Watanzania wenzangu mnafanya nini Mozambique?

Rene Jr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2014
Posts
3,714
Reaction score
2,376
Habari za kazi wakuu. Kumekuwa na mtiririko mkubwa sana wa Watanzania kuelekea Msumbiji, wanasema oportunities ziko nyingi kule, binafsi nimevutiwa sana lakini sijapata kuzungumza na Watanzania walioko huko kuskia wao wanapiga mishe gani na ni fursa gani zilizopo huko kwa sasa. Nimejaribu kufanya kautafiti kidogo kupitia google nimeona mji unaochipukia sana kwa sasa ni Tete, Je kuna watu walioko Tete kwa sasa ningependa kujifunza kutoka kwao. Mimi ni mwanamume mpiganaji, hivyo ningependda kujichanganya maeneo yaliyo active. Kama uko mji mwingine au unajua miji mingine na fursa zilizopo tusaidiane wakuu. i.e; sina mtaji mkubwa wa kujenga mjumba maana nimesoma sehem makazi yanahitajika sana, mtaji wangu ni mtaji kidogo, akili na nguvu nyingi. Nitashukuru kwa mawazo yenu wakuu.
 
Nenda Pemba kuna gesi so pako poa unaweza ukawekeza hapo na watanzania wapo ila kwa kuanzia nenda ukatembee uone mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nenda Pemba kuna gesi so pako poa unaweza ukawekeza hapo na watanzania wapo ila kwa kuanzia nenda ukatembee uone mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

asante kaka, wazo langu hasa ni hilo, nikishajua miji miwili mitatu itayonivutia nitainuka kwenda kuangalia mazingira. Pemba kuna mishe gani hasa zinazoweza kulipa?
 
vipi kuhusu permit za huko?Na je askari hawakusumbui kama wakikujua ni mgeni?
 
vipi kuhusu permit za huko?Na je askari hawakusumbui kama wakikujua ni mgeni?

Hata kama una permit askari ni wasumbufu. Unajua baada ya vita yao ya ndani askari wa FRELIMO na wale wa RENAMO walichanganywa, sasa hawa wenye asili ya RENAMO wakikusikia wewe ni mtz, basi utahujumiwa na utanyanganywa kila kitu mifano ya ndugu zangu waliofanyiwa hayo ipo mingi sana. Lakini usikate tama hizo ndiyo changamoto zenyewe
 
Biashara yoyote Pemba inafanyika kama duka baa hata hotel za kulala mgahawa na nk ni mji mzuri kwani wageni ni wengi jili ya gas,Husu permit haisumbui sana kwani ukifika una three month unapata ila wapewa mwezi mwezi ukiisha waongeza kama miezi 3 ikiisha ujapata kibali yakubidi utoke nje ya nchi na kurudi unapewa tena three month so haisumbui nafikiri mengine yapo poa .Pia waweza fanya biashara ya kuleta sigara za Tanzania na vitu vingi katika miji ya Pemba na kwa sababu hela yao iko juu utapata faida ukibadili tena ziwe shilling

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
watanzania wengi ni wauza unga bwashee, sikukatishi tamaa ila hakuna jipya huko kama fursa huzioni hapa basi huko wala usisumbuke ni story za vijiweni tu hizo.

Unga gani, unga wa mahindi au dawa za kulevya?
 
Hivi Pemba wanatumia pesa gani mkuu? Euro au rupee?
 
Wanatumia mitikashi (nimeshinda kuandikwa wanavo pronounce kwa kireno)...
 
Fursa nazojua ni kama za biashara. ..unachukua mali bongo unapeleka products za kibongo zapendwa....pili restaurants pia nazo zinalipa...kwa Kifupi watu wa Mozambique kiasi flan hawajaweza kuzitumia fursa zao zote...so ukiwa mjanja unatoka...
 
Sante mkuu nimekusoma. Wewe uko Mozambique? Niliwaza kupeleka viatu hivi vya kimasai wanavopenda wadada siku hizi, nikibeba kama pair mia tano kwenye bags je naweza kutembeza mtaani bila usumbufu? kuna watu wanaviuza huko? Gharama za guest house au nyumba za kupanga za chini kabisa zikoje?
 
Mkuu vipi kuhusu garama za malazi na chakula? guest za bei rahisi bei gani? chumba cha kupanga?
 
Chakula na gesti si gharama sana ni za kawaida na unaweza pewa contact ukaenda watu wengi wapo ila sandals za kimasai si good idea wangu ila zinalipa pia

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Viatu vya kimasai mkuu Sidhani kama ni njema...ila ningekushuri labda hardwares kama vifaa vya baiskeli na pikipiki na vitu kama hivo
 
Viatu vya kimasai mkuu Sidhani kama ni njema...ila ningekushuri labda hardwares kama vifaa vya baiskeli na pikipiki na vitu kama hivo

shukrani sana kaka, sasa harware si mpaka kupata frame mkuu? nilitaka vitu vya kuweza kubeba wakati nafanya research ili kujaribu kurejesha gharama za nauli na malazi. Frame za biashara huko zinatembea bei gani?
cc: kadafi
 
Last edited by a moderator:

Mkuu waweza pia kupeleka bidhaa kama vitunguu saumu. Unachukua Tanzania unapeleka moçambique inalipa sana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu vipi nauli kutoka Dar mpaka huko na gharama za pass na guesthouse kwaujumla kama mtafiti masoko

alafu kama walitawaliwa na wareno ivi je vipi English wanaelewa au ni Lugha gani inayotumika na watu wengi?

Ahsante sana.
 
Hawaelewi English (wachache mno kama wapo)..lugha ni kireno, kimakonde na kiswahili wanaelewa elewa kwa mikoa ya kaskazi kama cape delgado....na kuhusu usafiri kutoka Dar fika mtwara kwanza then pale kuna usafiri kwenda border (ziko njia nyingi)..ila sio bei kubwa saana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…