Watoto na mahusiano. . . .

Watoto na mahusiano. . . .

Sidhani kama kuna malezi yanayopelekea moja kwa moja mzazi kutembea na mtoto wake wa kike au wa kiume kwahiyo tusisingizie uzungu wala umarekani maana hata wao wanakataa mambo kama haya.

Katika hili Lizzy ukubali kwamba wazungu wanaruhusu, na nimeshuhudia mwenyewe na kubaki nimeuwaa. Na si kwa kificho bali kwa uawazi kabisa. Huu ni utamaduni wao.

Lakini kuna baadhi hawapendi utaratibu huo na wanawalea watoto wao kwa mtindo kama tufanyavyo waafrika, na wanawasikiliza sana wawaambiapo yanayofaa na yasiyofaa na kwamba lini itawafaa kufanya hivyo.
 
Kuna watu ambao wamefanikiwa kupata watoto bila ya ndoa na wengine wamefanikiwa kupata ndani ya ndoa ambazo hazikudumu. Mzazi yeyote yule ambae anafahamu/anaheshimu na kutimiza majukumu yake hua anampa/wapa mtoto/watoto wake kipaumbele kwenye maisha yake, haswa linapokuja swala la kuingia kwenye mahusiano au hata ndoa kwa mara nyingine. Najua wapo wazembe wachache ambao hua hawajali furaha na ustawi wa watoto wao kiasi kwamba hua wanaingia kwenye mahusiano na watu ambao hua wanaishia kuwanyanyasa watoto wao kimwili, kimapenzi, kiakili na kihisia. Mbaya zaidi hawa wazembe hua hawako makini, hivyo hua hawagundui kinachoendelea au hata mtoto akiwa na ujasiri wa kusema wanawadharau watoto wao na kuwa upande wa wenzi wao. Wanasahau kwamba watoto (kiujumla) ndio waohitaji ulinzi toka kwa wakubwa against wakubwa na sio wakubwa kulindana against watoto.

Nwy ushauri wangu ni kwa wale ambao wana watoto na wako kwenye mahusiano au wanatarajia kuwa kwenye mahusiano na watu ambao sio wazazi wenza.

Kwa waliopo ndani. . . . .
1. Mtoto wako anakuhitaji kwa kila namna , be there for him/her/them.
2. Kua na muda nae. Fanya utaratibu wa kutenga muda wenu wenyewe bila watu wengine ili kumhakikishia kwamba hujamtenga/chagua mwenzi wako juu yake.
3. Kua msikilizaji. Akikueleza kitu hata kama ni kidogo au kwenye akili yako unaona ni cha kijinga kipe maana mbele yake. Kuna watu wanaishi na wenzi ambao wanawanyanyasa watoto wao sexually ila wanakua kama hawajui kwa kutokua wasikilizaji na kuwa wapuuzaji.
4. Ongea nae.
5. Hakikisha anaelewa kwamba huyo mama/baba mpya hajaja kuchukua nafasi ya mama/baba yake ambae hayupo ikiwa wapo/walikua na mahusiano ya karibu.
6. Hakikisha mwenzi wako anaelewa kwamba watoto wako ni watoto wako, huwezi ukawakimbia wao kwaajili yake. Anapaswa awaheshimu kama sio kuwapenda.
7. Wafundishe watoto wako kumheshimu mwenzi wako ili kusiwe na matatizo kati yao.

Kwa ambao bado wako nje. . .
1. Kuwa muwazi kuhusu kuwa na mtoto/watoto pale unapokutana/anzisha urafiki na mtu ili hata akipenda kuwa na mahusiano na wewe awe anajua fika nini kinachomsubiria.
2. Usisite kumweleza mtu unaetarajia kuanza mahusiano nae umuhimu wa watoto wako kwako.
3. Usimtambulishe kwao mpaka utakapokua na uhakika kwamba urafiki/mahusiano yenu yana malengo. . . hii inasaidia kutowachanganya kwa kuwaletea wajomba/shangazi wapya kila siku.
4. Kabla ya kukubali muwe na mahusiano hakikisha anawapenda (LIKE, FOND OF, ADMIRE) watoto wako nao wanampenda yeye. Kama sivyo hali ilivyo usijidanganye kwamba mambo yatabadilika baadae. Hii itasaidia kukwepa ugomvi ambao utakua unakulazimu kuchagua upande kila wakati.

Namna ya kufahamu kwamba rafiki/mwenzi wako mtarajiwa anawapenda/jali watoto wako, and that he/she is nice to them:
1. Mnapokutana/wasiliana atapenda kujua hali zao pia na sio yako peke yako.
2. Unapowaongelea ukiwa nae (utundu, ukorofi, magonjwa na mengine yanayowahusu) uso anachangamka na sio anaonyesha kuboreka. Hii mtu anaweza akaFAKE ila baada ya muda anachoka.
3. Akiwa karibu nao watoto wanafurahi.
4. Wasipomwona kwa muda watoto wanamuulizia.

Kama kawaida wanaoficha makucha wapo ila ukiwa makini utagundua iwapo mtu anafake kufurahia, kupenda ama kujali watoto wako. Don't love blindly, husisha akili yako ili watoto wasije wakalipa kwa uzembe wako.

Be blessed.

Thanks alot Lizzy, be blessed!!!
 
malezi ya watoto nia pasua kichwa.
Wenye imani, shikeni mlichonacho, wenye kutumia akili zao, zitumieni hasa ili mfanikiwe.
Wanaotaka maisha rahisi bora wasiwe nao tu. .
 
Katika hili Lizzy ukubali kwamba wazungu wanaruhusu, na nimeshuhudia mwenyewe na kubaki nimeuwaa. Na si kwa kificho bali kwa uawazi kabisa. Huu ni utamaduni wao.

Lakini kuna baadhi hawapendi utaratibu huo na wanawalea watoto wao kwa mtindo kama tufanyavyo waafrika, na wanawasikiliza sana wawaambiapo yanayofaa na yasiyofaa na kwamba lini itawafaa kufanya hivyo.

Wazungu hawaruhusu sema wapo watu wanaofanya hivyo kama ambavyo hata kwenye jamii yetu wapo. Tusipende kulaumu kila kitu mzungu, mzungu wakati akili kila mtu kapewa yake. Kuendekeza hizo lawama na mawazo ya aina hiyo ni utumwa wa kifikira.
 
Ahsante Lizzy,

Haya mambo ni mazito sana...Kama ingewezekana, kila couple ilee watoto wao...Bahati mbaya haiwezekani kwa baadhi ya watu!!

Kuna wanawake wanaoogopa kuwaeleza wenzi wao wapya kwamba wana watoto kwa kuogopa kuachika..Hili limewafanya wengi wao kwenda kuwaficha kwa ndugu...Huko wengine wanapata malezi mabaya sana. Na kubwa zaidi wanakosa ukaribu na mama yao!!

Kwa wanaume walio wengi, hawana muda wa kuwa karibu na watoto wao. Wanawacha mikononi mwa mama wa kambo. Wengi wanaishia kuwa abused....

Kuna mzee mmoja kijijini kwetu ambaye aliachana na mke wake huku akiwa na watoto ambao walikuwa ni wakubwa kiasi...Yule mzee alishindwa kuoa tena kwa sababu wanawake walikuwa wanawaogopa watoto wake!!

Babu DC!!
 
Back
Top Bottom