Watashuka daraja

Hii ndio barua?
Mkuu unachokitaka wewe kwa Mtibwa ni hatua walizofanya kimaandishi kwenda kwa TFF au bodi ya ligi, lakini kwa Simba haukuleta hatua walizozifanya kimaandishi bali umeleta maamuzi ya TFF.

1) hakuna ushahidi wowote wa kimaandishi ulioletwa humu kuonesha kuwa simba waliandikia bodi ya ligi au TFF barua ya kuomba kuarishwa mechi. Bali tunaona ni barua ya maamuzi ya TFF kwa mechi baina ya Kagera vs Simba.

2) viongozi wa Mtibwa wamenukuliwa wakisema kuwa waliwasiliana na bodi ya ligi na kisha wakapewa maelekezo ya kuonana na watalamu wa afya na kwa mujibu wa hao hao viongozi wa Mtibwa, wanadai walifanya hivyo lakini wakaambiwa mechi ichezwe kwavile wana under 20. Kama kauli hii ya kiongozi wa Mtibwa ni ya uongo, alipaswa kuwajibishwa kwa kupotosha au kuchonganisha mashabiki na viongozi wa mpira. Lakini kukaa kimya nako inaonesha walitamka hivyo iwe kimaandishi au kwa njia ya simu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…