyozungumza.
Shure badala ya shule
Tafazari ----tafadhali
Burret tlain - bullet train
e.t.c
 
Hebu pitia kwanza blog zenu uone kama mnastairi kualikwa huko south afrika kufundisha kiswahili
 

Nilivyosoma kwa makini na kutafakari hizi aya zako, najiuliza kuhusu kiwango cha elimu cha watu unaokutana nao. Maana haingii akilini mhitimu wa ngazi ya shahada au stashahada ashindwe kuandika taarifa rasmi na kwa ufasaha kwa lugha adhimu ya kiswahili achia mbali lugha ya kiingereza.
 
Vijana wadogo wengi wa kitanzania wana tatizo kubwa la lugha ya kiswahili.

Umeongea ukweli kuhusu lugha.

Naona hata vijana wadogo wa kikenya kiswahili chao ni kibaya.
 
Kumbe mtoa mada ni mk 254 mental disability.Acha wenye akili kama zako waje.
 
Ila Jeni Kiswahili generally tunawapita.....

Japo tuna shida ya R na L sana,ila aisee hapa kwa Kiswahili nyie mna matatizo mengi zaidi

Mother tongues zinasumbua kotekote ila kwenye hasa Kenya interior ni balaa zaidi.

Itoe Mombasa kabisa,wapo elite level za Zanzibar na Dar-es-Salaam.

Hapa kiukweli kabisa,Kenya tumewaacha parefu!
 
Nakataa hakuna mkenya anaeweza andika kiswahili sanifu kwa usahihi kabisa . Nakataa nakataa hata Kenyatta tu na Ruto no shida hata hata ongea zao .

Wewe mwenyewe huo uandishi wako na hio lafudhi yako umeipata baada ya kukaa bongo kama sio kutembelea bongo sana .

Ushahidi upo hapa wakenya wenzako wanaandika pumba tu humu .

Hahahahahah MK254 unachekesha
 
Hamna sehemu nimejisifia kukijua Kiswahili zaidi ya Watanzania, nimesema huwa napambana kujiboresha kila siku narekebisha mapungufu yangu, ila nyie mpo mpo tu, hamtaki kujiongeza wala kukosolewa.
Sasa sisi tumezaliwa nacho turekebishe wapi hahahah
 
Kufikiri kuwa ni lazima kutumia lugha fasaha kila sehemu nao ni ujinga, et maandiko ya jf yanakufanya uhitimishe kuwa watz hawajui kiswahili, ongea uongeavyo lakin usilinganishe kiswahili kibovu cha kenya na cha TZ, mnaweza kutushinda kwenye vitu vingi lakini kwa lugha ya kiswahili mtasubiri sana mkuu, nafasi mliyopata ni kwa sababu tu viongozi wetu wamefeli katika kupambania fursa nje ya mipaka yetu wapo wanapambana na upinzani
 
Poleni
 
Jeni niaje?

Uko poa?
I am fine. Thank you.
Hili nalo halina ubishi. Watanzania wanajua kiswahili kuliko wakenya. Lakini kiswahili kinachofundishwa Kenya ni kama hiki chenu tofauti ni kuwa walimu wa tzedi hawajui kutofautisha r na l.
Wakenya hawazingatii ngeli wanapoongea kama nyie.
Kitabu yangu badala ya kitabu changu
 
Mim hapo tu kwenye kufukia kichwa na kuacha sehem zingine ndo pamenikwaza
 
Unajua maana ya kituko?? ulichoandika ni maana halisi ya kituko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…