Watembea kwa miguu acheni kujivuta kwenye zebra madereva sio malaika, mengi yanaweza kwenda vibaya

Zebra sio yako dereva,sema wenye madaha wapo
Mji mmoja tz, Niko kwenye haice mbele pale, tumesisima zebra maana ilikuwa asubuhi wanavuka na wanafunzi wengi kidogo, sasa gafla ilikatiza pisi moja Ilo tako charioke hafui kavalia suruli ya kuteleza alafu anatembea kna twiga han hraka, mark X moja mbele yetu ikapiga flashlight mwaaa mwaaa dereva wetu na si akajibu mwaaa mwaa😂😂 kumbe kulikuwa na traffic anachora tu akasimama kwenye zebra anamwabia dereva wa mark x pack pale akaja na kwetu akamwambia dereva nataka mniambie izo flashlight ni za nn 😂😂😂
 
Hahaha 🤣

Hafu mbele trafiki anasubiria ujifanye umevuka.
 
Tii sheria bila shuruti.. mzee anawezaje kukimbia kwenye Zebra??
Hiyo bodaboda isikufanye uvunjee sheria utakwenda segerea ohooohooo
 
Mleta mada una hoja... usikilizwe....

Mimi kama mtembea kwa miguu na mtumiaji mzuri wa Zebra hiyo nimeiona sana..

Kuna msemo unasema kila "Haki ina wajibu."

Kama mtembea kwa miguu haki na wajibu kwenye Zebra ni kujihakikishia Usalama wako ndipo uvuke..Mtu

Hivyo hivyo kwa Madereva pia..Taa ya Kijani Inamaana ya Nenda...Ila wajibu wako ni nenda kama kuna Usalama..

Ahsante..
 
Wakuu,

Ukiwa unatumia barabara unatakiwa uchukue tahadhari hata ukiwa kwenye sehemu ya kuvukia (zebra crossing).

Kuna watu wameshajiwekea nikipita kwenye zebra lazima chombo kisimame, kwahiyo yeye hajali chochote akifika kwenye zebra ni kuvuka tu. Anasahau kwamba mambo mengi yanaweza kwenda vibaya, mtu anaweza akawa na dharura anawahi mahala fulani kuna tatizo, chombo kinaweza kufeli breki, mtu anaweza akatoka resi huko stress zimempiga hajaona mtu akaondoka na wewe, bodaboda na bajaji inaweza kuchomoka huko ikakuvaa na kadhalika.

Sasa kuna wenzangu na mimi, akiwa kwenye zebra anaona huu ndio muda wake wa kutamba, muda wa kukomoa wenye magari, kuonesha machejo, kutembea kama mlimbwende, yaani kama vile malaika amesimamisha/atasimamisha vyombo vyote ili yeye apite, my friend endelea na huu mchezo ipo siku yatakukuta.

Kuwa makini wakati wote unapokuwa barabarani, lakini pia acha hizi tabia za kijivuta na kudhani kwamba muda wote madereva watakuwa 100% sawa.
ki ist chako ushaanza kunyanyasa watu
 
Mkuu baada yakununua gari Naona unaanza kutufokea sisi Watembea Kwa miguu😁
 
Tii sheria bila shuruti.. mzee anawezaje kukimbia kwenye Zebra??
Hiyo bodaboda isikufanye uvunjee sheria utakwenda segerea ohooohooo
Rudia kusoma vizuri uelewe, sijasema watu wavunje sheria, bali kuongeza umakini na kuacha kujivuta sababu mengi yanaweza kutokea.... unafata sheria lakini dereva mzembe anakuja resi huko utakaza fuvu kwakuwa upo kwenye zebra ama utaongeza umakini usikumbwe na kadhia? Lakini watembea kwa miguu wapo wengi ambao hawafati sheria kwakuw atu anajua yupo kwenye zebra
 
Kwa kifupi huwezi kumpangia mtu avuke namna gani akiwa kwenye zebra.

Kikubwa jifunze kuwa na moyo wa kuvumilia na kupuuza vitu unavyokutana navyo rodi.
 
Rudia kusoma vizuri uelewe, sijasema watu wavunje sheria, bali kuongeza umakini na kuacha kujivuta sababu mengi yanaweza kutokea.... unafata sheria lakini dereva mzembe anakuja resi huko utakaza fuvu kwakuwa upo kwenye zebra ama utaongeza umakini usikumbwe na kadhia? Lakini watembea kwa miguu wapo wengi ambao hawafati sheria kwakuw atu anajua yupo kwenye zebra
Anavunjaje sheria kwenye Zebra..???
 
Ukiwa unatumia barabara unatakiwa uchukue tahadhari hata ukiwa kwenye sehemu ya kuvukia (zebra crossing).
Mtembea kwa miguu taa ya zebra ikiruhusu unajimwambafai kwenye zebra unaweza hata ukalala pale na usifanywe kitu na mjinga yoyote Ila bongo ndio madereva hawajui sheria za zebra watu wanavuka wanakimbia gari linakuja speed ya ajabu kwenye zebra
 
Hilo ni kweli, madereva bongo wengi ni pasua kichwa, japokuwa kuna watembea kwa miguu wengine hukatisha hata taa ikiwa nyekundu mradi anapita kwenye zebra hajali kitu, kwahiyo ni muhimu kuwa makini.
 
Back
Top Bottom