vipi na wewe una miaka mingapi saizi na ushaolewa au bado.Loo! mama yangu alipata shida jamani, tumekulia katika huzuni kubwa sana, chakula kilikuwa kipo japo watoto wa nyumba ndogo walikuwa wanapata nyamanyama, sisi mboga mboga mama anachuma kwenye bustani maharage mtindo mmoja na maombi kwa sana.
Mama yangu alikuwa bi mkubwa, alikuwa mweusi mfupi, bi mdogo alikuwa mweupe mrefu, jamani alikuwa ana matusi mwanamke yule siwezi kumsahau ila nimesamehe. alikuwa anapenda ugomvi, anamtukana mama yangu, anamkimbiza ili wapigane mwee R.I.P mama yangu.
Baba nae alikuwa ametawaliwa na bi mdogo, yani bi mdogo alikuwa anaogopwa na baba kinoma, nyumbani hakuna amani hata chembe. mwe alitutesa alitutesa sana, Mungu amponywe maana bado lupo hai, ila naogopa hata kumwona
Hali hii imechangia familia yangu ya bi mkubwa kukumbwa na msongo wa mawazo, japo wote tumesoma hadi lavel za chuo, wengine diploma wengine form 4 tu lakini hakuna aliendelea kama watoto wa bi mdogo, kaka yangu mkubwa amekuwa mwalimu wa secondary kwa tangu ujana wake hadi uzeeni lakini kashindwa kusomesha watoto wake wawili wanahangaika tu
dada yangu mkubwa nae mtoto mmoja kasoma wengine wanaunga unga tu
dada yangu ninaefatana nae kapata kazi juzi na yupo kwenye 40s hajawahi pata kazi wala kunawili, kila mala alikuwa anaonekana kama analia hahaha, ndipo mimi nikaanza kumfundisha masomo ya kuachilia chuki, achilia hasira, achilia kila jambo linalokuumiza. Mimi pona yangu ni ibada na kusoma soma vitabu vya dini na meditation.
Watoto wa bi mdogo walisoma nao sawa sawa na natoto wa bi mkubwa, ila wao walikulia kwenye upendo hata kazi walipata mapema, maisha yao yalikuwa mazuri mpaka Magufuli alipoingia madarakani na wenyewe ndio maisha yao yaliingia dosali. Kuna waliopelekwa mahajamani kwa uhujumu uchumi, kuna walifukuzwa kazi sijui hata makosa yao.
Lala kwa amani mama yangu, nakukumbuka na nakupenda pia.
yes above 40s na nimeolewavipi na wewe una miaka mingapi saizi na ushaolewa au bado.
safi sana age mateyes above 40s na nimeolewa
Pole sana mpendwa... malipo ni hapahapa duniani.Loo! mama yangu alipata shida jamani, tumekulia katika huzuni kubwa sana, chakula kilikuwa kipo japo watoto wa nyumba ndogo walikuwa wanapata nyamanyama, sisi mboga mboga mama anachuma kwenye bustani maharage mtindo mmoja na maombi kwa sana.
Mama yangu alikuwa bi mkubwa, alikuwa mweusi mfupi, bi mdogo alikuwa mweupe mrefu, jamani alikuwa ana matusi mwanamke yule siwezi kumsahau ila nimesamehe. alikuwa anapenda ugomvi, anamtukana mama yangu, anamkimbiza ili wapigane mwee R.I.P mama yangu.
Baba nae alikuwa ametawaliwa na bi mdogo, yani bi mdogo alikuwa anaogopwa na baba kinoma, nyumbani hakuna amani hata chembe. mwe alitutesa alitutesa sana, Mungu amponywe maana bado lupo hai, ila naogopa hata kumwona
Hali hii imechangia familia yangu ya bi mkubwa kukumbwa na msongo wa mawazo, japo wote tumesoma hadi lavel za chuo, wengine diploma wengine form 4 tu lakini hakuna aliendelea kama watoto wa bi mdogo, kaka yangu mkubwa amekuwa mwalimu wa secondary kwa tangu ujana wake hadi uzeeni lakini kashindwa kusomesha watoto wake wawili wanahangaika tu
dada yangu mkubwa nae mtoto mmoja kasoma wengine wanaunga unga tu
dada yangu ninaefatana nae kapata kazi juzi na yupo kwenye 40s hajawahi pata kazi wala kunawili, kila mala alikuwa anaonekana kama analia hahaha, ndipo mimi nikaanza kumfundisha masomo ya kuachilia chuki, achilia hasira, achilia kila jambo linalokuumiza. Mimi pona yangu ni ibada na kusoma soma vitabu vya dini na meditation.
