Watoto wa mke mkubwa tukutane hapa

Watoto wa mke mkubwa tukutane hapa

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
5,915
Reaction score
7,210
Kama wewe ni mtoto wa mke wa kwanza kwa mzee wako, njoo hapa tukumbushane shida na karaha tulizoziahudunia wakiwa mama zetu kisa mke mdogo.

Watoto wa bi mkubwa tukikosa huduma huku watoto wa bi mdogo wakithaminiwa kama almasi

Nakumbuka mzee wangu hakuwahi hata kuninunulia shati au suruali. Nilikua kwa uwezo wa mama yangu.

Je, wewe ilikuaje?
 
Loo! mama yangu alipata shida jamani, tumekulia katika huzuni kubwa sana, chakula kilikuwa kipo japo watoto wa nyumba ndogo walikuwa wanapata nyamanyama, sisi mboga mboga mama anachuma kwenye bustani maharage mtindo mmoja na maombi kwa sana.
Mama yangu alikuwa bi mkubwa, alikuwa mweusi mfupi, bi mdogo alikuwa mweupe mrefu, jamani alikuwa ana matusi mwanamke yule siwezi kumsahau ila nimesamehe. alikuwa anapenda ugomvi, anamtukana mama yangu, anamkimbiza ili wapigane mwee R.I.P mama yangu.
Baba nae alikuwa ametawaliwa na bi mdogo, yani bi mdogo alikuwa anaogopwa na baba kinoma, nyumbani hakuna amani hata chembe. mwe alitutesa alitutesa sana, Mungu amponywe maana bado lupo hai, ila naogopa hata kumwona
Hali hii imechangia familia yangu ya bi mkubwa kukumbwa na msongo wa mawazo, japo wote tumesoma hadi lavel za chuo, wengine diploma wengine form 4 tu lakini hakuna aliendelea kama watoto wa bi mdogo, kaka yangu mkubwa amekuwa mwalimu wa secondary kwa tangu ujana wake hadi uzeeni lakini kashindwa kusomesha watoto wake wawili wanahangaika tu
dada yangu mkubwa nae mtoto mmoja kasoma wengine wanaunga unga tu
dada yangu ninaefatana nae kapata kazi juzi na yupo kwenye 40s hajawahi pata kazi wala kunawili, kila mala alikuwa anaonekana kama analia hahaha, ndipo mimi nikaanza kumfundisha masomo ya kuachilia chuki, achilia hasira, achilia kila jambo linalokuumiza. Mimi pona yangu ni ibada na kusoma soma vitabu vya dini na meditation.
Watoto wa bi mdogo walisoma nao sawa sawa na natoto wa bi mkubwa, ila wao walikulia kwenye upendo hata kazi walipata mapema, maisha yao yalikuwa mazuri mpaka Magufuli alipoingia madarakani na wenyewe ndio maisha yao yaliingia dosali. Kuna waliopelekwa mahajamani kwa uhujumu uchumi, kuna walifukuzwa kazi sijui hata makosa yao.
Lala kwa amani mama yangu, nakukumbuka na nakupenda pia.
 
Watoto wa mke mdogo sisi wala bata huku hapatuhusu?
 
vipi na wewe una miaka mingapi saizi na ushaolewa au bado.
 
Pole sana mpendwa... malipo ni hapahapa duniani.

Afadhali umesamehe na kusahau...

Sasa huyo bimdogo anayeumwa unakumbuka kumtembelea japo umkorogee uji? Na dingi hivi sasa hali yake ikoje?
 
mi bi mdogo namwogopa kama ninavyo ogopa nyoka hahaha kwahio wala simtembelei,,,dingi nae alifariki.
kweli bila kusamehe unajikuta umejitwika zigo kubwa sana,,,hakuna namna ni kusamehe tu

asante mpendwa
 
Sasa ili ulitue zigo vizuri, mtembelee ukamsalimu. Hakika utakuwa umelipa kisasi kwa upendo.

Atasutwa na nadhiri mpaka atakapoenda kaburini...

Pole sana kwa kumpoteza baba yako mpendwa. Mungu amrehemu na amsamehe pale alipomkosea.
 
Hapo hapana Aspin mh kama kuna kitu unakiogopa maishani basi wekea mfano huo, unaweza fika akaanza kukuchamba hahaha.
Ila moyoni mwangu sina neno nae maana hata baba anahusika katika hili, sasa naona haisaidii kumlalamikia mama wa kambo peke yake. Kuna kaka yangu ndio anawezana nae maana nae mtata sana ko wanawezana sana tu
 
Nashukuru sana, mambo ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo nayasikia kwa wenzangu.

MSHUA na MAZA wameridhiana wenyewe na hawana SHOBO lolote lile.

Poleni sana Ndugu zanguni ambao mmepitia/mlipitia/mnaopitia Maisha ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo.

Halafu Wazee wetu wa Kiswahili TABU sana, nilishuhudia moja yaani MZEE alikuwa na MKE mmoja na walibahatika kupata Watoto kama SABA hivi kama sijakosea.

