Uchaguzi 2020 Watia nia CCM Mbeya wachimbwa mkwara

Uchaguzi 2020 Watia nia CCM Mbeya wachimbwa mkwara

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
19 Julai 2020
Watia Nia CCM Mbeya Wachimbwa Mkwara

Mjiandae kisaikolojia, atakayesaliti kutimulia chama, Katibu Uenezi wa CCM Mpya ndugu Humphrey Polepole aongoza jopo kuwafunda

Hakuna mtia nia wa CCM kukimbilia upinzani, ukishindwa kura za maoni. Ukitusaliti tutakufuata popote ulipo asema Bashiru Madodi katibu uenezi CCM Mkoa Mbeya ktk mkutano wa makada wa CCM Mpya.

Mwaka huu huwezi kuharibu ushindi wa chama cha CCM ukabaki salama, tumepokea maagizo toka juu.

Chanzo: MbeyaYetuOnlineTV
 
Ni hivi hivi, mchana kweupe, upinzani unaanza kuchimbwa na wao wakishangilia kama inavyoonekana hapa.

Ukiachana na hivyo vitisho vya kipuuzi, angalia hawa mnaowasema kila siku akina Popole wanavyochakarika na kazi ndani ya chama wakifanya mikakati kila mahala, hata ile isiyokuwa halali na ambayo haitangazwa na kushangiliwa humu kwa sasa hivi.

Wapinzani kuja kustuka, too late, wamekwishafungwa goli! Mambo ni yale yale ya siku zote, lakini hakuna funzo linalosomeka.

Hawa, akina Popole, wapo sana huku vijijini, viongozi wa mashina wanatogota kimya kimya, wapinzani ndio kwanza wanajionyesha mijini.

Akina Popole wakiwafunda wagomea wao kila mahali, na kuwapa mbinu za kujaza fomu, wagombea wa upinzani watajaza fomu kama hawajawahi kaa darasani'
Halafu wanapokatwa kwa sababu za kipuuzi kabisa, upinzani ndio wanalilia wananchi wawaonee huruma!

Haya tunayaandika sio kwa furaha, lakini uzembe unapotokea hakuna sababu ya kuvungavunga ukweli ulivyo.

Sasa hivi wengi tunakaza roho, endapo uchaguzi utafanyika na ukaonyesha unafuu wa kutosha kwamba uvurugaji haukuwa mkubwa kiasi cha kutisha, na Magufuli akishinda katika hali hiyo tutashangilia, sasa tufanyeje kama waTanzania ndivyo walivyoamua kutokana na uzembe wa watu kufanya kazi zao kwa weledi.

Tunasubiri tu, uchaguzi ufanyike katika hali nzuri ya kuridhisha, tutameza vidonge vichungu na maisha yataendelea.

Na safari hii, baada ya kuipoteza nafasi hii, itabidi tusubiri muujiza uzuie kuwa kama Rwanda au Uganda kikamilifu kabisa.
 
Huu ni uthibitisho tosha kuwa hiki si Chama cha siasa tena Bali ni Chama cha kigaidi na wahuni tupu.

Hii inathibitisha kuwa Chama hiki kimekuwa kikiwaonea, kuwadhulumu, kuwafilisi na hata kuwapoteza watu ambao hawakiungi mkono. Ni uthibitisho rasmi kuwa CCM sasa inawafanyia watanzania zaidi ya Mkoloni mzungu alivokuwa akiwafanyia watanganyika.

Ni vizuri upinzani tukadhihifadhi hizi clips for future reference huko mbeleni tukianza kuwawajibisha hawa mashetani kwa huu ushetani wao.

Ni vizuri hizi clips kuwekwa na kutumwa hata kwa wafadhili wao wakiwemo kina Pompeo na vyombo vya kimataifa kama Al Jazeera na hata Umoja wa Mataifa ili wajue wanafanya Kazi na watu wa namna gani.

Ni dhahiri pia kuwa kwa haya yote hakuna budi kwa watanzania kutafuta Chama mbadala mwaka huu. CCM lazima wapumzishwe mwaka huu si kwa ushetani huu wanaouongea waziwazi
 
Ni hivi hivi, mchana kweupe, upinzani unaanza kuchimbwa na wao wakishangilia kama inavyoonekana hapa.

Ukiachana na hivyo vitisho vya kipuuzi, angalia hawa mnaowasema kila siku akina Popole wanavyochakarika na kazi ndani ya chama wakifanya mikakati kila mahala, hata ile isiyokuwa halali na ambayo haitangazwa na kushangiliwa humu kwa sasa hivi.

Wapinzani kuja kustuka, too late, wamekwishafungwa goli! Mambo ni yale yale ya siku zote, lakini hakuna funzo linalosomeka.

Hawa, akina Popole, wapo sana huku vijijini, viongozi wa mashina wanatogota kimya kimya, wapinzani ndio kwanza wanajionyesha mijini.

Akina Popole wakiwafunda wagomea wao kila mahali, na kuwapa mbinu za kujaza fomu, wagombea wa upinzani watajaza fomu kama hawajawahi kaa darasani'
Halafu wanapokatwa kwa sababu za kipuuzi kabisa, upinzani ndio wanalilia wananchi wawaonee huruma!

Haya tunayaandika sio kwa furaha, lakini uzembe unapotokea hakuna sababu ya kuvungavunga ukweli ulivyo.

Sasa hivi wengi tunakaza roho, endapo uchaguzi utafanyika na ukaonyesha unafuu wa kutosha kwamba uvurugaji haukuwa mkubwa kiasi cha kutisha, na Magufuli akishinda katika hali hiyo tutashangilia, sasa tufanyeje kama waTanzania ndivyo walivyoamua kutokana na uzembe wa watu kufanya kazi zao kwa weledi.

Tunasubiri tu, uchaguzi ufanyike katika hali nzuri ya kuridhisha, tutameza vidonge vichungu na maisha yataendelea.

Na safari hii, baada ya kuipoteza nafasi hii, itabidi tusubiri muujiza uzuie kuwa kama Rwanda au Uganda kikamilifu kabisa.
Mkuu ni mgeni kwenye Nchi hii? Hujui tangu 2015 CCM ndio wameruhusiwa kufanya siasa peke yao? Mara ngapi hata vikao vya ndani vya wapinzani vinavamiwa na Polisi....
 
Hahaha wameanza na kudanganywa eti wanafanyiwa na vetting kabisa, sasa kuna mijinga inaanza kuota ukuu wa wilaya, mkoa, n.k.

CCM waoga lakini nao wanatishana.
 
Tusinyimane uhuru wa kufunga.( freedom of association) kwani kuhamia chama kingine ni haki ya msingi. Vitisho si utamaduni wa Tanzania au ndo CCM mpya
 
Ccm sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha kijeshi kilichojivika koti la chama cha siasa. Na bila tume hii ya uchaguzi, na vyombo vya dola, ccm haiwezi kushinda uchaguzi.
Nimeipenda komenti yako
 
Wadau wa AMANI TANZANIA,

Hayo maneno, tutakufuata hukohuko kwenye kazi serikalini au kwenye biashara yako,

Je, siyo UCHOCHEZI?

NI VITISHO KWA WAPENDA AMANI NA DEMOKRASIA NCHINI.

WAHUSIKA KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE TUTIMIZE WAJIBU.

KUNA JINAI KWENYE KAULI HIYO.
 
Back
Top Bottom