Watoto wa bi mdogo walisoma nao sawa sawa na natoto wa bi mkubwa, ila wao walikulia kwenye upendo hata kazi walipata mapema, maisha yao yalikuwa mazuri mpaka Magufuli alipoingia madarakani na wenyewe ndio maisha yao yaliingia dosali. Kuna waliopelekwa mahajamani kwa uhujumu uchumi, kuna walifukuzwa kazi sijui hata makosa yao.
Lala kwa amani mama yangu, nakukumbuka na nakupenda pia.
mi bi mdogo namwogopa kama ninavyo ogopa nyoka hahaha kwahio wala simtembelei,,,dingi nae alifariki.Pole sana mpendwa... malipo ni hapahapa duniani.
Afadhali umesamehe na kusahau...
Sasa huyo bimdogo anayeumwa unakumbuka kumtembelea japo umkorogee uji? Na dingi hivi sasa hali yake ikoje?
Sasa ili ulitue zigo vizuri, mtembelee ukamsalimu. Hakika utakuwa umelipa kisasi kwa upendo.mi bi mdogo namwogopa kama ninavyo ogopa nyoka hahaha kwahio wala simtembelei,,,dingi nae alifariki.
kweli bila kusamehe unajikuta umejitwika zigo kubwa sana,,,hakuna namna ni kusamehe tu
asante mpendwa
Hapo hapana Aspin mh kama kuna kitu unakiogopa maishani basi wekea mfano huo, unaweza fika akaanza kukuchamba hahaha.Sasa ili ulitue zigo vizuri, mtembelee ukamsalimu. Hakika utakuwa umelipa kisasi kwa upendo.
Atasutwa na nadhiri mpaka atakapoenda kaburini...
Pole sana kwa kumpoteza baba yako mpendwa. Mungu amrehemu na amsamehe pale alipomkosea.
Mzigo gani si inakuwa kila mtu na Moshe zakemi bi mdogo namwogopa kama ninavyo ogopa nyoka hahaha kwahio wala simtembelei,,,dingi nae alifariki.
kweli bila kusamehe unajikuta umejitwika zigo kubwa sana,,,hakuna namna ni kusamehe tu
asante mpendwa
sijakwelewaMzigo gani si inakuwa kila mtu na Moshe zake
Unajua kwa nn alikataa talaka ni vile aliona akitoa talaka watoto wake watoto wake kwa bimkubwa watapunguza ushirikiano kwa mzee, hayo uyasemayo nayaona home,tatizo la yote hayo ni kuoa mke wa pili kwa vile wa kwanza labda ana kasoro Fulani inakuwa kama vile unamkomoa but pia kuachana na mlieishi nae pia ni ngumu kidogo hasa kunapokuw na sababu ambazo ni ngumu kuzirhibitishaNashukuru sana, mambo ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo nayasikia kwa wenzangu.
MSHUA na MAZA wameridhiana wenyewe na hawana SHOBO lolote lile.
Poleni sana Ndugu zanguni ambao mmepitia/mlipitia/mnaopitia Maisha ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo.
Halafu Wazee wetu wa Kiswahili TABU sana, nilishuhudia moja yaani MZEE alikuwa na MKE mmoja na walibahatika kupata Watoto kama SABA hivi kama sijakosea.
Cha ajabu yule MZEE sijui kavurugwa kitu gani!
Eti ameenda Kuoa Mke MBICHI, yaani Mtoto wake wa kwanza (wa huyo MZEE) Kiumri ni mkubwa kuliko huyo Bi Mdogo.
Sio siri, Watoto wa yule MZEE walimaindi sana kiasi kwamba ikaleta TAFRANI kubwa mpaka kufikia MAMA (Bi Mkubwa) wa wale Watoto kuomba TALAKA.
Cha ajabu yule MZEE amekaza, haikutolewa TALAKA.
Na kuonesha kuwa yule MZEE alikuwa dhaifu, kwenye Nyumba (aliyomjengea) ya Bi mdogo ndio akaamua kuhamia kabisa.
Yaani MZEE alikuwa hasikii na wala haoni.
Nyumba yao ambayo MZEE alikuwa akiishi na Bi Mkubwa, MZEE alikuwa anaenda kama kusalimia na kisha kuondoka, tena baada ya Muda mrefu