Wateule kuacha nafasi na kukimbilia ubunge inamaanisha nini?

Wateule kuacha nafasi na kukimbilia ubunge inamaanisha nini?

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Licha ya onyo kali la mwenyekiti kwamba mtu aliye mteuwa asijaribu kutangaza nia ya kugombea ubunge sehemu yoyote ile kwani atamkata,lakini hali imekuwa tofauti kabisa kwani wateuliwa asilimia kubwa wameonekana wakiachia nafasi zao na kwenda kuchukua fomu za kuomba kupitishwa kuwa wagombea ubunge majimbo mbalimbali kinyume na agizo la mwenyekiti wao.

Kwa wajuzi wa mambo ya siasi, Je hii inamaanisha nini,ni kwamba njaaa imezidi ama watu wameamua kujilipua kwenye ubunge kutokana na marupurupu mengi au wamechoka kutumika?
 
Kuna kila dalili kuwa utitiri wa viongozi wa kisiasa wanaotimka kwenda kugombea ubunge huku wakiacha nyazifa zao nzito walizopewa na Rais huenda wamechoka kutumikishwa na kupelekeshwa na vyeo vya dezo vilivyojaa manyanyaso, mateso, fitna, ubabe na sintofahamu.

Sote tunajua Rais hakutaka waende kwenye ubunge, akapiga mkwara mzito, akawasimanga kuwa ni walafi wa madaraka, lakini hilo halikufua dafu, bado wameendelea kutimka kama hawana akili nzuri kuusaka ubunge huku wengi wao wakiwa hawana nafasi yoyote ya kupenya kwenye kura za maoni, na hata wakipenya bado huenda wakakatwa na Rais, maana tayari wameonyesha dharau na wamekosa utii.

Kwa wadadisi wanaona, wateule hao wametumia hii kama fursa ya kumkwepa Rais aliyekuwa anawapa vyeo vya dezo kama mtego ili kuwatumikisha kwa faida yake binafsi. Hawataki tena kufanya kazi ndani ya hii serikali kwa vyeo vya kupewa. Wamechoka!

Watu wamesepa zao.
Mzee abakie na mandondosha yake?
 
Umeandika jambo la msingi sana. Vyeo vya kupewa na Rais vimekuwa KAA LA MOTO, watu wanafanya kazi huku wanafikiria kufukuzwa, kusimangwa au kutukanwa! Wengi wa watia nia hawana uhakika kabisa, ni kama wamepata njia ya kukimbia masimango!
 
Licha ya onyo kali la mwenyekiti kwamba mtu aliye mteuwa asijaribu kutangaza nia ya kugombea ubunge sehemu yoyote ile kwani atamkata,lakini hali imekuwa tofauti kabisa kwani wateuliwa asilimia kubwa wameonekana wakiachia nafasi zao na kwenda kuchukua fomu za kuomba kupitishwa kuwa wagombea ubunge majimbo mbalimbali kinyume na agizo la mwenyekiti wao.

Kwa wajuzi wa mambo ya siasi, Je hii inamaanisha nini,ni kwamba njaaa imezidi ama watu wameamua kujilipua kwenye ubunge kutokana na marupurupu mengi au wamechoka kutumika?
Sababu kubwa ni kuwa mtu akiwa mbunge ana uhakika na kazi yake kuwa 99% atamaliza miaka yake mitano bila wasiwasi, hivyo ni rahisi hata kupanga mipango yake, ya kiuchumi, kuliko hizo nafasi za kuteuliwa sekunde yoyote tu unatimuliwa!! Yaani ajira yako inategemea sana na jiwe ameamkaje, au anajisikiaje?!!. Sababu nyingine ni malipo na majukumu, ubunge hakuna majukumu makubwa ya kukuumiza kichwa, hutasikia kuwa ohooo, watoto wanakaa chini, atafutwe mbunge, mshahara wenyewe ndio huooo!!!
 
Kwa maoni yangu Utumishi wa umma jwa sasa ni utumwa,wateule hawana uhakika na kazi zao,kazi ya kuteuliwa kwa sasa unaishi kwa hofu kiasi kwamba wengi wana pressure,hivyo bora mtu apambane apate ubunge ili aitwe Muheshimiwa na asiishi kwa hofu ya kutumbuliwa kama wanavyoishi sasa.

Yaani maisha ya utumishi kwa sasa ni maisha ya hofu tupu,kila bosi ana bosi wake,kila mkubwa ana mkubwa wake.
Sasa Kitendo cha baadhi ya wakubwa kutukana waliochini yao hadharani tena mbele ya vyombo vya habari,halafu ukiwa na familia unaoneshhwa jinsi ulivyokuwa unatetema kulinda kibarua chako,inaumiza

Ndio maana wateule wote hawataki kazi tena,bora wakapiganie ubunge hata wakikosa watakuwa huru kuliko maisha ya sasa

Hicho ndio chanzo cha wateule kwenda kinyume na tangazo la Chama.
 
Back
Top Bottom