Watato wakiniona huwa wanacheka sana na kunizoea hata niwe mkali

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Wasalaam.
Kumekuwa na kawaida sana kwamba watoto wadogo wakiniona wananiangalia sanaaaaa.
Halafu baadae wanaanza kucheka kweli kweli. Hadi wazazi wao wanaanza kushangaa maana huwa hawachekagi hivyo sana. Siku nyingine nimekaa sehemu naingia tu nkatoto fulani kakike kamekuja kukaa karibu yangu kananiangalia sana usoni, baadae nikakapa simu yangu kakaanza kucheza Game ya Temple Run. Mama yake akaja pale kuniomba radhi na kuanza kukaraipia kwanini kanaazima simu za watu kasiowajua. Wale majirani zangu wakasema walihisi labda ni katoto kangu hivi. Nilimwambia mama yake mimi sina shida acheze tu, tukakaa nako pale kakacheza mpaka simu ikakata chaji. Kakaanza kunipigisha stori yani tumeongea nako hadi kakalala nikakabeba. Ile naondoka wacha kaanze kunililia ova kananijua yani.

Mara nyingi watoto huwa wanaanzanga kuniongelesha na kunizoea hadi nashangaa sana.
Sasa juzi nidyo nimeishiwa na nguvu, nimekaa kwenye mstari wa hospitali nikaona kajamaa fulani kana kama mwaka moja hivi. Yaani kadogo balaa (Andunje) kakamuacha maza wake kakanifuata pale nilipokuwa nimekaa, kakaniangalia kwa muda mrefu kweli halafu baadae kakaanza kucheka kama mtu mzima. Kalicheka hadi kanakaa chini, watu pale hawana mbavu wanaanza kuniangalia mimi hadi nkajistukia yani. Hii sii mara ya kwanza yaani sijui kuna nini kati yangu mimi na hivi vijamaa.

Nikiweka sura ya ukali ili kuvifukuza nidyo kabisaa vinazidi kucheka,
Yaani hata niwe mkali vipi vyenyewe hivyo mwilini. Mara kinivute sharubu, mara kinivue miwani.
Hiki kiko na andazi lake kinataka kunilisha na mimi yaani vurugu ova vinanijua atiii.
Yaani sijuia vinaniona mimi nimekaa kama likatuni fulani.
 
Kuna mshkaji wangu flani yupo disign kama yako, vitoto vidogo ikifika mida ya saa kumi na moja jioni unavikuta vimejikusanya nje ya geti lake ukiviuliza mnafanya nini hapo vinakujibu tunamtafuta uncle, jamaa anavichukua anavipakisha kwenye noah anaanza kuvizungusha mjini, siku nyingine avipa magame ya mpira...

kupendwa na watoto wanasema ni baraka
 

Hahahaa,
Mkuu imefika kipindi nilienda home mwaka mpya yaani nikakuta lundo la wajukuu pale.
Yaani nikitaka kutoka naacha kilio huku nyuma ikabidi niwe natembea nao.
Nimeondoka najua karibia katuni na chaneli zake yani balaa tupuuu!
 
je unawatoto?
kama huna huo ni ujumbe unatakiwa utafute mtoto.

wanasemaga kama huna watoto utapendwa sana na watoto.

Hahaha mkuu ninao!
Hawa wangu ndiyo balaa kabisa.
Nimewabadilisha Pampers, nimewalisha na nilikuwa na kazi ya kuwalaza.
Siku hizi wamekua ndiyo hawanililii sana lakini wanapiga simu kila siku asubuhi kunisalimu kabla ya shule.
 
Kuna watu tupo hivyo afadhal nipata mwenzangu nilikua nawaza cpati picha saa mi hata kitoto kikiwa kinalia wameshindwa kukinyamazisha mi nkikibeba kinakaa kimya gaflaa full kunitumbulia macho na kukiacha baada ya hapo ni mbinde cjui tatzo ni nn mweeee
 
Hahaha mkuu ninao!
Hawa wangu ndiyo balaa kabisa.
Nimewabadilisha Pampers, nimewalisha na nilikuwa na kazi ya kuwalaza.
Siku hizi wamekua ndiyo hawanililii sana lakini wanapiga simu kila siku asubuhi kunisalimu kabla ya shule.
hahahahahahahaha.....
sawa mkuu.

ila kama ndio wa kwenye.avatar hapo lazima wacheke tu.
hawana namna.
 

Hahaha,
Hiyo imenikuta sana kiongozi.
 
Kuna watu wanakuaga na mvuto kwa watoto, na wengine hawana watoto wakiwaona tu wanaanza kulia na kuogopa
 
Hata mimi nimecheka sana baada ya kusoma kichwa cha habari ulichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…