Watanzania wengi tumejikatia tamaa, tunaishi kwa kutegemea mikeka itiki

Watanzania wengi tumejikatia tamaa, tunaishi kwa kutegemea mikeka itiki

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Kiukweli zama zimebadilika sana, kwa sasa Watanzania wengi tunaishi kwa kutegenea mikeka.

Wanaume majumbani kwetu ndio usiseme, wife ukiona anakuzonga zonga unamwambia kuna mchongo huo naufukuzia ukitiki tu mambo yatakuwa poa kumbe mtu mzima una mkeka wako wa siri unangoja Odds ziteme.

Vijana wahitimu wa vyuo wanalialia tu mkeka wa Tamisemi ndio tumaini lao, Mkeka wenyewe ngumu kumeza umeweka timu kibao unangoja utiki.

Wakati vijana wengine wao nao hawana matumaini zaidi ya kungoja mkeka wa teuzi kelele nyingi mitandaoni kuliko kazi. Tofauti sana na zamani.

Sijuhi kwanini tumefikia hapa
 
Ila me nilishaamua furaha yangu usiwe pesa
Mkuu acha kabisa usiombe kuishiwa.. nilikuja mkumbuka yule msanii Joh Makini alie sema "japo pesa ndiyo kila kitu " kwenye songi lake la chochote popote.

Hivi bila pesa hiyo furaha ina kuja vipi kwa mfano.

Labda uwe unaishi kwa baba na mama halafu ni kula na kulala na ukitaka kupiga mashine uwe una piga beki 3 wa nyumbani hapo, kwa mchongo huo hapo ndiyo inabidi uchague furaha yako sio pesa acha kabisa.
 
Back
Top Bottom