Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

Screenshot_20240929-105741_Rifaly.jpg

Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
 
Watanzania wako na uwezo mkubwa wa kuendesha haya mashirika ya umma. Hawa ni watu waliotulia na wenye akili, shida inakuja kwa Mtawala, anataka achukue wa kutoka kenye chama, anayemlambalamba.

Hawa watu wenye uwezo huo, hawako kwaaajili hiyo. Wako kikazi zaidi na si uchawa. Wako kwenye level zingine, za kutaka Taasisi iendelee na kuleta faida. Tulionao mpaka hizo Taasisi zinakufa, wengi wamewekwa hapo kwa uchawa, zawadi ya cheo, kujuana n.k.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Kwenye "Entrepreneurship," (elimu ya ujasiriamaliz) tunajifunza namna ya kufanya biashara na siyo kuhusu biashara. In entrepreneurship we learn how to do business not about business . Hoja ni kwamba inawezekana wanaopewa dhamana wanaujuzi kuhusu biashara tu, kama huna tabia ama hata sifa moja ya ujasiriamali huwezi kufanya biashara yoyote ile
 
Mimi huwa nacheka yaani shirika la kibiashara, Rais anateua Jaji Mstaafu au Jenerali Mstaafu wa Jeshi kuwa Mwenyekiti wa bodi ili akasaidie nini!!
Ukiingia kule LinkedIn Kuna Watanzania wabobezi wengi tu,inashindikana nini kuwateua waendeshe Mashirika yetu????
 
Ukishaifanya siasa kuwa ni biashara inayolipa basi tambua kila kitu kitapitia kwenye siasa na kuwa biashara.

Private business, ni strictly business, wanahitaji faida na efficiency, unapohitaji vitu hivyo unahitaji watu wenye competence, skills, knowledge na exposure.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali

Wewe umeongea vizuri tuu watz wenye uwezo wa ku-run business tupo wengi tuu.ila siyo kwenye taasis za serikali Siyo Zile zinazoitwa Government Business Entities "GBE"

Huko wanafundishwa coruption na wanasiasa ambao ndiyo wasimamizi wakubwa.Waziri wa wizara husika kila siku anataka apewe fedha.Hata miradi tuu ya maendeleo inakwama hapo.yaani mawaziri unawaona mqjukwani kama watu wa maana ila ni wa hovyo sana inqookuja kwenye maadili

Maahirika haya yote yanayofanya biashara
ikiwezekana hata vyuo vikuu yalitakiwa yote yasiwe chini ya wizara yoyote,ila yawe labda chini ya wizara moja tuu ya fedha chini ya Treasury Registra.
usumbufu wa wanasiasa ndiyo unaou mashirika.

Kingine ilibidi nafasi zao zitangazwe na wapewe wasimamizi huru wa usaili( Independent Hiring Consultancy company)

Vinginevyo ni ujinga mtuupu na hasara tupu.mgao wa kwenda serikalini kama faida watakuwa wanamega mtaji wala siyo faida
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Miongoni mwa sababu ni pamoja na ile iliomtengua Tido Mhando TBC. Mashitika ya umma hayawezi kutengeneza faida, hata magereza haiwezi kulisha wafungwa, japo haiwalipi mishahara, na inawapa mlo mmoja na nusu kwa siku.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Kaka Paskali, asante sana kwa andiko hili. Niseme machache ya kwanini hutawaona watanzania kwenye nafasi za juu za makampuni makubwa hapa nchini..!!

