SoC04 Watoto wa Kitanzania wenye mabadiliko

SoC04 Watoto wa Kitanzania wenye mabadiliko

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mordecai Kilosa

New Member
Joined
May 24, 2024
Posts
4
Reaction score
1
Nchi ya Tanzania ni nchi iliyobarikiwa Sana kwa rasilimali nyingi na yenye watu wenye wenye moyo na kuwajibika. Nchi yetu iliweza kupambana na kuondoa ukoloni na pia kuingiza sera ya ujamaa na kujitegemea.

Katika hili tunajivunia kuwa na viongozi waliokua na maono juu ya nchi yao na kuwa na mitazamo chanya yenye athari kijamii.

Familia ni eneo muhimu Sana kwa nchi ili kuweka nguvu zetu ili kuhakikisha wazazi au walezi Wanasimamia vyema maswali ya malezi mazuri ya watoto na ukuaji kwa ujumla ili upate watu wazuri ni lazima uwe na mipango mizuri na maarifa ya kutosha kuhusu mipango husika.

Pia kwenye hili, nimejifunza Sana kwa watoto wengi wadogo katika mazingira yangu ya kazi zangu za kijamii nimewaona wameharibiwa kiasaikolojia na familia zao. Kwa Maana ya kwamba wamekosa utulivu wa kiakili na Ile Hali ya upendo Kutoka kwa watu wao wa karibu.

Wazazi au walezi katika hili wanahusika katika kupelekea athari kubwa kwa hawa watoto. Kwa asilimia 60.45 na kuendelea tafiti niliyofanya Kutoka katika huduma ninazofanya mashuleni shule za msingi na sekondari, nimegundua watoto wamekosa malezi Bora Kutoka kwa wazazi na walezi wao.

Kama taifa tulikuwa na mpango Gani juu ya vizazi vya baadae katika swala la uadilifu na tabia kwa ujumla Kutoka kwa vijana hao wa kesho?!

Ni rahisi kusema ni swala la walimu kufundisha na viongozi wa dini lakini hili sio hivyo tunavyodhani?! Katika maswala ya kisayansi, vinasaba vya mtu yoyote duniani aliyezaliwa na wazazi kwa kawaida kupitia asili ya kibinadamu, mtu ni kiumbe kitokanacho na vinasaba viwili, X au Y yaani Baba au Mama.

Asili hili hutengeneza Moja kwa Moja tabia zake za ndani, muonekano wake wa nje Kutoka kwa wazazi. Nadhani elimu hii kwa wanaofahamu inaweza ikaeleweka kwa haraka. Lakini Kuna elimu nyingine nimenukuu Kutoka katika Biblia, Kitabu Cha Ezekiel 16:44 "...akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake."

Vizazi vyetu vinaakisi maisha yetu wazazi na maadili au tabia zetu wazazi, hivyo Kuna umuhimu mkubwa wa kutengeneza vijana kutokea kwenye familia ZETU kwa njia ya kuwalea watoto kulingana na umri wao.

Hapa ni eneo la kuweka nguvu na juhudi katika malezi aidha kutumia Imani yenye kumpeleka mtoto kujua makusudi ya kuzaliwa kwake na kumfundisha mipaka ya kimaisha katika ngazi zote kipindi Cha ukuaji wa mtoto.

Hekima ni sehemu ya viongozi wetu wa serikali kulisemea hili liwe ni sheria kwa nchi yetu na sio kusubiri madhara na kizuia mitandao ya kijamii inayovunja maadili Maana Teknolojia ni kitu kizuri Sana kwa maendeleo ya maisha hasa katika kujenga urahisishaji wa miundombinu rafiki kwa wasomi wetu na vijana wetu.

Lakini pia eneo ambalo Tanzania tunatamani kufika lakini bado, ni kuwaona watoto wetu wadogo wana buni na kuvumbua vipaji vyao wakiwa bado wadogo, hasa wakitokea mashuleni na hasa kwenye taasisi mbalimbali binafai na za kidini kisudi kuwapa motosha watoto hawa na kuwafanya kuwa na shauku na hamu ya kufanya vitu Bora zaidi vya kimaendeleo kipindi chao wakiwa wadogo.

Maisha ya watoto wengi yenye furaha au huzuni yanaanzia na kichangiwa na wazazi au walezi wao, hili sisemi kuwa wazazi wanamakosa bali ni kawaida pale mtu anapokosa maarifa juu ya jambo Fulani hupelekea anguko au uharibifu mkubwa kwake, kwa familia yake, jamii yake na hata taifa lake.

