Watengeneza content za kuoga au kuvunja vitu kwenye barabara zenye foleni kubwa wachukuliwe hatua, wataleta maafa!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu mpo vizuri?

Huyu jamaa aliyejirekodi akioga na kuvunja nazi katikati ya barabara aliona hii ndio njia sahihi ya kuchekesha? Hapana, huu ni ujinga na hatari.

Kwanza, anachafua barabara kwa mabaki ya nazi na maji, akiharibu miundombinu. Pili, amesababisha foleni kwa madereva waliolazimika kusimama au kupita kwa tahadhari.

Zaidi ya hayo, anavunja sheria za usalama barabarani. Kitendo chake kilisababisha mkusanyiko wa watu eneo lisilo salama. Barabara ni mali ya umma kwa usafiri, si mahali pa kufanya maigizo kiholela.

Mtu akipata ajali kwa sababu ya vitendo hivi, nani wa kulaumiwa? Tabia za kujitafutia matatizo halafu tunailaumu serikali kwa uzembe wetu.

TANROADS na mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua kama funzo kwa wengine wenye tabia kama hizi. Au nyie mnaonaje, Wakuu?

Your browser is not able to display this video.
 
We unasema content mwenzio anafanya kweli. Sawa unataka utajiri je masharti utayaweza?
Hata kama ni kweli bado haizuii kuchukuliwa hatua kabla maafa hayajatokea kwani hii ni hatari mkuu
 
Angeoga uchi wa mnyama tujue kweli anaoga.

Hapo si anapiga passport tu.(ndugu zangu mliosoma boarding maeneo yenye baridi mtanielewa)
 
Content tu hizo, hamna ukweli hapo.

Anajitafutia matatizo kwa clip ambayo si ajabu isimlipe chochote.
 
Mbona anaerekodi na anaeoga hawapo pamoja? Na wanaorekodi ni wengi tu, huyo hatengenezi content, kachotwa tu akili kwamba afanye hivyo atafanikiwa. Ni uwendawazimu, ni ugonjwa wa akili tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…