Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

mkuu nadhani huelewi hawajakamatwa na gongo hao wamekamatwa na kemikali bandia za kutengeneza pombe ambazo si sahihii kutumika na binadamu!!

Unajua ni watu wangap watawaua kuwaharibia figo??? unajua kwann matatizo ya figo yanazidi ndo hawa wanaotengeneza kemikali na kusidanyanya kama pombe ni hatar

china wangenyongwa
 
Jera maisha! Hv Daniel yona, na Pesambili mramba walifungwa miaka mingapi jera?
Nakumbuka Mramba kwa kesi ya ufisadi wa mambilioni ya TSh, alipewa kifungo cha nje, akawa anapelekwa hoapitsri ya mnazi, mmoja kufagia! Eti ndio adhabu,
Wakati huo V8 lake limepaki pembeni lipo silence!
Wadogo zangu Bora uibe pesa nyingi aiseee
 
Kwa Ulaya hawa wangesaidiwa wakaanzisha kiwanda halali, bongo wanafungwa maisha!
Nikweli Kuna NGO moja ya mzungu inalea watoto yatima na wenye Maisha magumu..

Siku moja Yule mfadhili mzungu alitembelea kituo alipo kua ameacha mkoba mle ofisin ikagundulika mtoto mmoja akaiba pesa kwenye ule mkoba

Baada ya kufanya msako mtoto mmoja akagundulika ndie Alie chukua zile pesa Basi wale walezi waafrika wakaanza kumshambulia kwa bakora na maneno..

Yule mzungu akawakemea wale walezi akamwita mtoto kwa upendo na kumfanya Yule mtoto rafiki na alipo ondoka akamwachia pesa na Mara kwa Mara akawa anamfuatilia maendeleo yake tangia siku hiyo..

Wenzetu hupenda kutumia Positive punishment Ila kina sisi waafrika Ni mwendo wa negative punishment
 
Ndo hukumu ya maisha jela. Naona zimetumika hisia zaidi
 
Sasa hakimu anatakiwa nae ajiongeze, hivi unajisikiaje kutoa hukumu ambayo inakuja kutenguliwa. Unaonekana huna akili wala welidi juu ya taaluma yako. Kuna taalum hutakiwa kuwa unakosea kabisa.
kwa sisi tunao jua njaa na msoto unafananaje tunaweza sema jamaa waliamua kutumia loophole so vijana wanao jitafuta Tanzania ndio nchi pekee ambayo kutoboa Ni very EASY
Yaan hakuna uangalizi sure unaona mfano haha maji ya kunywa unaweza yapiga copy na ukayaingiza sokoni easy
The same case kwa bidhaa nyingine nyingi hususani izo pombekali cooker, smart gin, shigwah,robot, sungura E.t.c

Nipo nasikiliza Wimbo wa BUSHOKE_ DUNIA NJIA
 
Ethanol inaua brother.

Hawa njaa zao zilikuwa zinaua watu wengine.

Ingechunguzwa zaidi walioathirika na madhara ya hizo pombe feki.

Inaweza kuwa mbaya zaidi.

Ulaya wangehukumiwa zaidi.
Hivi kumbe ethanol ni miongoni mwa madawa ya kulevya? Mbona Ethanol, jina lake la kawaida ni Alcohol au kilevi na POMBE ZOTE ziwe za kienyeji au za viwandani kilichomo humo na ambacho ndicho kinachowalewesha wanywaji ni alcohol aina ya Ethanol? Ethanol pia inatumika katika kutengeneza vipodozi, dawa za kutibu magonjwa ya ngozi n.k.n.k. Kwa hiyo kosa lao hao jamaa ni kumiliki Ethanol na sio kutumia ethanol? Kama ni kumiliki ethanol basi wangeshtakiwa wote wenye magroceries, vilabu n.k. kwani huko ndo ethanol ilipo na kwa viwango (%) tofauti-tofauti. Kama kosa ni kutumia ethanol, basi walevi/wanywaji pombe wote wangeshtakiwa au kwani sheria inasema ethanol ya concentration kiasi gani ndo mtu binafsi haruhusiwi kumiliki au inakuwaje? Sielewi.
Dah! Hao jamaa wamtafute wakili ili wakate rufaa labda njia ya kutokea inaweza kupatikana. Pole zao lakini.
 
Kwa bongo hata aliyempiga shoka mtu hadharani mbele za watu na kumuua hanyongwi (wanaosaini kunyonga wanadaiwa eti kuogopa dhambi), ndio wanyongwe hawa ambao hata hatuna uhakika kama wameua mtu?
Mzee

Kuna THE UNIVERSAL DECLARATION OF HUMAN RIGHTS viongozi wengi wanabanwa

So inabidi uwe na roho ngumu Kama kiongozi kuwafunga kwenye viroba na kuwatosa kwenye mito, ziwa na baharini
 
ulaya ipi unaizungumzia ndugu

kagushi bidha za ulaya ndani ya ulaya uone litakalokukuta
Kwani hawa jamaa wametiwa hatiani kwa kosa la kughushi bidhaa au kwa kosa la kukutwa(Kumiliki) Ethanol? Kama ni kughushi bidhaa, basi Mlalamikaji au mwenye kiwanda Halali ndiye anayefungua mashtaka dhidi ya mtuhumiwa i.e. Mwenye Hatimiliki (Nembo ya Kiwanda) Ndiye anayeshtaki Mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…