Ni hivi hivi, mchana kweupe, upinzani unaanza kuchimbwa na wao wakishangilia kama inavyoonekana hapa.
Ukiachana na hivyo vitisho vya kipuuzi, angalia hawa mnaowasema kila siku akina Popole wanavyochakarika na kazi ndani ya chama wakifanya mikakati kila mahala, hata ile isiyokuwa halali na ambayo haitangazwa na kushangiliwa humu kwa sasa hivi.
Wapinzani kuja kustuka, too late, wamekwishafungwa goli! Mambo ni yale yale ya siku zote, lakini hakuna funzo linalosomeka.
Hawa, akina Popole, wapo sana huku vijijini, viongozi wa mashina wanatogota kimya kimya, wapinzani ndio kwanza wanajionyesha mijini.
Akina Popole wakiwafunda wagomea wao kila mahali, na kuwapa mbinu za kujaza fomu, wagombea wa upinzani watajaza fomu kama hawajawahi kaa darasani'
Halafu wanapokatwa kwa sababu za kipuuzi kabisa, upinzani ndio wanalilia wananchi wawaonee huruma!
Haya tunayaandika sio kwa furaha, lakini uzembe unapotokea hakuna sababu ya kuvungavunga ukweli ulivyo.
Sasa hivi wengi tunakaza roho, endapo uchaguzi utafanyika na ukaonyesha unafuu wa kutosha kwamba uvurugaji haukuwa mkubwa kiasi cha kutisha, na Magufuli akishinda katika hali hiyo tutashangilia, sasa tufanyeje kama waTanzania ndivyo walivyoamua kutokana na uzembe wa watu kufanya kazi zao kwa weledi.
Tunasubiri tu, uchaguzi ufanyike katika hali nzuri ya kuridhisha, tutameza vidonge vichungu na maisha yataendelea.
Na safari hii, baada ya kuipoteza nafasi hii, itabidi tusubiri muujiza uzuie kuwa kama Rwanda au Uganda kikamilifu kabisa.