DOKEZO Wateja wapya wa huduma ya maji Manispaa ya Morogoro hawajapata huduma kwa kuwa MORUWASA hawana mita za ziada

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro wanaohitaji kuunganishwa na huduma ya maji safi na salama wamelalamikia kukosa huduma hiyo kwa takribani miezi sita kwa madai kuwa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira MORUWASA inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mita.

Mamlaka ziangalie kuhusu hili suala

==========
Updates...

Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, Mhandisi Tamimu Katakweba amefafanua kwa kusema:

“Ni kweli hakuna Mita kwenye soko lakini kuna Wazabuni wamejitokeza tumefanyanao mawasiliano, wametuahidi kutuletea Mita 2,000 za kuanzia ndani ya mwezi moja kutoka sasa.

“Pia sisi kama Mamlaka tumeagiza kontena la Mita kutoka Uturuki.

"Changamoto ni kuwa zile fedha za UVIKO-19 kwenye miradi ya maji Nchi nzima zilikausha Mita kwenye soko hasa class inayopaswa kutumikia ambayo ni class C, lakini kwenye soko kuna class A na B ambazo hazifai. Kuhusu kontena tunatarajiwa kupata mzigo kuanzia mwezi Juni 2023.

"Mahitaji ya Mita ni zaidi ya 10,000 ambapo itajumuisha na miradi mipya ya Bigwa, Kauzeni na kwingineko.

"Hapo bado kuna mita za kubadilisha kutokana na ubovu, hivyo jumla tunaweza kujikuta tukihitaji Mita 30,000.

"Mita ni kipimo kama ilivyo mzani, kanuni za uwepo wake zinasimamiwa na EWURA, hatuwezi kufunga maji bila Mita kwa kuwa mteja anaweza kuja kesho kusema umembambikia bili, hivyo ni lazima kuwe na Mita."
 
Naamini ujumbe umewafikia wahusika na Serikali kwa jumla ili waufanyie kazi. Maji ni uhai
 
Back
Top Bottom