Watiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwatapeli kimapenzi 'mishangazi' mtandaoni

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Raia wa Ghana Frederick Kumi maarufu mtandoni ‘Abu Trica’ amekamatwa kwa tuhuma za utapeli wa kimapenzi na kuwaibia wazee na watu wazima ambao ni Wazungu nchini Marekani kiasi cha fedha Dola milioni 8 za Marekani.

Waendesha mashtaka wa Marekani wanasema kijana huyo mwenye miaka 31, alitumia zana za akili bandia (AI) kuunda utambulisho usio wa kweli, pia aliwasiliana na waathiriwa kupitia tovuti za kutafuta wapenzi na mitandao ya kijamii, kisha polepole akajenga imani yao kabla ya kuwaomba fedha.

Abu Trica anakabiliwa na mashtaka nchini Marekani ya kula njama ya kufanya udanganyifu wa kielektroniki (wire fraud) na utakatishaji wa fedha na akipatikana na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 jela.

Wachunguzi wanasema Abu Trica, ambaye pia hutumia jina jingine Emmanuel Kojo Baah Obeng, amekuwa akiwasiliana na kina mama hao watu wazima kupitia simu, baruapepe na ujumbe wa maandishi.

Inadaiwa mbinu ambayo hutumia kuwapata huanza kwa kuwaeleza taarifa za kusikitisha zinazomhusu za kiafya, matatizo ya safari au fursa za biashara akiwa na lengo kuwashawishi kutuma fedha au vitu vya thamani.
 
mishangaz mitamuu mazee dah...mwenzenu naipendaa:AMOGUS::BatChesting:😀
1000237069.jpg
1000237070.jpg
 
Emmanuel 'Kojo'.... Abu'Trica', nimajina ya kitapeli ya wazi, hao mishangazi walishindwa kujihoji?
 
Hao miaka ya tisini walitambulika kama "Yahoo Boys" wamewapukutisha sana wazungu.

"Scammers"
 
Sa hv ndo weng Mpaka FBI wanaenda kuwakamata
Yeah, huku kwetu, kuna demu yuko Canada anatokea kukupenda FB, anakuomba urafiki alafu badae anasema anataka kukutumia zawadi ukijaa tu unapigwa.
 
Back
Top Bottom