Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Habari Wana Jamvi,
Mitaa mingi ya Jiji la Mbeya kwa sasa imekuwa ikikambiliwa na changamoto ya ongezeko la vibaka au matukio yanayohusisha vibaka.
Kumekuwa na matukio kadhaa ya watu kuripoti kuibiwa na kwa asilimia kubwa Wananchi wengi tunaona wanaotajwa kuhusika ni Watoto wanaoonekana mitaani.
Hali hiyo imekuwa ikiathiri mitaa ya kuanzia Mafiati mpaka Sae ambapo kumekuwa na vibaka wengi na Wananchi wanaripoti kuwa wahusika ni watoto wadogo.
Watoto ambao tunawashuku ukiwakuta mchana wanakuwa ni wale wanaofanya kazi ya kuombaomba maeneo ya Kabwe na pia wamekuwa wakicheza kamali na kuvuta Bangi maeneo ya Sido Mashine za Mpunga.
Natoa wito kwa Mamlaka za Serikali zinazohusika kuingilia kati suala hili na kukomesha kabisa vibaka kwani Wananchi tukianza kuchukua Sheria mkononi yanaweza kuwa mambo mengine.
Mara nyingi ikifika jioni pale Mitaa ya Kabwe panageuka Soko na Kuna kuwa na Msongamano mkubwa, vibaka nao hutumia mwanya huo wa uwingi wa watu kufanya uhalifu.
Pia, Serikali ya Mkoa wa Mbeya tunaomba liondoeni Soko la jioni pale Kabwe ibaki Stendi tu ili kuweka usalama sawa.