Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
๐ช๐๐ง๐๐ก๐๐๐๐ ๐๐๐ง๐จ๐ข ๐๐๐ ๐จ๐ข๐๐ข๐ญ๐ ๐ ๐ช๐๐ก๐ญ๐ ๐ช๐๐ง๐๐๐๐ช๐ ๐๐จ๐ง๐ข๐ ๐๐จ๐๐จ๐ ๐ ๐ญ๐ ๐๐๐๐ฅ๐จ๐ฅ๐ ๐๐ช๐ ๐ฆ๐๐ ๐ฎ๐ฐ
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda โ Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu.
Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza
Amesisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika.
โHii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi saa 24.โ
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthubitisho wa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia watanzania na kujali changamoto mbalimbali nchini.
โKituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 kwenda Mwaka 2020, kilisimama baada ya wenzetu kujitoa, lakini Rais Dkt. Samia akasema tutakijenga kituo hiki kwa fedha zetu ili wavuvi waweze kupata huduma ya usalama katika kazi zaoโ