1. Imani kwamba industry flani ni mpya Tanzania
Kuna nyakati, mambo ya madini, simu wakati yanaanza, etc vilikuwa vinaonekana na kutajwa kwamba ni mambo mapya kwetu. haya yalisemwa na almost wote, kuanzia wawekezaji, viongozi serikalini na mpaka watendaji wakuu wa sekta husika. Hii ilipelekea, kweli kila kitu kionekane kipya kwetu watanzania. Lakini, pampu ya maji iliyokuwepo pale Kahama KMCL (kwenye makinikia) haina tofauti na ya DAWASCO, au genereta lililokuwepo pale kwenye mnara wa simu wa Mkuranga, halina tofauti na genereta la nyumbani kwa mtu. Mtazamo wa upya, ukapelekea kila kitu kionekane kipya na kinahitaji shule kubwa sana kukijua. Lakini kiuhalisia haikuwa hivyo. Kuna vilivyoikuwa vipya na vile tulivyowahi kuvifanyia kazi kwingine.

2. Proper succession plan
Kaka, tushawekwa sana kwenye succession plans ili uweze kumrithi mzungu. Lakini, sera zetu zinawabeba sana wazungu kwenye kuelimisha watanzania halafu wachukue nafasi wakifikisha uwezo. Mtu unakaa kwenye plan hiyo, lakini plan haina mwisho. Sera zetu hazitoi nafasi kwa watanzania kurithi nafasi kubwa. Mwisho mtu anakuwa frustrated na anaamua kuondoka.

3. Imani yetu kwa wazungu
Kuna watu wanawaamini sana wazungu. Mzungu nakisema kitu kinaonekana cha maana sana kuliko cha mbongo. Nyerere ashshawahi kusema, kuna wengine kitu kikitajwa kwa kiingereza kinaonekana cha maana sana kuliko uhalisia wake. Lakini nikuambie, nilishawahi kufanya kazi na mzungu, jina lake kuandika ilikuwa ni ishu. Ni hawa MINEBOY wa Sauzi. Kakulia kwenye spana kama msaidizi wa babaake mgodini. Mwisho wasiku shule haitaki.

4. Majungu tunayopigana wenyewe kwa wenyewe
Kwenye majungu hatujambo. Kuna watu wakisikia tu fulani ana uwezekano wa kuchukua nafasi fulani, inakuwa hatari sana kwao. Watu wanahaha huku na huko kuhakikisha hicho kitu hakitokei.
 
Wakristo wanashika top ten ya matajiri wote Tanzania, watumishi wengi serikalini ambao ni wasomi wazuri ni wakristo,serikali haina ufisadi sababu wakristo ni wahaminifu kwa jina la yesu, Samia hadi 2040
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Kwenye telecom, hakuna blablabla, kama serikalini, huku issues zinatafutiwa solutions, anayeleta madudu anaadhibiwa fasta, maana ukiruhusu madudu, unakosa mapato,kampuni inakufa, kila mfanyakazi, anajua juhudi zake kuhakikisha hakuna fuckups, ndio kampuni inasonga mbele,
Serikalini, kwanza kuna politics nyingi, mtaani kwangu, senior retired civil servants, hawalipi bill za maji, wala umeme, wanatumia bureeee, serikalini, hata usipojishughrisha Sana, salary will come, ukitibua Sana, unahamishwa tu, hakuna "owner ship" Ya task Fulani, madudu y akitokea, hujui nani atumbuliwe, kuna mlolongo mreeefu wa protocali!
Telecom, kuna clear standard operation procedures SOP, ikitokea shida tu, aliyechemka, anaanza kuwajibika, kurekebisha, kabla Mambo hayajawa mabaya!
Tatizo linaweza likatokea kwenye mnara Kyelwa mrongo border, inaweza ikawa issue ya pesa kibao, itasoviwa kwa conference call btn wahusika, hakuna eti MTU atoke Dar aende ziarani kagera, kote huko kuna watendaji, mnazungumza kupitia conference call, aliyechemka, anapata adhabu halo halo, kama kibarua kinaota nyasi, ni, hapo hapo uamuzi, unatoka,! No time to waste
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Usiseme huko kwote tunahsinda,,huon CRDB,,NMB,,NBC zote Zina CEos wa kibongo na zinakimbiza kuliko za wazungu.Angalia pia Barric nao chini ya Mtanzania zinae da vizuri
 
Back
Top Bottom