Watanzania wengi wana tatizo la uelewa na ufahamu (upeo mdogo). Hii inawapa mwanya wajanja kuwatapeli kirahisi

Futa uongo wako huo naonaga unacopy taarifa mbali mbali lakini ukitumia taarifa zako mwenyew kwa utashi huna kitu unapelea YULE MWIZI ALIIBA KWA MWANAJESHI SURGENT ANA VII 3 na tukio lilitokea mlandizi.... Na jamaa alilia na police tulifuka wapi mwisho bi mkubwa alifingua zipi ya kijana akapona na wameenda mbali HAPO HAPO MLANDIZI KUNA MWANAJESHI MSTAFU ALINASA KWA KADADA AMBAE JAMAA YAKE NI MVUVI wakagandiana vibaya UNAJUA TEGO WW LA WAZARAMO, WANDENGEREKO WATU WA TANGA kwa kuwa bado hujakua unajipa visifa vya kujikubali endelea karibu NERO
 


Illusion and delusion. Acha kuamini mambo ya uongo.
 


Babu wa loliondo aliletwa na serikali ili kuziba pengo la mgomo wa madakitari.

Hakuna MTU yeyote aliyepona baada ya kunywa kikombe .
 
Tafsiri ya neno UJINGA sehemu hii inatumika vibaya.

Ndio maana hata wasomi wanaojua hiki ulichokiandika hapa zaidi yako mara 5,walikwenda kule au kwa nabii yeyote unayemuona ni tapeli.

Labda neno linalokaribiana kufafanua hayo ni USHAMBA,ambalo nalo halisadifu asilimia zote.
 
Ni kweli kabisa
 
Illusion and delusion. Acha kuamini mambo ya uongo.
Papa wa baharini hajui kabisa kama kuna kiumbe kuku,na akiambiwa huwika saa 4:00 atabisha mnooo.

Inabidi tu tuwe tunakubari kutokuelewana.
 

Mtu kusoma haimaanishi hawezi kutapeliwa, kudanganywa.

Mtu asiyedanganywa ni yule mwerevu, asiye na tamaa na asiye mvivu.

Nazungumzia ishu ya utapeli, ulaghai au uongo.
Matapeli hutumia udhaifu wa upeo mdogo wa mtu kuhusu jambo Fulani, au tamaa ya mtu kuhusu jambo Fulani kama chambo, au uvivu wa kufuatiliwa.

Matatizo ya mtu hayana uhusiano wowote na kutapeliwa
 
😁😁😁hivi mkuu unatafakari unachoandika???matatizo ya mtu hayahusiani na..............

Mimi sikuombei upate matatizo ili ukatapeliwe ujifunze,hapana.

Umeshawahi kushuhudia mtu anaumwa na hospital hawaoni tatizo akiwa na imani,uelewa na elimu ya kutosha na bado anakubali kwenda kutizama NAMNA nyingine(waganga).
 
Binadamu hukua mpaka dakika yake ya mwisho
Ila suala la Ukweli haliangalii mtu kakua au hajakua. Ukweli ni Ukweli tuu.
Nasisitiza,ENDELEA KUKUA.

Siku moja utajua pia hata ukweli husimama kutegemea na point ulipo.9 inawezakuwa 6 kutokana na upande,na wote tukakubaliana ni sahihi kwa kila upande.
 
Nasisitiza,ENDELEA KUKUA.

Siku moja utajua pia hata ukweli husimama kutegemea na point ulipo.9 inawezakuwa 6 kutokana na upande,na wote tukakubaliana ni sahihi kwa kila upande.

Ukweli ni Ukweli siku zote. Ukweli hauangalii mazingira labda kama hujui maana ya Ukweli.

Sawa naendelea kukua, nawe endelea kukua katika Ukweli
 

Kwa hiyo wewe ukiumwa alafu mtu akakuambia ili upone unatakiwa kuingiziwa uume, utakubali?

Matatizo yapo, lakini sio sababu ya kuwa na upeo Mdogo.
Yaani kwa Lugha nyepesi ni kuwa, wewe kuwa na matatizo hakukufanyi uwe na upeo Mdogo wa kufikiri.

Na wala wewe kuwa na utajiri hakukufanyi uwe na upeo mkubwa wa uelewa. Ndio maana unaweza kuwa huna matatizo na ukalaghaiwa kwa sababu ya tamaa.

Wewe nafikiri katika kujadili mada hii kuna sehemu huelewi, sijui unafanya kusudi au ni kweli hauelewi.

Mfano wale wanawake wanaodanganywa na waganga wa kienyeji kuwa dawa inatakiwa iingizwe kwa uume sehemu zao za siri, wakakubali. Ni matatizo yao au ni upeo wao wa akili kuwa finyu?

Najaribu kuelewa hoja zako, lakini nashindwa. Au labda Mimi mbishi
 
Mkuu unawakumbuka Wasabato Masalia waliotaka kwenda kuhubiri Gombo huko Ughaibuni bila kuwa na tiketi ya ndege wala Passport ya kusadiria eti Passport yao ni Biblia? Tena unaenda kuhubiri kwa Waliotuletea Dini eti Masalia tuwaweke kundi gani?
 
Popote pale duniani wajinga ni wengi kuliko werevu sio Tz tu.
 
Nchi hii ina wajing wengi sanaaa

Ova
 
Kwa hiyo wewe ukiumwa alafu mtu akakuambia ili upone unatakiwa kuingiziwa uume, utakubali?
Tezi dume inapimwa kwa kuingizwa kidole,unadhani waliopimwa waliandika barua ya maombi ili waingiziwe hivyo vidole???
Matatizo yapo, lakini sio sababu ya kuwa na upeo Mdogo.
Yaani kwa Lugha nyepesi ni kuwa, wewe kuwa na matatizo hakukufanyi uwe na upeo Mdogo wa kufikiri.
Upeo mdogo wa kufikiri unaupimaje??wakati wa dharula!!!hivi gari ikikata break mteremkoni inahitaji dereva mwenye upeo kiasi gani kutopindua gari??jibu kwa rejea ya udereva wa keybod😄sio barabarani zingatia.
Na wala wewe kuwa na utajiri hakukufanyi uwe na upeo mkubwa wa uelewa. Ndio maana unaweza kuwa huna matatizo na ukalaghaiwa kwa sababu ya tamaa.
ndio sababu nikaandika ni matatizo hufanya watu kukosa utulivu mpaka kufanya mambo ambayo sio ya kawaida kabisa.
Wewe unajua matatizo ya wanawake mkuu🤭🤭,au tunapiga tu soga hapa!!!!

Najaribu kuelewa hoja zako, lakini nashindwa. Au labda Mimi mbishi
Haaya mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…