Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

mkuu mayalla ,hawa HELIOS si ndio wenye umoja na MILICOM walioshilikiana na TIGO kumfuatilia RISU?
je kwenye kesi yao hawata husika kweli?
au hawa wanahusika na kusambaza minara tu mambo ya kutunza taarifa hayawahusu?
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Moja ya kitu naona kwenye nchi yetu

Ni fikra za kijamaa ziliathiri sana watanzania wengi kuanzia kwa Viongozi wetu Hadi kwa wananchi

Viongozi kuamini serikali inaweza kuendesha Kila kitu haswa miradi ya kiuchumi na Biashara na wakati huo huo watoze Kodi ni fikra hasi ya kijamaa

Na wananchi vile vile wanaamini serikali kuchukua nafasi kubwa ya Kusimamia uchumi wao na sio wananchi kuwajibika Kusimamia uchumi wao

Mfano mzuri ni mashirika na viwanda vingi vilivyoasisiwa kipindi Cha ujamaa vingi vilikufa na vilivyobaki ni hasara

Bahati mbaya Viongozi wetu wengi hawajifunzi makosa yaliyopita bado wanataka kuaminisha wananchi kwamba serikali inaweza kuendesha miradi Kama HUDUMA

Nilisikitika niliposikia TRC ndio itaendesha SGR kutoa huduma nikajua ni suala la Muda tu

Embu fikiri Viongozi wanajivunia kukopa Tena Mabasi ya mwendokasi Leo mradi unakaribia miaka kumi

ukiwa na wateja wa kutosha Hadi inawaacha barabarani

Lakini umeshindwa kujiendesha kwa faida

Mradi wa mabasi Kuna watanzania wanaendesha vizuri tu wenyewe Tena kwenye maeneo yenye competition kubwa .
Tena wengine ni mtanzania tu mwenye Elimu yake nzuri ya la Saba , Ila Kila mwaka mradi wenyewe unakuja na kuongeza mabasi
 
Kaka Paskali, asante sana kwa andiko hili. Niseme machache ya kwanini hutawaona watanaznia kwenye nafasi za juu za makampuni makubwa hapa nchini..!!

1. Imani kwamba industry flani ni mpya Tanzania
Kuna nyakati, mambo ya madini, simu wakati yanaanza, etc vilikuwa vinaonekana na kutajwa kwamba ni mambo mapya kwetu. haya yalisemwa na almost wote, kuanzia wawekezaji, viongozi serikalini na mpaka watendaji wakuu wa sekta husika. Hii ilipelekea, kweli kila kitu kionekane kipya kwetu watanzania. Lakini, pampu ya maji iliyokuwepo pale Kahama KMCL (kwenye makinikia) haina tofauti na ya DAWASCO, au genereta lililokuwepo pale kwenye mnara wa simu wa Mkuranga, halina tofauti na genereta la nyumbani kwa mtu. Mtazamo wa upya, ukapelekea kila kitu kionekane kipya na kinahitaji shule kubwa sana kukijua. Lakini kiuhalisia haikuwa hivyo. Kuna vilivyoikuwa vipya na vile tulivyowahi kuvifanyia kazi kwingine.

2. Proper succession plan
Kaka, tushawekwa sana kwenye succession plans ili uweze kumrithi mzungu. Lakini, sera zetu zinawabeba sana wazungu kwenye kuelimisha watanzania halafu wachukue nafasi wakifikisha uwezo. Mtu unakaa kwenye plan hiyo, lakini plan haina mwisho. Sera zetu hazitoi nafasi kwa watanzania kurithi nafasi kubwa. Mwisho mtu anakuwa frustrated na anaamua kuondoka.

3. Imani yetu kwa wazungu
Kuna watu wanawaamini sana wazungu. Mzungu nakisema kitu kinaonekana cha maana sana kuliko cha mbongo. Nyerere ashshawahi kusema, kuna wengine kitu kikitajwa kwa kiingereza kinaonekana cha maana sana kuliko uhalisia wake.

