Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
WATIBELI SIO MBUZI WA KAFARA. KAMWE HATUTAKUBALI KUGEUZWA CHAMBO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Sisi tunaongozwa na mambo makuu manne; HAKI, AKILI, UPENDO NA UKWELI. Hayo ndio yanayotuongoza na ndio mhimili mkuu katika maisha yetu.
2. Huwezi mgeuza mtibeli mbuzi wa kafara au chambo. Never! Kamwe! Sisi hatutumiki kwa majaribio. Sio watu wa namna hiyo.
3. Hatupo upande wa waovu, wadhulumaji, wauaji, watekaji, mashoga, wauza madawa, wachawi n.k.
4. Lakini pia kamwe hatuwezi kuwatetea wanaodhulumiwa ambao ni wanafiki, waoga, wabinafsi, wasio na upendo, wasiojua thamani ya kupiganiwa. Hilo hatutaweza na tunajisikia fahari.
5. Watibeli tunaamini huwezi msaidia mtu ambaye hajaomba msaada, pili, huwezi msaidia mtu ambaye haoni kama yupo kwenye matatizo,
Huwezi msaidia mtu ambaye wewe unaona anaonewa lakini yeye anamwona anayemuonea ni mwema.
Tunajua, msaada wakati mwingine si suala tuu la kifalsafa bali pia la kisaikolojia.
6. Watibeli moja ya udhaifu wetu ni kutoumizwa na maoni au mitazamo ya wengine kutuhusu. Kwa sababu tumezaliwa haki ikiwa ndani yetu. Tunajua watu wengine wanahaki juu ya uelewa, maoni na mitazamo yao vile watakavyoona.
Ni udhaifu kwa sababu tunatamani na sisi tuumie kama wengine wanaoumia wakisikia maoni ya wengine dhidi yao. Tunahisi huo utakuwa ni ubinadamu na hiyo inatufanya tujione tunakasoro fulani. Kwamba kwa nini hatuumizwi na maoni ya watu wengine?
7. Tunatetea wanaohitaji kutetewa. Tunatetea ambao wapo tayari kutetewa.
Tunatetea muda sahihi ukifika.
8. Hatukwazwi na wengine kujitoa mhanga wala hatukwazwi kwa wengine kutolewa kafara au kufanywa chambo. Wana haki zao na hatuwalaumu.
9. Ila hatupo tayari kuingizwa kwenye mbuzi wa kafara au chambo kwa jambo ambalo halina Akili(matokeo mazuri).
Kwetu matokeo mazuri ni sehemu ya mpango. Hatuwezi kufanya jambo kwa ku-bet hasa jambo linalohusu uzima na kifo.
10. Mfano kwenye Oktoba 29.
Hatuoni shida watu wakiandamana kwa kudai haki zao. Hatuoni tatizo wao kufanya hivyo.
Na hatuoni tatizo wengine wakienda kutiki(kupiga kura) hatuoni tatizo.
Kila mtu anahaki katika hilo.
11. Tatizo ni pale mmoja anapozuia haki ya mwingine. Mfano; Wakuandamana azuie mwingine asiende kupiga kura. Au wakupiga kura amzuie wakuandamana. Hiyo sio Haki.
12. Watibeli tunajua watu wa kawaida hawapendi Ukweli ila wakati huohuo wanajifanya wanapenda HAKI.
Huwezi kupenda haki wakati huohuo hutaki UKWELI.
13. Watibeli kikawaida ni watu wa daraja la juu. Hivyo ni vizuri kuwaelewa mitazamo yao, falsafa zao, imani zao, fikra zao ili wasije wakakusumbua akili yako. Ujue wanafikiria kwa namna ipi.
Kama hilo litakusumbua basi mfano wewe ni Mzazi angalia vile unavyomchukulia mtoto wako, mtazamo wako juu yake, hivyo ndivyo watibeli tulivyo.
Au Mwalimu na mwanafunzi
Au Mwajiri na mfanyakazi
Au Hakimu na mshtaki au mlalamikaji.
14. Kwa hiyo kwa namna yoyote unapokutana na mtibeli lazima ujue yeye anakuona upo chini yake. Hasa usipokuwa mtibeli mwenzake.
Vyovyote utakavyofanya, utakavyokuwa, utakavyojiona, vyovyote vile kama wewe sio mtibeli basi mtibeli atakuona upo chini.
Ni vizuri kama sio mtibeli kujitahidi kuwaona watibeli wapo chini yako ili isikuumize kama una roho ndogo.
15. Ukishakuwa mlalamikaji, unaona unaonewa, unahitaji msaada kwa mtu mwingine ambao wewe huwezi kufanya mwenyewe, unafika ofisini au popote unataka kuzingatiwa badala ya kuzingatiwa kuwepo automatically basi jua wewe upo chini tuu. Wewe sio Mtibeli.
