Watanzania wengi wana msongo wa mawazo (stress) kwasababu hawafanyi Utalii wa ndani

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (56)✍️
Unaishi miaka 70 mpaka unakufa hujawahi hata kuzunguka maeneo yaliyopo ndani ya nchi yako (Tanzania) ambayo yataifurahisha akili yako. Si kwamba huna hela, bali unaendekeza sana mambo ya hovyo kuliko mambo mengine mazuri.

Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii na maeneo mengi ya kufanya utalii. Lakini ajabu sana wageni kutoka nje wanaijua Tanzania kuliko watanzania wenyewe.

Si kwamba watanzania hatuna hela za kufanya utalii wa ndani - watanzania wengi tuna hela lakini tunapenda sana kutumia hela zetu kwenye starehe za kuumiza akili na miili yetu kama vile unywaji wa pombe, ngono, uvutaji wa moshi, matumizi ya madawa ya kulevya, sifa za kununua magari, simu za gharama, nguo za gharama, n.k.

KWA MFANO;
✓ Wapo watanzania wanaoishi kule Moshi na Arusha hawajawahi hata kuusogelea MLIMA KILIMANJARO - lakini kutwa wapo kulipa Bills za pombe wanazokunywa kila siku.

✓ Wapo watanzania wanaoishi kule Mlowo, Vwawa, Tunduma, Iyula, & Ileje katika Mkoa wa Songwe hawajawahi kufika kwenye KIMONDO kilichopo kijiji cha Ndolezi - lakini kutwa wapo kutumia pesa nyingi kwenye pombe kwenye Grocery za Mpemba na Tunduma.

✓ Wapo watanzania wanaoishi kule Kiomoni, Amboni, Mabokweni, na Tanga mjini katika Mkoa wa Tanga hawajawahi hata kufanya utalii wa kuingia kwenye MAPANGO YA AMBONI - lakini kutwa wapo kugharamia ngono kwenye mahoteli ya gharama.

✓ Wapo watanzania wanaoishi kule Songwe Kiwandani, Mbalizi, na Mbeya mjini katika Mkoa wa Mbeya hawajawahi kutembelea eneo la MAPANGO NA MAJI MOTO ya Kijiji cha Nanyara - lakini kutwa wapo kunywa pombe kule Canivo, Mbeya Pazuri, n.k

✓ Wapo watanzania wanaoishi kule Mikumi na Morogoro mjini katika Mkoa wa Morogoro hawajawahi kutalii kwenye MBUGA YA WANYAMA - lakini kutwa wapo kununua simu za gharama ili wazitumie kutafutia mabwana na wasichana.

✍️Watanzania hatupendi kufanya utalii wa ndani ili kuweka vizuri akili zetu, tunatumia pesa nyingi kufanya mambo ambayo yanasababisha tatizo la afya ya akili, ndo maana "homa kidogo" tunakimbizwa India kutibiwa - tuna stress nyingiiiiiiii.

Right Marker
Dar es salaam.
images (15).jpeg
Kimondombozi.jpg
 
tatizo umaskini watanzania wengi furaha yao ni mateso kwa watu wenye exposure kama sisi yan what we call suffering ndo furaha yao

kushinda vijiweni,vibanda umiza n.k
 
Njaa kali
 
Kufanya utalii kunahitaji kipato,,sasa watanzania wanavipato gani vya Kufanya utalii?watanzania wanapata stress sababu ya maisha magumu,,ila wanajikaza tu
 
Back
Top Bottom