Yes and no, Ni kweli kuwa SA usalama umezorota karibia kila mahali, ila huwezi kulinganisha maeneo kama limpopo na cape town, na hata ndani ya miji kuna mitaa hatari kuliko mengine, currently maeneo ya cape town kama Mitchells plain na vitongoji vyake kama cape flats,elsies river, bishop lewis, hanover park, valhalla nk ni hatari kuliko sehemu nyingine yoyote ndani ya SA, jana tu mtoto wa miaka mitano amepigwa risasi ya kichwa huko hanover park, imagine, na pale vita among gangs ndiyo vinavyogharimu maisha ya watu wengi, kuhusu vita ya kibiashara nadhani wahanga wakubwa ni pakistanis, hao wanauana hata wao kwa wao kwa wivu wa kibiashara, ndiyo maana mitaa yenye biashara nyingi za wa pakistan zinaongoza kwa drive by shooting, yaani mtu anapita tu anakutandika risasi hashuki hata kwenye gari,anaenda zake, KZN (Durban etc) inaongoza kwa utekaji wa cash vans( CIT robbery) gauteng ni kidnapping hub.