Watoto na mahusiano. . . .

Sidhani kama kuna malezi yanayopelekea moja kwa moja mzazi kutembea na mtoto wake wa kike au wa kiume kwahiyo tusisingizie uzungu wala umarekani maana hata wao wanakataa mambo kama haya.

Katika hili Lizzy ukubali kwamba wazungu wanaruhusu, na nimeshuhudia mwenyewe na kubaki nimeuwaa. Na si kwa kificho bali kwa uawazi kabisa. Huu ni utamaduni wao.

Lakini kuna baadhi hawapendi utaratibu huo na wanawalea watoto wao kwa mtindo kama tufanyavyo waafrika, na wanawasikiliza sana wawaambiapo yanayofaa na yasiyofaa na kwamba lini itawafaa kufanya hivyo.
 

Thanks alot Lizzy, be blessed!!!
 
malezi ya watoto nia pasua kichwa.
Wenye imani, shikeni mlichonacho, wenye kutumia akili zao, zitumieni hasa ili mfanikiwe.
Wanaotaka maisha rahisi bora wasiwe nao tu. .
 

Wazungu hawaruhusu sema wapo watu wanaofanya hivyo kama ambavyo hata kwenye jamii yetu wapo. Tusipende kulaumu kila kitu mzungu, mzungu wakati akili kila mtu kapewa yake. Kuendekeza hizo lawama na mawazo ya aina hiyo ni utumwa wa kifikira.
 
Ahsante Lizzy,

Haya mambo ni mazito sana...Kama ingewezekana, kila couple ilee watoto wao...Bahati mbaya haiwezekani kwa baadhi ya watu!!

Kuna wanawake wanaoogopa kuwaeleza wenzi wao wapya kwamba wana watoto kwa kuogopa kuachika..Hili limewafanya wengi wao kwenda kuwaficha kwa ndugu...Huko wengine wanapata malezi mabaya sana. Na kubwa zaidi wanakosa ukaribu na mama yao!!

Kwa wanaume walio wengi, hawana muda wa kuwa karibu na watoto wao. Wanawacha mikononi mwa mama wa kambo. Wengi wanaishia kuwa abused....

Kuna mzee mmoja kijijini kwetu ambaye aliachana na mke wake huku akiwa na watoto ambao walikuwa ni wakubwa kiasi...Yule mzee alishindwa kuoa tena kwa sababu wanawake walikuwa wanawaogopa watoto wake!!

Babu DC!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…