Wingi wa wagombea CCM ni dalili mbaya sana, kwa sababu ndio inaleta hatari kubwa sana ya "MPASUKO MKUBWA" ndani ya chama pindi watakapo katwa majina walio wengi wao (Asilimia kubwa ya hawata ridhika pindi panga likipita).
Sasa chukua hao watakao kutana na "PANGA", jumlisha "WAFANYABIASHARA (Waliofilisiwa/Tapeliwa/Walioonewa na TRA/BODI YA MADINI), VIJANA WASIO NA AJIRA, WAKULIMA WALIOKAANGWA BEI ZA MAZAO, MADEREVA WALIOBAMKIZIWA FINE BARABARANI (MABASI, BAJAJI, BODABODA, DALADALA), WANANCHI WALIOTOLEWA MANENO YA DHARAU NA VIONGOZI, WANANCHI WALIOBAMBIKIZWA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI NA JINAI, WALIOTUMBULIWA, WALIOTEKWA/KUPOTEZWA/KUULIWA.
Usisahau na hasira za wananchi dhidi ya "UTAPELI" uliofanyika kwenye "UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA".
Majibu ya kasheshe watakayokutana nayo CCM #Uchaguzi2020 utayapata.
CCM tatizo lao ni ubishi na kujisifia kupita kiasi, ila kwa wenye akili hio ni dalili ya kushtua sana.