Kutokana na matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni na baraza la mitiani, kama ukifuatilia vizuri wale watoto waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao na kuingia kwenye top ten kuna mabinti wawili wa familia moja ya mzee Mcharo yaani: Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya na Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya. Hawa watoto wameshika nafasi za juu kabisa kwenye hiyo mitihani iliyofanyika mwaka jana. Kufanya vizuri kwa hawa watoto kunanikumbusha kabisa lile tangazo la Vodacom linalosema Mcharo amekuwa mtamu, yaani mzee ambaye alikuwa ni muendesha bodaboda na ghafla maisha yake yalibadilika na kuanza kutunza familia yake vizuri sana ikiwemo watoto wake wanaosoma boarding. Yaani kwa kweli nilivyoona haya matokeo mazuri ya hawa mabinti Angel na Jenifa yamenifanya nione kama kuna uhalisia fulani. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza watoto hawa na familia nzima ya mzee Mcharo.