Kile kishule cha vidudu? Mie nilikataa kusoma hapo miaka hiyo kwani nilijua nikirudi kijijini, kaka zangu watanicheka sana kuwa nilisoma shule ya VIDUDU na mie pia ni kidudu.
SIdhani kama utakuwa unanifahamu kwani sikuwa mwenyeji sana zaidi ya jamaa wa Block 4 kama akina Rashidi, Mohamed, Deo na kaka zake, Ray, nk. Kwa mbali bwana Nguvu, kijana Paul na miwani yake, dada yake na wadogo zake. Mhh, zile chips za Mangi na soda zake tamu si kawaida. Ila baadaye mama wa kiarabu(mama Halidi-Marehemu) akaweka Kiosk chake chini ya dirisha letu la jikoni.... Block IV hiloooo baba, miaka hiyo wanaliita ghorofa la watu wanaoshindana. Ukiweka AC, wanajibu, ukiweka antena ya TV, wanakujibu, ukanunua gari, wanakujibu. Kiboko yao ni yule Msomali, ila mkewe alikuwa anatumia sijui mi LADYGAY?? Akipita basi unafeel Oxygen imekwisha. Sijui alikuwa anawezaje kupumua na hiyo harufu?
Nilikuwa pale mwezi wa tatu, nilipotea. Pamebadilika sana. Ikabidi nianze kutafuta nyumba yetu. Mungu bariki nikamuona mama Sembuli (dada ya Marehemu Sembuli wa Yanga)........, heee,kamaliza Chuo kikuu na degree yake ukutani. I was too proud of her. Wamepanda miti na nyuma ya Block IV, nasikia mama Mkapa kanunua lile eneo na ghorofa la Posta na wako busy kuweka jengo hapo. Too sad maana jamaa walikuwa wakicheza mpira hapo jioni (wazee) huku watoto wakichezea huku kwenye shule ya vidudu. Ilikuwa saa nne usiku na sikuonana na watu zaidi ya majirani wa karibu. Sikurudi tena pale. Miaka 10 sasa tangu niwe pale mara ya mwisho na karibu miaka 17 tangu niondoke........... Kumbe yule Mzaramo karibu na Wasabato walimuhamisha na wakajenga kanisa jipya ..... too much change.....