Watoto, SEXUALITY

Watoto, SEXUALITY

Miaka ya nyuma ilikuwa mtu akipata mtoto wa kiume anafurahi mpaka basi, akipata wa kike anaanza kufikiria itakuwaje akipata mimba kabla ya kuolewa. Mtoto wa kike alikuwa analeta wasiwasi kwa baba/mama kwasababu ya 'AIBU' anayoweza kuwaletea wazazi na familia kwa ujumla. Mtoto wa kiume yeye alikuwa anaonekana hana 'AIBU' anayoweza kusababisha maana hata akimpa msichana mimba 'huo ndio uanaume'.

Ila siku hizi hata mtoto wa kiume anaumiza kichwa maana akiwa mkubwa anaweza akampelekea mzazi wake BOYFRIEND badala ya GIRLFRIEND. Yani mzazi anapumua pale mtoto anapokua kijana na kuonyesha dalili za kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti na yake.

Binafsi sina uhakika nachukuliaje swala la ushoga (kuwa gay) linapoongelewa kwa ujumla bila kuhusisha mtu wa karibu yangu. Nadhani naweza nikawa sijali (yani sichukii wala sisupport) kwasababu ni maisha yao. Ila kichwa kinaniuma nikifikiria kwamba kaBebé kangu kanaweza kuangukia huko. Mungu amuepushie hali hiyo lakini nimejikuta nikijiuliza kama mzazi. .ikitokea akawa hivyo ntachukuliaje, ntaikubali hiyo hali,ntamsupport, ntamtenga? I don't know. Inabaki kuwa ni mtihani ambao namuomba Mungu aniepushe nao. Maadam nilizaa mtoto wa jinsia ya kiume basi awe attracted na jinsia ya kike.

Wewe je, ikitokea mtoto wako wa kiume au hata ndugu/rafiki akawa shoga utafanyaje? Utakubali hali yake na mkaendelea kuwa karibu kama awali? Utamtenga? Utakasirika? Utamsupport kwenye hali yake hiyo?
Duuh
 
Back
Top Bottom