Uchaguzi 2020 Watia nia wengi 2020 bomu jipya kwa CCM | wataiangusha CCM 2025

Uchaguzi 2020 Watia nia wengi 2020 bomu jipya kwa CCM | wataiangusha CCM 2025

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Ukiona kunguru wengi sehem ujue kuna mzoga.

Kwenye mada: Kwanza kabisa tunapaswa kukumbuka kuwa hii ni rekodi mpya kwa watia nia wa Ubunge.

Katika tafiti za kawaida tu inaonyesha ukosefu wa ajira na kukimbilia maslahi makubwa bila kuwa na sera zenye tija,kweli wote watakuwa na nia ya kuwatumikia watanzania? Kama ndio kwanini mtu aache kazi akatafute kazi? Uache uRC ukagombee ubunge? Kwani huko haukua ukiwatumikia watanzania?.

Watakao katwa pamoja na watakao shindwa ubunge watatoka na hasira kali sana na kutakuwa na wimbi la wakosoaji wengi sana kipindi hichi,kipindi cha utawala wa Magu waliotumbuliwa,wenye vyeti feke wapiga dili wote hao. Jambo ambalo litafanya CCM ichukiwe au kutokeza makundi mengi.

Hitimisho.
Kutokana na vuguvugu hilo lazma wengi wawe na hasira ya kuitoa ccm kwa hali yoyote ile. Kwaio usemi wa Nyerere wa atakaeiangusha CCM ni CCM wenyewe. Ni hayo tu.

(Mchambuzi mdogo wa mambo ya kisiasa na kijamii)
 
Wingi wa wagombea CCM ni dalili mbaya sana, kwa sababu ndio inaleta hatari kubwa sana ya "MPASUKO MKUBWA" ndani ya chama pindi watakapo katwa majina walio wengi wao (Asilimia kubwa ya hawata ridhika pindi panga likipita).

Sasa chukua hao watakao kutana na "PANGA", jumlisha "WAFANYABIASHARA (Waliofilisiwa/Tapeliwa/Walioonewa na TRA/BODI YA MADINI), VIJANA WASIO NA AJIRA, WAKULIMA WALIOKAANGWA BEI ZA MAZAO, MADEREVA WALIOBAMKIZIWA FINE BARABARANI (MABASI, BAJAJI, BODABODA, DALADALA), WANANCHI WALIOTOLEWA MANENO YA DHARAU NA VIONGOZI, WANANCHI WALIOBAMBIKIZWA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI NA JINAI, WALIOTUMBULIWA, WALIOTEKWA/KUPOTEZWA/KUULIWA.

Usisahau na hasira za wananchi dhidi ya "UTAPELI" uliofanyika kwenye "UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA".

Majibu ya kasheshe watakayokutana nayo CCM #Uchaguzi2020 utayapata.

CCM tatizo lao ni ubishi na kujisifia kupita kiasi, ila kwa wenye akili hio ni dalili ya kushtua sana.
 
Tuanze na msemo wako... 'ukiona kunguru wengi...' kunguru original hawakusanyikii mzoga, labda kunguru fake wa Dar.

Wanaokusanyikia mzoga ni tai vishingo wasiokuwa na manyoya kichwani (mbeshi) waishio maporini huko kusorolea mizoga na uozo!

Tukija kwenye point yako, tayari umekwisha kusahau kuupima upepo wa hawa wanaojiita watia nia!

Huu 'utoto' na mzaha wa 'kuchukua fomu', kama makaratasi yasiyokuwa na thamani uliasisiwa na watia nia wa ugombea urais mwaka 2015, je unakumbuka waliochukua fomu walikuwa ni wangapi kugombea nafasi1?

Na baada ya kukatwa ilikuwaje? Kwa hiyo ni lazima kwanza tupime kuanzia hapo, labda wanaweza kuwepo ila kwa uchache mno kama ilivyotokea kwa Membe.

Hawa unaosema wewe watageuka kuwa wapinzani si kweli,hao wataishia kujichekesha chekesha kama chama chao kinavyoagiza kuwa atayeshindwa lazima amuunge mkono aliyeteuliwa.

Watapimwa kwa hilo, na atakayenuna wanamMembefy mapema kama mfano, abakie kulia tu na miti.

Hawana umoja kusema wakiisha kukatwa majina watapata muda tena wa kukusanyika na kuanza kujadili, hilo halipo kila mmoja ataenda kufia mbele kivyake.

Kipindi kilichopita waliokatwa na kuchujwa kwenye huo mchakato wa ubunge, wengi wao waliambulia teuzi za ukuu wa mikoa na wilaya, lakini safari hii sidhani kama Magufuli ataitumia tena njia hiyo dhaifu ya uteuzi, keshajifunza kutokana na viburi na kutoridhika na madaraka anayowapa wateule wake hao.

Nikwambie tu kwamba, hakuna lolote watakalofanya hao watakapokatwa majina yao, maana wengi wao hawana 'impact' yoyote katika jamii, ni wasaka tonge kwa ajili ya chakula cha kushibisha matumbo yao na familia zao si wanasiasa ni wanamaslahi.

Embu tukae tusubiri tuone mambo yatakavyokuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Ukiona kunguru wengi sehem ujue kuna mzoga.

Kwenye mada: Kwanza kabisa tunapaswa kukumbuka kuwa hii ni rekodi mpya kwa watia nia wa ubunge.

