Watendaji Serikalini kusubiri matamko ya viongozi wa juu ndio watimize majukumu yao inaonesha kuna shida kwenye mamlaka

Watendaji Serikalini kusubiri matamko ya viongozi wa juu ndio watimize majukumu yao inaonesha kuna shida kwenye mamlaka

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Wiki iliyopita nilitazama taarifa moja ambao nainukuu hapa ilivyoanza;

“Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wahakikishe wanamfikisha katika vyombo vya sheria baba mzazi wa mwanafunzi wa darasa la pili (7) Jijini Arusha kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake…”

Ukisoma taarifa hiyo kwa umakini utagundua kuwa siyo ya kwanza kwa viongozi wa Serikalini kuitoa katika mikutano ya hadhara au matukio kadhaa yanayohusisha viongozi hao.

Nakumbuka wakati ameingia madarakani mwanzoni, Rais Samia aliwahi kusema kuwa moja ya mambo ambayo hatayafurahia ni kuona wananchi wakijitokeza na mabango kwenye mikutano yake ya hadhara wakiwa wanaelezea shida ambazo zinaweza kutatuliwa na mamlaka za chini.

Alisema atashughulikia mabango hayo lakini atawageukia watendaji wake au wasaidizi wake wa eneo husika kisha kudili nao, kwa kuwa hiyo itaonesha hawatendi haki au majukumu yao inavyotakiwa.

Sasa mwendelezo wa kauli kama hizo unapoona zinaendelea inatoa ishara gani?

Inamaana mtu anafanya tukio baya lakini kukitumika ‘namna’ inamaanisha hakutakuwa na msaada hadi pale ambapo kiongozi wa juu atakuja kuingilia kutoa msaada, hiyo siyo sawa.

Inaonesha bado watu wengi hasa watendaji wa Serikalini hawawajibiki inavyotakiwa, badala yake wanaongozwa na kufanya kazi kwa miheko, hawajali haki na wanaendekeza rushwa.
 
Serikali anayeweza kumshauri boss ni madaktari tu.
Kwingine tunatumia akili ya boss.
 
Ukichapa kazi kupitiliza utaonekana unajimwambafai
 
Wakati mwingine uoga unachangia katika kufanya kazi.
Nchini kwetu mfumo wa uongozi haupo sawa kabisa, kwani bado kuna hali ya itakuaje akijua mimi ndie nimefanya hivi?.
Kuna haja ya kuweka mfumo wa uongozi ambao akitoka mtu, basi ijulikane kuwa ametoka kwenye uongozi na traits zake zisahaulike.
 
Hayana utofauti na WEO wa kata ya Ikunguigazi wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita kugeuka hakimu wa kuamua kesi za mimba kwa wanafunzi ofisini kwake, hata hiyo imalizwe tu kwa WEO wa huko Arusha

Nchi hii hakuna wanaojali wananchi masikini, ukiwa na pesa wewe au cheo unakuwa juu ya sheria za nchi ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom