Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Tutake ama tusipende English ni muhimu sana na kuna ulazima wa kuifahamu hii lunga hata kwa bakora esp. huko tunakoelekea.kwa ambao mmeenda chuo na mnaotarajia kwenda chuo nje ya Tanzania naomba mkazane sana kwenye English ya kuongea na kuandika.
nilishuhudia watu toka tanzania wakitia sana huruma kwenye presentation. wanaongea english mbovu sana adi inapelekea wakose ujasiri wa kusimama mbele.
jambo ilo lilinisikitisha sana kwa mtanzania kushindwa wakat wengine niliosoma nao toka china. mexico, said arabia, qatar,malaysia etc walikuwa wanajitaid japo walifundishwa secondary kwa lugha zao za ndani.
wito wangu kwa mnaosoma na mnaoenda chuo. English ni lazima ujue
Mkuu hebu fafanua manake sijakuelewa hapaAlafu tabia ya watanzania wanaoenda kusoma collage huko ughaibuni wakija hapa wanasema wamesoma university waacheee,wanaoenda kusoma ughaibuni wachache ndio wenye uwezo waliwengi hupewa nafasi kwa kujuana,ua uwepo wa pesa home
Hahahaha,
Umenikumbusha enzi zangu.
Mwaka wa kwanza nilimletea mzozo Profesa wa Philosophy na kelele za atheism/ far left, mpaka ikawa noma kama nataka ku dominate darasa.
Kila siku ligi darasani, si miswali, mwalimu neocon far right libertarian halafu judge and author, mie super liberal leftie atheist, total opposites. Nikaona huyu siku ya mtihani wa mwisho lazima anifelishe, lakini namtilia ngumu.
Kufika wiki ya mtihani wa mwisho wa semester kaniambia "wewe usije kwenye mtihani, class participation yako ishakupasisha darasa".
Nikamuuliza sasa utanipimaje? Utanipa maksi gani?
Akaniambia ubishi wako wa darasani kila siku na coursework ushapata A kwenye somo langu, ule ubishi ulikuwa umezama kwenye falsafa kubwa kuliko ya darasa hili. Mimi nilikuwa naona ule ubishi kama naharibu, kumbe kinyamwezi mwanafunzi mbishi vile ndio anaonekana anafuatilia mambo. Mwalimu anasema you did your readings, bila kusoma usingekuwa na cha kubisha. Na ulikuwa unatoa classic arguments.
Nikaona kweli mnyamwezi hana hiyana, bongo ukibishana na profesa darasani si anakufelisha kabisa?
Kwa hiyo nashukuru mimi sijawahi kuwa na tatizo la presentation na kujieleza.
Kama kuna wabongo wengi wana tatizo hilo, tupo wengine tunawakilisha.
Heri yetu sie wabeba maboksi proper. Hatuna mambo ya kuwasilisha mada wala term paper.
Ni mambo ya kupinda mgongo tu na yes - no, bhaaaas.
Kila Ijumaa ikifika unaenda zako kuchukua paycheck yako halafu huyo...destination Walmart MoneyCenter kui-cash.
Alafu tabia ya watanzania wanaoenda kusoma collage huko ughaibuni wakija hapa wanasema wamesoma university waacheee,wanaoenda kusoma ughaibuni wachache ndio wenye uwezo waliwengi hupewa nafasi kwa kujuana,ua uwepo wa pesa home
Kupiga box kuna expiry date boss, na ukumbuke kurudi home, nyumbani ni nyumbani naimagine kutunzwa nursing homes za wazee ni soo!!
Usipotoshe watu. Hakuna aliyesema lugha ya kiingereza haina umuhimu. Kwa dunia ya leo ni muhimu sana lakini hiyo haifanyi tuidharau lugha yetu. Tunachotakiwa kufanya tuimarishe ufundishaji wa lugha ya kiingereza na kiswahili pia. Ni kweli nchi nyingi zilizoendelea zinatumia lugha zao wenyewe. Mfano Uingereza, Ujerumani, Italia, China, Japan, Uturuki n.k. Tuufute UTUMWA wa mawazo kwenye fikra zetu. Hakuna lugha iliyo bora duniani.Tutake ama tusipende English ni muhimu sana na kuna ulazima wa kuifahamu hii lunga hata kwa bakora esp. huko tunakoelekea.
Kuna maimunas watakaokuja kutoa povu hapa na kukwambia kuwa eti kwa nini tutumie lugha ya mkoloni sababu huo ni ukoloni wa fikra. Wataendelea kuja na hoja ooh mbona China wanatumia Chinese kila mahali. Subiri tu.
Halafu Mungikis, Popos na Ankoles wakija kuchukua ajira zenu kwaajili ya umaimuna mnalia.
Nunueni hata Rosetta Stones ikibidi. Ushindani unakuja na tutaachwa
Usipotoshe watu. Hakuna aliyesema lugha ya kiingereza haina umuhimu. Kwa dunia ya leo ni muhimu sana lakini hiyo haifanyi tuidharau lugha yetu. Tunachotakiwa kufanya tuimarishe ufundishaji wa lugha ya kiingereza na kiswahili pia. Ni kweli nchi nyingi zilizoendelea zinatumia lugha zao wenyewe. Mfano Uingereza, Ujerumani, Italia, China, Japan, Uturuki n.k. Tuufute UTUMWA wa mawazo kwenye fikra zetu. Hakuna lugha iliyo bora duniani.
Kiswahili ni kigumu, mi sjakuelewa boss
Mkisoma college msiseme mmesoma university ndo analomaanisha!!!!!