Watetezi wa 'Legacy' ni kipi katika haya mabadiliko msichokipenda?

Watetezi wa 'Legacy' ni kipi katika haya mabadiliko msichokipenda?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nyie hamfurahii kurudi kwa uhuru wa habari na kutoa maoni kinzani kwa watu wote?

Hamfurahii kuona redio na TV zikiwa zimechangamka na za moto kwa mijadala mbalimbali?

Hamfurahii kuona magazeti yameanza kuvutia wasomaji tena?

Hamfurahii kuona ada tata za YouTube zinaanza kuondolewa?

Hamfurahii kuona CAG anaweza kuisoma ripoti yake na ikaibua mijadala ya kuboresha utendaji wa taasisi, idara na mashirika ya nchi?

Hamfurahii Spika akiibua mjadala wa bandari ya Bagamoyo na ukajadiliwa?

Hamfurahi kuona wafanyabiashara, wafanyakazi na watu wengine wakiongelea kwa uhuru mambo yalivyokwenda na yanavyotakiwa kwenda mbeleni?

Kama hamfurahii hayo katika eneo la uhuru wa habari na kutoa maoni huru tu na mabadiliko mengine mengi sehemu nyingine nyingi mnataka nchi ya aina gani basi?
 
Hatupendi kabisa kuona nguvu nyingi zikitumika kujaribu kufuta hedaya (legacy) BORA KABISA ya JPM. WATU WASHIKE ADABU & ADABU ZIWASHIKE!!! ~ Kwa Udhamini wa Mbunge makini wa Mtera.
 
Hata ingepita miaka 1, 000 na mingine na mingine, tutaendelea sana tu kumjadili JPM as if angali hai bado. Hatukusimuliwa kuhusu utendaji wake --- WE SAW IT WITH OUR CLEAR, NAKED EYES!
 
Wamehamuka kwanza maana walikuwa kwenye maombi juu ya Hotuba ya mama.
 
"Anayeweza kukubali mikataba ya Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni kichaa tu"
~ JPM
 
JPM is even more alive now as though he never died; talk to REAL PEOPLE, then utayaamini maneno yangu.
 
Leo nilikuwa nasikiliza magazeti asubuhi clouds fm..yaani Masoud Kipanya na wenzake wamshauri Raisi kabisa cha kufanya..kuwa asiishie kwenye matamko tu,abadilishe sheria. Pia akakosoa live kabisa serikali kuwapa tenda taasisi za serikali kwa kiasi kikubwa huku private sector ikiyumba.

Chini ya utawala wa Jiwe hakuna aliyekuwa anaweza kucheua. Kweli mabadiliko yanaanza kuonekana
 
Hatufurahii style CAG aliyoitumia kusoma ripoti yake kama vile kwa fitina huku akizishushia na maji baridi.

Hatukufurahia mijadala kama bandari ya Bagamoyo na ATCL ilivyo ibuka mara tu ya kumzika mwendazake. Kama vile kulikuwa na watu ambao walishajiandaa wanasubiria afe wamzike ili waanzishe yao.

Hawa watalipia hii mienendo yao isiyo furahisha wala kuwa na chembe ya utu kwa Majira na Wakati wa Bwana Mungu wa Mbinguni ukifika.
 
Watetezi wa "legacy" wamekwisha sahau kuhusu yale maneno ambayo mara kwa mara tulikuwa tukiyanukuu kutoka ktk maandiko matakatifu enzi za utawala wake.

MENE, MENE, TEKELI & PERESI

Mwisho wa enzi ulikwisha pita, tuendelee kuchapa kazi chini ya Rais wa sasa.
 
Anzeni kumsema vibaya mama samia sasa.

Kisha mtaona, mama anaweza kufanya nini.

Kivi mikutano ya kisiasa imeruhusiwa?
 
Eti eeh

Na yy wakati anabeza na kubagaza kila lililokuwa limefanyika awamu zilizopita?

Mkuki kwa nguruweee

akwendreee
Hatufurahii style CAG aliyoitumia kusoma ripoti yake kama vile kwa fitina huku akizishushia na maji baridi.

Hatukufurahia mijadala kama bandari ya Bagamoyo na ATCL ilivyo ibuka mara tu ya kumzika mwendazake. Kama vile kulikuwa na watu ambao walishajiandaa wanasubiria afe wamzike ili waanzishe yao.

Hawa watalipia hii mienendo yao isiyo furahisha wala kuwa na chembe ya utu kwa Majira na Wakati wa Bwana Mungu wa Mbinguni ukifika.
 
Kila rais anatakiwa awe na akili timamu(kikatiba).

Maana yake rais Samia asilazimishwe kufuata ya Kaisari Magufuli.
 
eti eeh

na yy wakati anabeza na kubagaza kila lililokuwa limefanyika awamu zilizopita.!?

Mkuki kwa nguruweee....

akwendreee

Yeye si aliwambia uso kwa uso live bila chenga. Wao wanasubiri kunanga marehemu akili za ajabu hizi eti unajaribu kufuta ndege na miundo mbinu kama stijilazi kwa kutumia prof kumi kumi! Wameshindwa hata kabla ya kùanza.
 
  • Je hawafurahii kuona rais akimsisitiza cag aache kigugumizi anapoelezea mapungufu aliyoyabaini kwenye ukaguzi wake?
  • Je hawafurahii kuona angalau sasa tunathubutu kutamka "Tujihadhari na covid-19"?
- Je hawafurahii kuona wafanyabiashara wanataka tena kurejesha biashara zao baada ya kuzisimamisha kwa muda?
- Je hawafurahii kuona kiongozi wa nchi akiwakemea tra kuacha ubabe wa kuwafilisi wafanyabiashara kwa kutakiwa kuja na njia rafiki za ukusanyaji kodi na kupanua wigo wa walipa kodi?

Wasiofurahia wana nongwa na tunadiriki kusema walikuwa marafiki na wanufaikaji wa utawala kandamizi.
 
Huku unatumia mbinu za unaye muona alikosea kwenye kushughulika na corona huku unaunda tume. Yale yale ya kipofu kumtahadharisha mwenye kuona kwamba hapo kunashimo utadumbukia.
 
Back
Top Bottom