GE2025 Watia nia wa CCM wanaswa live wakigawa vitenge na fedha kwa wajumbe

GE2025 Watia nia wa CCM wanaswa live wakigawa vitenge na fedha kwa wajumbe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mara imewakamata wanachama saba wa Chama cha Mapinduzi kwa tuhuma za kugawa fedha nje ya ukumbi wa uchaguzi Musoma vijijini, huku baadhi ya watia nia wa nafasi ya udiwani viti maalumu wa chama hicho wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, ambapo wameonekana katika picha mjongeo mtandaoni, wakigawa fedha na vitenge kwa wajumbe kuwashawishi wawachague katika kura za maoni .



============

​
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mara imeeleza kuwahoji watu tisa wanaodaiwa kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wakihusishwa na mchakato wa uchaguzi wa viti maalum katika wilaya za kichama za Musoma Mjini na Musoma Vijijini. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara, Mohamed Shariff amesema uchunguzi wa matukio hayo bado unaendelea, ingawa amesema kumekuwa na changamoto kadhaa katika utekelezaji wa kazi hiyo, ikiwemo vikwazo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama husika
 
Wameona kanga ndio kipaumbelee Cha wananchi kweli ktk miaka 60 hii ya uhuruuu🤔🤔🤔

Inasikitisha sanaa
 
Back
Top Bottom