Watanzania wenye uwezo kuwa CEO's wa multilateral companies tunakwama wapi? Kama Helios Towers Watanzania wameweza huko, kwingine tunakwama wapi?

mkuu mayalla ,hawa HELIOS si ndio wenye umoja na MILICOM walioshilikiana na TIGO kumfuatilia RISU?
je kwenye kesi yao hawata husika kweli?
au hawa wanahusika na kusambaza minara tu mambo ya kutunza taarifa hayawahusu?
 
Moja ya kitu naona kwenye nchi yetu

Ni fikra za kijamaa ziliathiri sana watanzania wengi kuanzia kwa Viongozi wetu Hadi kwa wananchi

Viongozi kuamini serikali inaweza kuendesha Kila kitu haswa miradi ya kiuchumi na Biashara na wakati huo huo watoze Kodi ni fikra hasi ya kijamaa

Na wananchi vile vile wanaamini serikali kuchukua nafasi kubwa ya Kusimamia uchumi wao na sio wananchi kuwajibika Kusimamia uchumi wao

Mfano mzuri ni mashirika na viwanda vingi vilivyoasisiwa kipindi Cha ujamaa vingi vilikufa na vilivyobaki ni hasara

Bahati mbaya Viongozi wetu wengi hawajifunzi makosa yaliyopita bado wanataka kuaminisha wananchi kwamba serikali inaweza kuendesha miradi Kama HUDUMA

Nilisikitika niliposikia TRC ndio itaendesha SGR kutoa huduma nikajua ni suala la Muda tu

Embu fikiri Viongozi wanajivunia kukopa Tena Mabasi ya mwendokasi Leo mradi unakaribia miaka kumi

ukiwa na wateja wa kutosha Hadi inawaacha barabarani

Lakini umeshindwa kujiendesha kwa faida

Mradi wa mabasi Kuna watanzania wanaendesha vizuri tu wenyewe Tena kwenye maeneo yenye competition kubwa .
Tena wengine ni mtanzania tu mwenye Elimu yake nzuri ya la Saba , Ila Kila mwaka mradi wenyewe unakuja na kuongeza mabasi
 
Je sisi tuna proper succession plan endapo rais aliyeko madarakani akipata majanga hasa kifo?, samahani kama nawatoa kwenye reli lakini lengo ni kujenga nyumba moja kwaajili ya huko baadae
 
Tatizo ni uthubutu kuomba kazi kampuni za kimataifa ndio maana hata Pascal Mayala anayejiita mwandishi wa habari nguli uswahilini Tanzania anaishia tu kuandika vihabari uchwara vya ndani ya nchi vyombo vya habari vya ndani hajawahi ajiliwa BBC au Voice of America nk kama akina Kikeke nk ambao Mayala kawazidi qualifications kielimu tena mbali mno

Wenzie wamestaafu vyombo vya habari vya kimataifa wanalipwa monthly pensions kwa dola yeye anauza sura tu jamii forums na vigazeti vya uswahilini
 
Lakini hakai kimya, ni muhimu kujadili kuhusu jamii yetu ili kupata majawabu ya nini kifanyike kuwezesha kupiga hatua badala ya kuwaachia wanao ahirisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data kumbuka pia, "silence surrenders public responsibilities"
 
Wakristo wanashika top ten ya matajiri wote Tanzania, watumishi wengi serikalini ambao ni wasomi wazuri ni wakristo,serikali haina ufisadi sababu wakristo ni wahaminifu kwa jina la yesu, Samia hadi 2040
Nadhani unamaanisha Kinyume maana Zakaria, Patel, Gharib Salim Bilal, Said Salim Bhakresa hawa wote hawaingii kanisani. Just to mention a few.
 
Nchi walizoabzishia nalo muhimu
 
Tatizo ni uthubutu tu kuomba kazi nje au makampuni ya nje mbona wako watanzania ma CEO nje kama huyu

Massawe, Benki ya Kigali, benki kubwa ya Rwanda kwa mali, imemthibitisha Deogratius Massawe kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kitengo cha teknolojia, BK Techouse.

Deo alikuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kigali (BK) Techouse tangu Agosti mwaka 2023.

Kabla ya kuchukua wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji, aliwahi kuwa Afisa Mkuu wa Teknolojia (CTO) wa BK Techouse kwa miaka mitatu.

"Ninashukuru kushiriki kwamba nimeidhinishwa kuwa Afisa Mkuu Mtendaji (Mkurugenzi Mtendaji) wa BK Techouse.. Nimefurahishwa na fursa zilizo mbele katika sura hii mpya," Deo alisema kwenye LinkedIn.

BK Techouse iliyoanzishwa mwaka wa 2016 ni mmoja wa wahusika wakuu katika kuweka uchumi wa Rwanda kwenye dijitali.

Inatoa teknolojia ya ubunifu na huduma katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kilimo, teknolojia ya elimu na teknolojia ya fedha.

Ni mifumo ya malipo ya kidijitali ina zaidi ya watumiaji milioni 3.

Kabla ya kuhamia Rwanda, Deo (pichani) alifanya kazi nchini Marekani katika kampuni kubwa ya mawasiliano ya T-Mobile kwa zaidi ya miaka 14.

Alishikilia nyadhifa mbalimbali katika T-T-Mobile, ikiwa ni pamoja na Meneja Mwandamizi wa Bidhaa na Teknolojia na hapo awali alifanya kazi kama CTO/COO katika kampuni ya kuendesha gari ya Moovn.

Katika miaka yake ya mapema nchini Marekani, Massawe pia alifanya kazi kama mshauri mkuu wa IT wa Microsoft na mhandisi wa mfumo wa ndani katika IBM.

Ana MBA katika usimamizi wa biashara na habari za afya kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Georgia na Shahada ya Sayansi ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Washington.

 
Mbona huzungumzii katazo la uraia pacha linavyopoteza watanzania wenye nia ya dhati kurudi kusaidia nyumbani.?

Wapo watu wengi tu wana nafasi kubwa sana katika nchi za watu ila waliamua kukacha utanzania ili wachukue fursa hizo na ndio nchi ikawa imepoteza asset .

Hata wale waliokuwa 50% -50% muda ulivyoenda nao waliona wakache uraia moja kwa moja maana waliojaribu kurudi walikutana na kauli za [maelekezo kutoka juu, hii huwa tunafanya hivi miaka yote "] sasa kwa mtu aliye na exposure kubwa hawezi kufit kwa watu kama hawa tofauti na hapo ndio ile ya kuamua kuweka akili pembeni na kufuata hayo niliyoyataja.

Swali lianzie kwanini Tanzania haitaki uraia pacha ?
 
watumishi wa umma wako kwenye luxury comfort zone hapo nchi ya gizani. usitegemee maajabu.
 
Mbona huzungumzii katazo la uraia pacha linavyopoteza watanzania wenye nia ya dhati kurudi kusaidia nyumbani.?
Ajira zinazolipa vizuri ni kampuni za kimataifa hizo hazijali uraia wa mtu ni hapa kazi tu ulichoandika ni nje ya mada

Mleta mada anaongelea watanzania kuwa ma CEO wa makampuni ya kimataifa sio ya ndani kama TRA au treni ya mwendo kasi au shirika la masoko la kariakoo nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…