Hili ni jambo linalohitaji maarifa na sio tu kwa elimu za duniani pekee hata kwa kupitia maandiko ya vitabu vitakatifu pia nimenikuu kwenye kitabu cha Biblia, Hosea sura ya 4 na mstari wa 6 ikisema, " Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako".

Tukitafakari namna ya kuweza kufanikisha jambo hili, tunaweza kupata majibu katika hili kwa kuingia kujifunza maarifa kwa watu waliojariwa maarifa na hekima katika kitengo muhimu Cha watoto hasa wale wanaohitaji kufikiwa waliokosa malezi Bora na pia kuanzisha vitengo au elimu ya malezi katika ngazi zote kuanzia Shule za Awali hata Vyuoni walipo vijana wetu wote.

Katika haya mawazo ambayo nimejaribu kushiriki kwa taifa langu Mimi kama mdau pia na ni mwalimu wa hawa watoto nimejifunza mambo mengi Kutoka kwao na wamenieleza mengi watoto wanayokumbana nayo na mengine sio rahisi kuyasikia Kutoka kwao ila kwa kuwa ni jambo la utaalamu ya maarifa haya basi wanatueleza kwa kuwa wanatuamini.

Nipende kusema, Tanzania ni nchi nzuri Sana mpaka Sasa eneo kubwa ambalo kulingana na sensa ya taifa ya kuanzia 2012 na hivi karibuni pia hesabu ya idadi ya watoto na vijana kuwa ni kubwa kulinganisha na watu wakubwa.

Hivyo kama taifa hili ni jukumu la Kila mdau kwenye hili hasa serikali na viongozi wa dini nchini kuwaelimisha wazazi na walezi na watoto Kila panapowezekana na kuwa ni jambo endelevu na lengo ni kutatua matatizo ya jamii kwa urahisi kupitia familia kwa mtu mmojammoja, kwa jamii, na kwa taifa kwa ujumla.

Napenda kumshukuru Mungu Sana kwa kutupa Raisi Mwanamke Samia Suluhu Hassan hivyo natumai atakapo kaka na wadau ambao ni waelevu katika maswala ya malezi na ninaamini ataweza kupata Suluhu kwenye hili Mama yetu Samia Suluhu Hassan.

Kwa hiyo, kulingana na mawazo haya niyalete kwenu wadau wa Jamii Forum nipende kuwashukuru pia kwa kunipa nafasi kuchangia yangu ya moyoni katika "Stories of Changes 2024" basi ningependa kuwaombea kwa Mungu, kwa Jina la Yesu Kristo.

Nikitamani muwafikie watu wengi zaidi wenye mawazo mazuri na kuyaleta kwenye jamii yetu ya watanzania na Tanzania yetu, kubadilishwa na kuwa ya viwango na nchi za wenzetu kuiga nchi yetu katika malezi Bora ya watoto kuanzia chini hata vijana wetu wa shule za elimu ya juu.

ASANTENI SANA.

MWENYEZI MUNGU IBARIKI JAMII FORUMS, MBARIKI RAIS WETU SAMIA NA VIONGOZI WETU WOTE NA WATOTO WA TANZANIA WOTE.

TANZANIA NAKUPENDA SANA NCHI YANGU NIWAPO DUNIANI NITAKUCHAGUA WEWE, NITAKAA NDANI YA MIPAKA YAKO NA NITAKUOMBEA SIKU ZOTE.
 

Attachments

  • IMG_20240307_160557_450.jpg
    IMG_20240307_160557_450.jpg
    2.3 MB · Views: 12
Upvote 2
Maisha ya watoto wengi yenye furaha au huzuni yanaanzia na kichangiwa na wazazi au walezi wao, hili sisemi kuwa wazazi wanamakosa bali ni kawaida pale mtu anapokosa maarifa juu ya jambo Fulani hupelekea anguko au uharibifu mkubwa kwake, kwa familia yake, jamii yake na hata taifa lake.
Akili za mzazi/mlezi zianze kufundishwa na kupimwa kama anayo hikma ya kulea watoto?
Hili ni jambo linalohitaji maarifa na sio tu kwa elimu za duniani pekee hata kwa kupitia maandiko ya vitabu vitakatifu pia nimenikuu kwenye kitabu cha Biblia, Hosea sura ya 4 na mstari wa 6 ikisema, " Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako".
Na maarifa yapo, makala zipo, vitabu na semina vipo. Kwa hivyo mzazi na mtoto wanaoyakataa maarifa, wanaokataa kujifunza, kufundishwa na kufundishika wamejikatalia furaha wao wenyewe. Iko wazi.
 
Back
Top Bottom