Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Julius kaka yangu.
Makosa yaliyofanyika Tanzania yanaelekewa ya historia kidogo lakini nadhani yana mwisho wake, ingawa mwisho huo unaweza kufikiwa wakati hatuna nchi. Kosa la kwanza lililofanyika Tanzania ni pale tulipojenga mfumo ambao tulimwamani sana kiongozi kuwa ni mzalendo na anafanya kila jambo kwa msalahi ya nchi. Nyerere, Sokoine na viongozi wengi wa kizazi cha kwanza walikuwa wazalendo, kwa hiyo tukawa tunawaamini, hatukujenga mfumo wa kuwahoji na kuwaadhibu viongozi hao. Baada ya viongozi wazalendo kuisha, tukapata viongozi wajasiliamali ambao hawakujali maslahi ya nchi zaidi ya faida zao binafsi chini ya mfumo ule ule tuliokuwa nao wakati tukiwa na viongozi wazalendo. Wakatumia nafasi zao kutafuna nchi huku wengine wakitumia mali za serikali kufanya hivyo. Sijui niwalaumu viongozi wazalendo kwa kutotuachia misingi ya kuwaadhibu viongozi au niwalaumu wananchi wenzangu kwa kuwa wavumilivu kupita kiasi huku tukilalamikia chini chini.
Nasikia sasa hivi Tanzania ni ya tatu kwa uchimbaji wa dhahabu duniani, lakini Tanzania haiopnekani kama nchi ya dhahabu; vile vile nimesikia kuwa katika miaka 12 Tanzanite yote itakuwa imekwisha, na bado Tanzania haitaonekana kama nchi ya Tanzanite. Tutabaki na mashimo matupu ambayo yatazagaa nchi nzima hadi kwenye barabara zetu za Dar es Salaam.
Inabidi wananchi tuamke kusema sasa basi; tudai katiba mpya inayoruhusu viongozi (hata rais) kuadhibiwa papo kwa papo inapogundulika kuwa wamepotumia madaraka yao vibaya na kusababisha hasara kubwa kwa nchi. Tuondoe huo usiri wa serikali, kwa sababu serikali ni ya wanachi siyo kuwa ni kampuni binafsi ya walio madarakani. Sijui kama wakati wa kuamka ni huu au bado lakini nadhani haitachukua muda wananchi wataamka.