4. Majuku tunayopigana wenyewe kwa wenyewe
Kwenye majungu hatujambo. Kuna watu wakisikia tu fulani anauwezekano wa kuchukua nafasi, inakuwa hatari. Watu wanahaha huku na huko kuhakikisha hicho kitu hakitokei.
Je sisi tuna proper succession plan endapo rais aliyeko madarakani akipata majanga hasa kifo?, samahani kama nawatoa kwenye reli lakini lengo ni kujenga nyumba moja kwaajili ya huko baadae
 
Tatizo ni uthubutu kuomba kazi kampuni za kimataifa ndio maana hata Pascal Mayala anayejiita mwandishi wa habari nguli uswahilini Tanzania anaishia tu kuandika vihabari uchwara vya ndani ya nchi vyombo vya habari vya ndani hajawahi ajiliwa BBC au Voice of America nk kama akina Kikeke nk ambao Mayala kawazidi qualifications kielimu tena mbali mno

Wenzie wamestaafu vyombo vya habari vya kimataifa wanalipwa monthly pensions kwa dola yeye anauza sura tu jamii forums na vigazeti vya uswahilini
 
Tatizo ni uthubutu kuomba kazi kampuni za kimataifa ndio maana hata Pascal Mayala anayejiita mwandishi wa habari nguli uswahilini Tanzania anaishia tu kuandika vihabari uchwara vya ndani ya nchi vvyombo vya habari vya ndani hajawahi ajiliwa BBC au Voice of America nk kama akina Kikeke nk ambao Mayala kawazidi qualifications kielimu tena mbali mno

Wenzie wamestaafu vyombo vya habari vya kimataifa wanalipwa monthly pensions kwa dola yeye anauza sura tu jamii forums na vigazeti vya uswahilini
Lakini hakai kimya, ni muhimu kujadili kuhusu jamii yetu ili kupata majawabu ya nini kifanyike kuwezesha kupiga hatua badala ya kuwaachia wanao ahirisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data kumbuka pia, "silence surrenders public responsibilities"
 
Wakristo wanashika top ten ya matajiri wote Tanzania, watumishi wengi serikalini ambao ni wasomi wazuri ni wakristo,serikali haina ufisadi sababu wakristo ni wahaminifu kwa jina la yesu, Samia hadi 2040
Nadhani unamaanisha Kinyume maana Zakaria, Patel, Gharib Salim Bilal, Said Salim Bhakresa hawa wote hawaingii kanisani. Just to mention a few.
 
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo.

View attachment 3110071
Huu ni muendelezo wa sisi Watanzania kujitathmini uwezo wetu wa uongozi kwenye corporate level, jee Watanzania tuna uwezo wa kuongoza makampuni makubwa profitability, kama ATCL, SGR, TAZARA etc na yaka oparate kwa faida.

Kampuni ya Helios Towers Tanzania ni Kampuni ya kimataifa ya Uingereza, iko kwenye nchi 8 barani Afrika na Oman Arabuni. CEO wa Helios Towers ni Mtanzania, Gwakisa Stadi ambaye pia ni Boss wa Helios Towers Kanda ya Afrika Mashariki. Kati ya hizo nchi 8 za Afrika ambazo Helios Towers wapo, Ma CEO 3 ni Watanzania na habari njema zaidi ni hata CEO wa kwanza aliyeanzisha Helios Towers Oman, ni Mtanzania!.

Huu ni uthibitisho kuwa Watanzania tunaweza!. Kama Watanzania wameweza kwenye Helios Towers, huko kuingine kote Watanzania tunashindwa nini?.

Paskali
Nchi walizoabzishia nalo muhimu
 
Tatizo ni uthubutu tu kuomba kazi nje au makampuni ya nje mbona wako watanzania ma CEO nje kama huyu

Massawe, Benki ya Kigali, benki kubwa ya Rwanda kwa mali, imemthibitisha Deogratius Massawe kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kitengo cha teknolojia, BK Techouse.

Deo alikuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kigali (BK) Techouse tangu Agosti mwaka 2023.

Kabla ya kuchukua wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji, aliwahi kuwa Afisa Mkuu wa Teknolojia (CTO) wa BK Techouse kwa miaka mitatu.

"Ninashukuru kushiriki kwamba nimeidhinishwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji (Mkurugenzi Mtendaji) wa BK Techouse.. Nimefurahishwa na fursa zilizo mbele katika sura hii mpya," Deo alisema kwenye LinkedIn.