Katika tafiti za kawaida tu inaonyesha ukosefu wa ajira na kukimbilia maslahi makubwa bila kuwa na sera zenye tija,kweli wote watakuwa na nia ya kuwatumikia watanzania? Kama ndio kwanini mtu aache kazi akatafute kazi? Uache uRC ukagombee ubunge? Kwani huko haukua ukiwatumikia watanzania?...
Nikupe hongera kwa matarajio yako ya CCM kuparaganyika kwa sababu ya kuwepo wagombea wengi. Tofauti na wenye mawazo kama yako (kuanguka kwa CCM) wanaoshutumu CCM kuwa na mgombea mmoja wa Urais aaliyejitokeza

Kwa hoja yako hiyo ina maana vyama vya siasa vyenye wagombea wengi kiti kimoja km Urais au jimbo moja ni dalili za uhasama na si ukuaji wa demokrasia au watu kutambua maana ya uwakilishi.

Tuombe matarajio yako yatafanikiwa
 
Sababu kubwa ni ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha na sio etii UKUAJI WA DEMOKRASIA kama wao wanavyodai.
Vijana wengi waliotiania CCM, wanajulikana ni vyama vya upinzani hasa CDM.
 
Tuanze na msemo wako....'ukiona kunguru wengi...' kunguru original hawakusanyikii mzoga, labda kunguru fake wa Dar.

Wanaokusanyikia mzoga ni tai vishingo wasiokuwa na manyoya kichwani (mbeshi) waishio maporini huko kusorolea mizoga na uozo!

Tukija kwenye point yako, tayari umekwisha kusahau kuupima upepo wa hawa wanaojiita watia nia!...

Naunga mkono hoja yako. Kwanza system ya jiwe ukimsema au kumpinga kwa lolote unapigwa Bakora hiyo peke yake inatosha baada ya watu kukatwa kutawanyika.

Kwa Taifa la watu wanaojitambua kama kumletea noma Jiwe angeshaletewa kitambo, Vyeti feki huku kamkumbatia Madereva akituhumiwa na vyeti feki hivyo hivyo.

Yapo mengi sana kama ndio noma ingekuwa ishaletwa. Lakini ndio Taifa la mafisi, unaonewa halafu unaunga mkono kuonewa kwako.
 
Ukiona kunguru wengi sehem ujue kuna mzoga.

Kwenye mada: Kwanza kabisa tunapaswa kukumbuka kuwa hii ni rekodi mpya kwa watia nia wa ubunge...

Kama kweli wewe ni mchambuzi wa mambo ya siasa na kijamii basi utakuwa unalisha watu matangopoli.

Ukiona watia nia wengi ndani ya chama , basi ujue chama hicho kina demokrasia, na ni chama kisicho na mizengwe.

Mfano wake jifunze zama za Elimu bure na Elimu ya kulipia watoto wengi waliandikishwa kipindi gani.

Ukipata hilo jibu utakuwa umejijibu.
 
Wote mmeangalia kwa narrow eye. Tuseme ukweli:

1. Wingi huu unaonyesha kukua sana kwa demokrasia yaani waziwazi wananchi wanakua na choice kubwa.

2. Kwetu ambao ni wana CCM kamili kwa miaka 30 tumethibitisha Chama kina mvuto hata ngedere wa kule kama kina Silinde, Nasarinja wengine wamekielewa.

3. Katika hao wengi atakaechaguliwa atakua na nidhamu Ata piga kazi sababu anajua kuna wengi wenye sifa yaani mwaka huu sio kupita ni kupenya na hatakua na hati miliki ya jimbo.

4. Hazina ya kifedha na rasilimali watu inaonekana wazi ndani ya CCM.

5. Ikiwa Magufuli anataka safu bora basi aangalie ya mwaka huu..

6. Ila Wasira, Mtemvu, Kapuya mmechukua fomu tena kwani CCM imewakosea nini mnataka kufa nayo jamani?!
 
Kama kweli wewe ni mchambuzi wa mambo ya siasa na kijamii basi utakuwa unalisha watu matangopoli.

Ukiona watia nia wengi ndani ya chama , basi ujue chama hicho kina demokrasia, nanichama kisicho na mizengwe...
Acha kupotosha umma, hao watia nia wote njaa zinawasumbua na sio ukuaji wa demokrasia
 
Kama watu wenye sifa wameshakua wengi kiasi hicho ndani ya chama basi kuanzia sasa nafasi za ubunge zitangazwe kama nafasi za ajira, wagombea watume CV zao, wafanyiwe interview atakaepita ndio awe mgombea.
 
Mkuu Kama Wana njaa wamepata wapi sh. Milioni moja ya fomu? Manake fomu zinauzwa kiasi hicho
Form ni laki tu, nimesema wana njaa kutokana na kua hawaridhiki na madaraka waliyonayo. Mfano tu kesho wakitangaza kua ubunge ni kazi ya kujitolea sidhani kama utasikia watia nia
 
Form ya ubunge ni laki moja mkuu, Diwani elfu kumi tuu
So kweli mkuu Nina jamaa zangu 2 wanagombea gharama ni fomu laki moja na 1M mnachangia uendeshaji wa chama jumla nu hiyo milioni moja na laki moja uliza mtu yeyote aliyegomea
 
Form ni laki tu, nimesema wana njaa kutokana na kua hawaridhiki na madaraka waliyonayo. Mfano tu kesho wakitangaza kua ubunge ni kazi ya kujitolea sidhani kama utasikia watia nia
Nina jamaa zangu 2 wanagombea fomu ni laki moja na 1M mnachangia uendeshaji wa chama jumla ni 1.1M uliza waliogombea watakuambia
 
Kama kweli wewe ni mchambuzi wa mambo ya siasa na kijamii basi utakuwa unalisha watu matangopoli.

Ukiona watia nia wengi ndani ya chama , basi ujue chama hicho kina demokrasia, na ni chama kisicho na mizengwe.

Mfano wake jifunze zama za Elimu bure na Elimu ya kulipia watoto wengi waliandikishwa kipindi gani.

Ukipata hilo jibu utakuwa umejijibu.

Irelevant.
 
Back
Top Bottom