DOKEZO Watoto wa Mitaani Mbeya wanajihusisha na matukio ya uhalifu, wanaanza kuwa tishio, Serikali itatue kabla hali haijawa mbaya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mlikua mnawacheka wakazi wa Dar na Panya rd!
 
Habari Wana Jamvi,

Mitaa mingi ya Jiji la Mbeya kwa sasa imekuwa ikikambiliwa na changamoto ya ongezeko la vibaka au matukio yanayohusisha vibaka.

Kumekuwa na matukio kadhaa ya watu kuripoti kuibiwa na kwa asilimia kubwa Wananchi wengi tunaona wanaotajwa kuhusika ni Watoto wanaoonekana mitaani.

Hali hiyo imekuwa ikiathiri mitaa ya kuanzia Mafiati mpaka Sae ambapo kumekuwa na vibaka wengi na Wananchi wanaripoti kuwa wahusika ni watoto wadogo.

Watoto ambao tunawashuku ukiwakuta mchana wanakuwa ni wale wanaofanya kazi ya kuombaomba maeneo ya Kabwe na pia wamekuwa wakicheza kamali na kuvuta Bangi maeneo ya Sido Mashine za Mpunga.

Natoa wito kwa Mamlaka za Serikali zinazohusika kuingilia kati suala hili na kukomesha kabisa vibaka kwani Wananchi tukianza kuchukua Sheria mkononi yanaweza kuwa mambo mengine.

Mara nyingi ikifika jioni pale Mitaa ya Kabwe panageuka Soko na Kuna kuwa na Msongamano mkubwa, vibaka nao hutumia mwanya huo wa uwingi wa watu kufanya uhalifu.

Pia, Serikali ya Mkoa wa Mbeya tunaomba liondoeni Soko la jioni pale Kabwe ibaki Stendi tu ili kuweka usalama sawa.

Si wa mikoani mnawacheka wanaume wa Dar sasa imekuwaje tena mnaanza kulialia?
 
Huko Mbeya si ndio kuna gereza la watoto la maadilisho kule Irambo, Mbeya Vijijini. Je limeacha kufanya KAZI?
 
Back
Top Bottom