Watch "Tanzania's BRT system has been running for 3 years" on YouTube

Waongeze mabasi Basi Kama wanatengeneza hela.
 
Wanakimbilia kujenga railway wakat mwendokasi imewashinda

mkuu wa mkoa anakimbilia kutaka kubadri kigamboni iwe texas marekan wakat kero ambazo zipo wazi hataki kuzitatua
Nilitegemea hii kero angeitatua..
Leadership is all about solving current problems.

Tutakujua kuwa wewe ni mwanaume wa shoka unapotatua changamoto ambazo wengine walizishindwa sio kukimbilia kwenye mambo mengine..

Come on guys...
 
Changamoto ndogo ndogo zipo ila sio kila siku na sio kila route,
Maana naona mapovu ya wivu 😂😂😂
 
Brt ni project iliyofanikiwa 100% tatizo la kuzidi kwa watu ni changamoto tu za kiuendeshaji ila sio kwamba serikali ilikosea ila ukileta siasa kwenye hili ndio nitakuona mjinga ,wasiotumia huu usafiri ndio utaona maneno yao humu ya hovyo changamoto zipo kwa mataifa yote na sio kwamba mamlaka husika imekaa tu Bali inatafuta ufumbuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we fala unatoka wapi? Nina uhakika chuo hujafika Wakenya hawahawa corrupt dudes ndo unawasifia! Wafuta njaa kwao kwanza! Ama hamia Kenya! 2020 unaleta ngonjera za Wakenya in hospitality industry!

Geza wewe ni mkongwe humu bana. Uwe na lugha ya staha kidogo. Ukweli mwendokasi ni aibu kwa jinsi inavyoendeswa labda kama hujawai kutumia huo usafiri hivyo huwezi kujua kero yake. Ata ukitukana ukweli ndo huo na jua ata sisi tuna uhuru wa kutoa mawazo ili huduma ziwe bora.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mimi nimeleta habari za Watanzania wenyewe, halafu ni nyingi sana yaani nikiamua kuendelea kuzileta nitajaza server za watu bure na ukizingatia mradi unazidi kuzorota.
 
Wewe jamaa hizi picha huwa unazitoa wapi ?.🤠 , Hilo jambo sio zuri lakin limenifurahisha.

Mbona zipo maelfu ya picha kama hizi, wala huhitaji kuhangaika kutafuta, ila hii ya mwanaume kuvizia mtoto imeniuma sana, sio jambo nzuri kwa kweli, inapaswa watoto wa kibinti watengewe sehemu...

 
Huo ndio utamu wa mwendokasi

Sent using Jamii Forums mobile app

Bro pamoja na ligi zetu za kawaida nakuheshimu sana humu JF maana kiaina huwa uko level headed and mature, kama wewe ni baba wa binti mdogo haupaswi kushabikia kitu kama hiki, picha inaonyesha kabisa huyo ni mtoto, hajabalehe, libaba lote hilo bila aibu limejisukumiza kwa mtoto, hovyoo sana.
 
Mimi nimeleta habari za Watanzania wenyewe, halafu ni nyingi sana yaani nikiamua kuendelea kuzileta nitajaza server za watu bure na ukizingatia mradi unazidi kuzorota.
To be honest, the idea was brilliant na ukizingatia mji ulivyojengwa ni rahisi sana kwa project ya aina hii, the problem ni kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya kuendesha huu mradi ilikuwa 'pasua kichwa', labda kutakuwa na mabadiliko kwa kuwa sasa wanataka kutoa kandarasi kwa wengine. Maisha yangu yote hapa Dar nilipanda mwendo kasi siku moja tu na sitamani tena, nilibanwa mbavu kidogo waniue...
 

Uhalsia wa Dar ninavyoijua, huu mradi haupaswi pale, labda kwa mji kama Dodoma ambao ndio mnaanza kuujenga na kuchora chora ramani. Dar ni pasua kichwa, completely hectic. Pale mnapaswa kuwa na mfumo wa treni zinazokatiza mjini, na ndio kitu hata huku tunajiandaa nacho, tunazo tayari ila hazitoshi itabidi zijengwe zaidi, na pia sisi tunatumia mabasi makubwa ya abiria ila yanayomilikiwa na makampuni binafsi, sio hayo yanayoendeshwa na operator mmoja.
Haya mabasi yamezagaa mjini yanakatiza kote, likija linameza idadi kubwa ya abiria, hamna cha kama hayo ya BRT eti lifuate utaratibu fulani kwamba linaweza kuja na lisibebe mtu kisa limepangiwa ratiba fulani.

Mimi nilijaribu hiyo BRT ila nikakinai kama wewe, kuna kipindi pia nilikata tiketi nikasubiri mpaka ikabidi nitoke stendi kwenda kusaka taksi.

Angalia hii picha ya mabasi ya mjini Nairobi, kila moja hapo linabeba muda wowote

 
Naenda kupanda mwendokasi hapo kimara naenda posta, will share the pics

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo Kimara utayapata maana ndio maeneo ya mwanzo mwanzo ila jongea humo maeneo ya kati uone balaa yake, usikose kupiga picha za stend mnazopita watu wamezubaa hawajui cha kufanya, na pia ingekua poa uzitumie mida ya asubuhi au jioni wakati mnasongamana mkirudi au kutoka uswazi.
 
Aaah, ushaanza maneno mzee, tulia..
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Akhaaaa aseee! Hao watu noma. Ila siku hizi wameacha huo ujinga baada ya kuona Matatizo tu now wanabanana ila sio kivile.


Naomba mgonjwa wa corona asije ingia kwenye bus hizo hasa jioni ruti za Gerezani to Kimara mbona tunazika.


MK254 Kuna wakati management inatuharibia yaani basi 20 ziko parking tu 2 zinabeba?

Huuu ujinga.


Hata hivyo mradi ukitulia na kuendeshwa kwa ufanisi na kujitoa mbona hata wazungu wanakuja kuiga.


Maana una pesa ule. Mzee fikiria hao watu wote wamelipa Tsh 650, hapo tu wakipelekwa mara moja na wengine waje tutatengeneza ngapi kwa siku.


Uzembe tu
 

Mradi ununuliwe na kampuni binafsi halafu nauli iongezwe 1,000 ili kuongeza ufanisi, hapo ndio mtateleza kwa raha zenu, lakini hili la kutegemea ruzuku ya serikli, mtakwama sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…