Watoto wa kiume 1,114 walilawitiwa mwaka 2021

Watoto wa kiume 1,114 walilawitiwa mwaka 2021

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Waziri wa maendeleo ya Jamii wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema katika kipindi cha mwaka jana pekee watoto wa kiume wapatao 1,114 wamelawitiwa ambapo ni sawa na wastani wa watoto 93 wa kiume wanafanyiwa ukatili huo kila mwezi.

Waziri Gwajima ametoa takwimu hizo Leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike na kueleza kwamba asilimia 60 ya vitendo hivyo vinatokea kwenye makazi ya familia.

Kuhusu watoto kuolewa wakiwa na umri mdogo chini ya miaka 18 waziri Gwajima amesema tayari serikali kupitia wizara za kisekta imeanza kufanya mapitio ya sheria ya ndoana kwa sasa tayari maoni yameshaanza kuchukuliwa na timu bado inaendelea kukusanya maoni ya wananchi kwa hatua zaidi ikiwemo kufikishwa bungeni

Katika maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike baadhi ya wasichana wametumia maadhimisho hayo kuiomba serikali kuondoa kodi kwenye taulo za kike huku wakikipongeza kituo cha EATV kupitia kampeni yake ya namthamini kwani imekuwa msaada mkubwa kwa mtoto wa kike ambaye amekuwa akishindwa kwenda shule wakati wa hedhi kwa kukosa taulo hizo za kike.

Chanzo: EATV
 
Kodi itozwe kwa taulo za kike toke nje, ila zile zinazotengenezwa nchini zipewe ruzuku kabisa, lazima tulinde ajira za ndani
 
Mambo ya hovyo kabisa halafu mara nyingi watu wanaoaminika ndio wanaofanya mambo ya kishenzi kama hayo. Angalizo usiruhusu mgeni kulala na watoto au mtoto wako
 
Back
Top Bottom