BK Techouse iliyoanzishwa mwaka wa 2016 ni mmoja wa wahusika wakuu katika kuweka uchumi wa Rwanda kwenye dijitali.

Inatoa teknolojia ya ubunifu na huduma katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kilimo, teknolojia ya elimu na teknolojia ya fedha.

Ni mifumo ya malipo ya kidijitali ina zaidi ya watumiaji milioni 3.

Kabla ya kuhamia Rwanda, Deo (pichani) alifanya kazi nchini Marekani katika kampuni kubwa ya mawasiliano ya T-Mobile kwa zaidi ya miaka 14.

Alishikilia nyadhifa mbalimbali katika T-T-Mobile, ikiwa ni pamoja na Meneja Mwandamizi wa Bidhaa na Teknolojia na hapo awali alifanya kazi kama CTO/COO katika kampuni ya kuendesha gari ya Moovn.

Katika miaka yake ya mapema nchini Marekani, Massawe pia alifanya kazi kama mshauri mkuu wa IT wa Microsoft na mhandisi wa mfumo wa ndani katika IBM.

Ana MBA katika usimamizi wa biashara na habari za afya kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Georgia na Shahada ya Sayansi ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Washington.

yyyyy.jpeg
 
Mbona huzungumzii katazo la uraia pacha linavyopoteza watanzania wenye nia ya dhati kurudi kusaidia nyumbani.?

Wapo watu wengi tu wana nafasi kubwa sana katika nchi za watu ila waliamua kukacha utanzania ili wachukue fursa hizo na ndio nchi ikawa imepoteza asset .

Hata wale waliokuwa 50% -50% muda ulivyoenda nao waliona wakache uraia moja kwa moja maana waliojaribu kurudi walikutana na kauli za [maelekezo kutoka juu, hii huwa tunafanya hivi miaka yote "] sasa kwa mtu aliye na exposure kubwa hawezi kufit kwa watu kama hawa tofauti na hapo ndio ile ya kuamua kuweka akili pembeni na kufuata hayo niliyoyataja.

Swali lianzie kwanini Tanzania haitaki uraia pacha ?
 
Kwenye telecom, hakuna blablabla, kama serikalini, huku issues zinatafutiwa solutions, anayeleta madudu anaadhibiwa fasta, maana ukiruhusu madudu, unakosa mapato,kampuni inakufa, kila mfanyakazi, anajua juhudi zake kuhakikisha hakuna fuckups, ndio kampuni inasonga mbele,
Serikalini, kwanza kuna politics nyingi, mtaani kwangu, senior retired civil servants, hawalipi bill za maji, wala umeme, wanatumia bureeee, serikalini, hata usipojishughrisha Sana, salary will come, ukitibua Sana, unahamishwa tu, hakuna "owner ship" Ya task Fulani, madudu y akitokea, hujui nani atumbuliwe, kuna mlolongo mreeefu wa protocali!
Telecom, kuna clear standard operation procedures SOP, ikitokea shida tu, aliyechemka, anaanza kuwajibika, kurekebisha, kabla Mambo hayajawa mabaya!
Tatizo linaweza likatokea kwenye mnara Kyelwa mrongo border, inaweza ikawa issue ya pesa kibao, itasoviwa kwa conference call btn wahusika, hakuna eti MTU atoke Dar aende ziarani kagera, kote huko kuna watendaji, mnazungumza kupitia conference call, aliyechemka, anapata adhabu halo halo, kama kibarua kinaota nyasi, ni, hapo hapo uamuzi, unatoka,! No time to waste
watumishi wa umma wako kwenye luxury comfort zone hapo nchi ya gizani. usitegemee maajabu.
 
Mbona huzungumzii katazo la uraia pacha linavyopoteza watanzania wenye nia ya dhati kurudi kusaidia nyumbani.?
Ajira zinazolipa vizuri ni kampuni za kimataifa hizo hazijali uraia wa mtu ni hapa kazi tu ulichoandika ni nje ya mada

Mleta mada anaongelea watanzania kuwa ma CEO wa makampuni ya kimataifa sio ya ndani kama TRA au treni ya mwendo kasi au shirika la masoko la kariakoo nk
 
Back
Top Bottom