16. Ukiona mkeo au watoto hawakuheshimu, na unataka heshima na unaiona ya maana sana. Heshima ambayo haiji naturally. Jua wewe upo chini kuna mambo Una lack na sio mambo ya nje bali ya ndani yako mwenyewe.
17. Ukiona umeenda ukweni wanakuletea dharau, hawakuzingatia na unajitahidi kuzingatiwa. Ujue wewe upo chini. Kuna mambo ya ndani unatakiwa ufanye. Ambayo kwa sisi watibeli tuko nayo naturally.
18. Mambo hayo ya ndani ndio ukiyakosa wengine watakutumia kama mbuzi wa kafara au chambo nawe utafanya ili upate kile ambacho ulikuwa unahisi hauna kumbe unacho lakini ubinafsi wako, unafiki wako, ujinga wako, dhulma yako, vilikupofusha.
19. Huwezi lalamika unalipwa mshahara mdogo wakati hujalazimishwa kufanya kazi. Watibeli hatuko hivyo. Udogo wa mshahara ni suala la mindset, mindset ndio inaleta mambo mengine ya bajeti, mipango, malengo n.k. mfumo wa kuajiriwa siku zote ni wa kinyonyaji.
Na ukiamua kunyonywa basi ni haki yako kunyonywa. Ingawaje ni muhimu katika unyonywaji wako upate mahitaji yako ya msingi ya lazima kama chakula, mavazi na malazi.
Huwezi ajiriwa alafu ukapigania haki ya kuongezwa mshahara ili ununue gari au usomeshe watoto shule nzuri. Ni kama huelewi kwa nini umeajiriwa.
20. Robert unakatisha watu tamaa! Nope! Nazungumzia ukweli uliopo.
Usikubali kutolewa kafara au kufanywa chambo kwa watu wasiostahili. Watu wasiojua thamani ya kile unachoenda kukifanya. Watu wabinafsi na wanafiki.
21. Sio level ya kitaifa tuu. Hata Level ya kifamilia.
Baba au mwanaume kamwe usijejitoa kafara kwa mwanamke asiyejielewa, au mwanamke asiye kupenda, mbinafsi, ambaye pesa yake ni yake, yakwako ya wote. Never! Au ujitoe kafara kwa matoto majinga yasiyo na akili, yasiyokutii kama Baba, yasiyo na shukrani. Kamwe usifanye hivyo. Hiyo sio HAKI.
22. Au unalea watoto wa mwanaume mwingine. Wakati baba yao yupo. Huo sio upendo. Huo ni ulofa. Hakuna mwenye akili na mpenda haki atafanya jambo kama hilo.
Tena hukuombwa!
23. Mwenye jukumu la kukuomba umlelee watoto wake ni mwanaume mwenzako yaani baba wa hao watoto sio mwanamke aliyewazaa. Akiweza kufanya hivyo walee. Na bahati nzuri hakuna mwanaume atakuja akuombe mwanaume mwenzake unayeishi na mwanamke aliyemzalisha umlee mtoto wake. Na kama hakuna unagundua wewe ni mbuzi wa kafara tuu uliyekosa akili na usiyejitambua.
24. Robert! Mbona unachanganya madesa sasa!
Ndivyo nilivyo!
25. Wewe utetee wengine ambao wao wamejilaza na wake zao huko. Wanakusakizia, nenda nenda, sema sema, wanakupeleka kama chombo, na ulivyo akili mbili unaenda. Kama mbuzi wa kafara isiyo na faida.
26. Yakikukuta! Yanapiga mayowe mwezi mmoja. Kisha yanakuweka dampo huko. Yanatafuta mbuzi mwingine. Nend! Nenda! Wewe ni shujaa. Historia itakukumbuka! Nyokonyoko! Nawe unaenda tena hujifunzi kwa mbuzi aliyetangulia. Unaenda mizimu inakata kichwa.
27. Kuna wakati mbuzi wa kafara ananusurika kutolewa kafara,, akili zinamrejea. Anasema mimi siendi atokee mwingine aende. Walewale alioenda kujitolea kwaajili yao wanaanza kumzomea. Toka hapa! Mnafiki wewe, kwanza muoga wewe, umepewa pesa wewe na mizimu mbona hawajakuchukua mbuzi mee wa kafara. Wanakutukana.
28. My friend, ogopa watu ambao wanajificha nyuma alafu wanakuambia wewe nenda tuko nyuma yako. Ogopa sana kwenye maisha yako. Usijaribu.
29. Hata kama unanguvu ya kuwatetea kamwe usimtetee mtu wa hivyo. Ambaye anaogopa kufa kwaajili ya haki yake lakini anataka wewe ufe kwaajili yake. Never! Usijaribu kujitoa kafara kwani itakuwa umejidhulumu pakubwa. Na kama mbingu itakuwepo hautaenda Kamwe!
Acha nipumzike sasa
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam