Hahahaha,
Umenikumbusha enzi zangu.
Mwaka wa kwanza nilimletea mzozo Profesa wa Philosophy na kelele za atheism/ far left, mpaka ikawa noma kama nataka ku dominate darasa.
Kila siku ligi darasani, si miswali, mwalimu neocon far right libertarian halafu judge and author, mie super liberal leftie atheist, total opposites. Nikaona huyu siku ya mtihani wa mwisho lazima anifelishe, lakini namtilia ngumu.
Kufika wiki ya mtihani wa mwisho wa semester kaniambia "wewe usije kwenye mtihani, class participation yako ishakupasisha darasa".
Nikamuuliza sasa utanipimaje? Utanipa maksi gani?
Akaniambia ubishi wako wa darasani kila siku na coursework ushapata A kwenye somo langu, ule ubishi ulikuwa umezama kwenye falsafa kubwa kuliko ya darasa hili. Mimi nilikuwa naona ule ubishi kama naharibu, kumbe kinyamwezi mwanafunzi mbishi vile ndio anaonekana anafuatilia mambo. Mwalimu anasema you did your readings, bila kusoma usingekuwa na cha kubisha. Na ulikuwa unatoa classic arguments.
Nikaona kweli mnyamwezi hana hiyana, bongo ukibishana na profesa darasani si anakufelisha kabisa?
Kwa hiyo nashukuru mimi sijawahi kuwa na tatizo la presentation na kujieleza.
Kama kuna wabongo wengi wana tatizo hilo, tupo wengine tunawakilisha.