Wateja wa BANCABC wawekewa riba za mikopo ya 2%

Wateja wa BANCABC wawekewa riba za mikopo ya 2%

mbongowakweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
848
Reaction score
684
BANCABC wametangaza riba za mikopo za asilimia 2%, kama nilivyosikia, kwa mikopo ya aina zote, kama ni kweli basi tuwasubiri @crdbbank na NMB Tanzania nawo wawathamini wateja wao...
Kazi kwenu...
@bancabctanzania Yatangaza Punguzo la Riba za Mikopo via YouTube, tuone @NMBTanzania na @CRDBBankPlc kama nawo wanajali wateka wao..
 
Hata wakitoa bila riba, ni wangapi wanakopesheka?
 
Hawa jamaa kwenye ile kadi yao wako poa sana..
 
Nafikiri hauna taarifa sahihi za riba za mikopo kwa benk mbali mbali. Nmb wanariba ya 1.83333 kwa mwez sawa na 22% kwa mwaka kwa mikopo ya biashara,watumishi 18% na wajeshi 16%.
 
Hujaelewa vizuri.
Yamepunguza 2% kwenye Riba zao za zamani. Mfano kama ilikuwa 20% itakuwa 18%.
 
Hujaelewa vizuri.
Yamepunguza 2% kwenye Riba zao za zamani. Mfano kama ilikuwa 20% itakuwa 18%.
Braza hizo benk zna riba kubwa sana znafika hadi 30 kwa mwaka. Pia kwenye ishu ya mkopo kuna mifumo ya kuchaji riba kuna straight balance na reducing balance. Hapa sasa ndio wengi tunapopigwa kwenye mikopo hadi watu wanafunga biashara. Kwenye mifumo ya kuchaji riba hata kama kiwango cha riba ni 22% ila kwa mfumo wa kwanza utarejesha riba kubwa kwani utachajiwa 22% kila mwez kwa kiwango kile kile tofauti na redecing balance ambayo unachajiwa 22% ya deni lililobaki
 
Hiyo mikopo tutafanyia nini sasa,maana biashara tra wameamua tuikimbie kilimo ndo ugonjwa labda tunywee kimpumu na kuhonga warembo wa bongo muvi
 
Ukiondoa crdb na nmb benk nyingne ni kama hela za moto na wanachokukamatia ni kwamba wanakupa hela fasta kwa mashart kama nafuu ila shughul marejesho
 
Braza hizo benk zna riba kubwa sana znafika hadi 30 kwa mwaka. Pia kwenye ishu ya mkopo kuna mifumo ya kuchaji riba kuna straight balance na reducing balance. Hapa sasa ndio wengi tunapopigwa kwenye mikopo hadi watu wanafunga biashara. Kwenye mifumo ya kuchaji riba hata kama kiwango cha riba ni 22% ila kwa mfumo wa kwanza utarejesha riba kubwa kwani utachajiwa 22% kila mwez kwa kiwango kile kile tofauti na redecing balance ambayo unachajiwa 22% ya deni lililobaki
Hata kwenye mikataba yao hakuna kipengere kuwa utakatwa reducing au la japo wao wanapokushawishi wanakudanganya utawekwa kwenye reducing ukiingia tu nao mkataba wanakugeuka
 
Hiyo mikopo tutafanyia nini sasa,maana biashara tra wameamua tuikimbie kilimo ndo ugonjwa labda tunywee kimpumu na kuhonga warembo wa bongo muvi
hapana. una avatar ya ccm unakiaibisha chama chako kwa comment isiyokua na akili
kama mentally uko fit basi mikopo ina mengi ya kufanya ukiweka malengo
 
leo nimesikia kwenye magazeti watoa taarifa kuwa crdb wamepunguza riba kwa asilimia 4 na saiv unaweza ukarudisha mkopo kwa miaka 7 ..
na tunawaomba kina nbc ma nk. wawaige crdb la sivyo wateja watakimbilia crdb.
 
Back
Top Bottom