RR,....umeleta 'unyuzi' mzuri sana. Unyuzi huu unagusa wengi kwa namna moja au nyingineo.
Hapa pia kunahusisha watoto ambao tangu wangali tumboni wazazi wao kwa namna moja au nyingine
walikosa kufikia muafaka wa mimba na mtoto atapozaliwa.
Kuna incidences ambazo mtoto alikoseshwa haki zake na kuja kutambulishwa kwa baba yake siku ya msiba
yaani mwana analetwa kuja kutoa last respect tu kwenye jeneza la baba yake. Bahati mbaya, hili halichagui umri,
kuna wengine wanaletwa wangali wadogo, kuna wengine wanaletwa wakiwa kwenye teen age...
Ni mada nzuri sana na itatufundisha mengi tukiichukulia seriously.