31 Aug 2020 — Uchaguzi 2020 Makonda azuiwa kukaa Jukwaa Kuu kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM
View: https://m.youtube.com/watch?v=KQcxTeoUIrs
JINSI IKULU INAVYOFANYA KAZI
Mzee Lee Njiru mwandishi wa habari wa marais wa Kenya kwa miaka 42 katika ikulu ya Nairobi Kenya alikuwa na haya ya kueleza, ambayo mwaandishi uchwara Deus Balile na mwandishi mheshimiwa sana Daniel Chongolo kuhusu ukiwa karibu na watawala hutakiwi kufanya kabisa :
View: https://m.youtube.com/watch?v=8ICU1vEaYRQ
Mzee Lee Njiru alikuwa mwandishi wa mkoani akiwa kijana na ghafla akajikuta ameteuliwa kuwa mwandishi wa Ikulu.
Sasa hawa kina Deus Balile ambao wakiwa kila mara wanaalikwa ktk mikutano na watawala wanajiona nao tayari wamekuwa na 'mamlaka', wakati hayo mamlaka hawana bali wanatumiwa.
Kilichomtokea mwandishi wa habari Daniel Chongolo inapaswa waandishi wa habari wote wajifunze ukiwa karibu na rais, lazima muda wote unachunguzwa mienendo ya maisha yako, na hili la Chongolo siyo
ajali bali ni jambo linalotegemewa kutokea ukikosa uangalifu na kudanganywa na
press club ya waandishi wenzake akina Deus Balile n.k waliodhani sasa wame ukaribia urais.
Mzee Lee Njiru anazungumzia zaidi kuwa watu wa usalama wa rais humwangaliwa mkuu wa nchi kwa saa zote 24 ya siku kumchunga, kumshauri, kumkataza kuwa karibu ya mtu fulani ikiwemo kuwachunguza wale wote walio karibu na rais bila kubagua iwe ni mume au mke wa rais, mwandishi, katibu mkuu wa aina yoyote, mwenyekiti wa baraza la waandishi wa habari, ndugu, jamaa na marafiki.
Na kuwa watu wa usalama wana mlinda rais kwa wivu mkubwa na ndiyo jukumu lao.... Hivyo hili la Daniel Chongolo, Deus Balile, Sukuma gang n.k ukimsikiliza Mzee Lee Njiru akielezea Siri za Ikulu na Maisha yake ya miaka 42 akiwa karibu na marais ..... ni somo kubwa
View: https://m.youtube.com/watch?v=g-Vz49ZizUE