Wasalaam.
Kumekuwa na kawaida sana kwamba watoto wadogo wakiniona wananiangalia sanaaaaa.
Halafu baadae wanaanza kucheka kweli kweli. Hadi wazazi wao wanaanza kushangaa maana huwa hawachekagi hivyo sana. Siku nyingine nimekaa sehemu naingia tu nkatoto fulani kakike kamekuja kukaa karibu yangu kananiangalia sana usoni, baadae nikakapa simu yangu kakaanza kucheza Game ya Temple Run. Mama yake akaja pale kuniomba radhi na kuanza kukaraipia kwanini kanaazima simu za watu kasiowajua. Wale majirani zangu wakasema walihisi labda ni katoto kangu hivi. Nilimwambia mama yake mimi sina shida acheze tu, tukakaa nako pale kakacheza mpaka simu ikakata chaji. Kakaanza kunipigisha stori yani tumeongea nako hadi kakalala nikakabeba. Ile naondoka wacha kaanze kunililia ova kananijua yani.
Mara nyingi watoto huwa wanaanzanga kuniongelesha na kunizoea hadi nashangaa sana.
Sasa juzi nidyo nimeishiwa na nguvu, nimekaa kwenye mstari wa hospitali nikaona kajamaa fulani kana kama mwaka moja hivi. Yaani kadogo balaa (Andunje) kakamuacha maza wake kakanifuata pale nilipokuwa nimekaa, kakaniangalia kwa muda mrefu kweli halafu baadae kakaanza kucheka kama mtu mzima. Kalicheka hadi kanakaa chini, watu pale hawana mbavu wanaanza kuniangalia mimi hadi nkajistukia yani. Hii sii mara ya kwanza yaani sijui kuna nini kati yangu mimi na hivi vijamaa.
Nikiweka sura ya ukali ili kuvifukuza nidyo kabisaa vinazidi kucheka,
Yaani hata niwe mkali vipi vyenyewe hivyo mwilini. Mara kinivute sharubu, mara kinivue miwani.
Hiki kiko na andazi lake kinataka kunilisha na mimi yaani vurugu ova vinanijua atiii.
Yaani sijuia vinaniona mimi nimekaa kama likatuni fulani.