Watoto wetu wanafundishwa ujinga na serikali yetu inalijua hili hivi ni makusudi ya watawala wetu au wasomi wetu wajinga.Leo nimempeleka dogo shule, ana miaka 7,nilipokuwa kuwa naye shule akanionyesha mwalimu mmoja, eti baba unamuona yule mwalimu pale, nikamwambia ndiyo akasema ni muongo balaa.
Nikamuuliza kwanini, akajibu ni mwalimu wetu wa kishwahili lakini huwa anatupigiaga hadithi, eti baba we ushawahi kumuona sungura anaendesha baiskeli au tembo akaitisha mkutano harafu wanyama wote wakaja, nikamwambia amuheshimu mwalimu.