Cha ajabu yule MZEE sijui kavurugwa kitu gani!

Eti ameenda Kuoa Mke MBICHI, yaani Mtoto wake wa kwanza (wa huyo MZEE) Kiumri ni mkubwa kuliko huyo Bi Mdogo.

Sio siri, Watoto wa yule MZEE walimaindi sana kiasi kwamba ikaleta TAFRANI kubwa mpaka kufikia MAMA (Bi Mkubwa) wa wale Watoto kuomba TALAKA.

Cha ajabu yule MZEE amekaza, haikutolewa TALAKA.

Na kuonesha kuwa yule MZEE alikuwa dhaifu, kwenye Nyumba (aliyomjengea) ya Bi mdogo ndio akaamua kuhamia kabisa.

Yaani MZEE alikuwa hasikii na wala haoni.

Nyumba yao ambayo MZEE alikuwa akiishi na Bi Mkubwa, MZEE alikuwa anaenda kama kusalimia na kisha kuondoka, tena baada ya Muda mrefu
 
mi bi mdogo namwogopa kama ninavyo ogopa nyoka hahaha kwahio wala simtembelei,,,dingi nae alifariki.
kweli bila kusamehe unajikuta umejitwika zigo kubwa sana,,,hakuna namna ni kusamehe tu

asante mpendwa
Mzigo gani si inakuwa kila mtu na Moshe zake
 
Nashukuru sana, mambo ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo nayasikia kwa wenzangu.

MSHUA na MAZA wameridhiana wenyewe na hawana SHOBO lolote lile.

Poleni sana Ndugu zanguni ambao mmepitia/mlipitia/mnaopitia Maisha ya Bi Mkubwa na Bi Mdogo.

Halafu Wazee wetu wa Kiswahili TABU sana, nilishuhudia moja yaani MZEE alikuwa na MKE mmoja na walibahatika kupata Watoto kama SABA hivi kama sijakosea.

Cha ajabu yule MZEE sijui kavurugwa kitu gani!

Eti ameenda Kuoa Mke MBICHI, yaani Mtoto wake wa kwanza (wa huyo MZEE) Kiumri ni mkubwa kuliko huyo Bi Mdogo.

Sio siri, Watoto wa yule MZEE walimaindi sana kiasi kwamba ikaleta TAFRANI kubwa mpaka kufikia MAMA (Bi Mkubwa) wa wale Watoto kuomba TALAKA.

Cha ajabu yule MZEE amekaza, haikutolewa TALAKA.

Na kuonesha kuwa yule MZEE alikuwa dhaifu, kwenye Nyumba (aliyomjengea) ya Bi mdogo ndio akaamua kuhamia kabisa.

Yaani MZEE alikuwa hasikii na wala haoni.

Nyumba yao ambayo MZEE alikuwa akiishi na Bi Mkubwa, MZEE alikuwa anaenda kama kusalimia na kisha kuondoka, tena baada ya Muda mrefu
Unajua kwa nn alikataa talaka ni vile aliona akitoa talaka watoto wake watoto wake kwa bimkubwa watapunguza ushirikiano kwa mzee, hayo uyasemayo nayaona home,tatizo la yote hayo ni kuoa mke wa pili kwa vile wa kwanza labda ana kasoro Fulani inakuwa kama vile unamkomoa but pia kuachana na mlieishi nae pia ni ngumu kidogo hasa kunapokuw na sababu ambazo ni ngumu kuzirhibitisha
Mimi nilisema baba/mama asimulie ubaya wa mwenzie hayo hayanihusu nilikataa kuegemea upande yeyote asimulie nasikilizaga na kukaa kimya ila atakayehatarisha maslahi yangu huyo ndo atakuwa adui yangu ila sio kusimuliwa huyu hivi au vile
 
Sometime kuoa mke mwingine hufanywa na mtu kutokana na mateso ya mke ulonaye. But this isn't a ticket kutesa watoto.
Wanawake jitambueni acheni upumbavu.
Hata watumishi wa ustawi wa jamii jitambueni tabia zenu ziko wazi kuthamini wanawake kwa ujinga wafanyao.
Sihitaji kuleta case study hapa ukweli inahuzunisha.
Wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa kutegemea mteremko sasa akikuta utofauti au vyuma vikikaza usaliti mtindo mmoja mwanaume akijiongeza yeye anatumia watoto kama fimbo.
Mbona mnapoachika na kuzalishwa huko mnachakaa mno na wanaowachakaza hamuwafungulii mashtaka.
Wapo wanawake wanaonewa lakin ni wachache mno. Wanawake jitambueni unamwambia mme hela haitoshi wewe yako iko wapi uongeze ili itoshe.
Mungu aliposema mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake mwenyewe hakika alilijua hili. Hakuna mwanaume anayevunja nyumba bali nyumba huvunjwa na mwanamke hiyo ndiyo principle ya Mungu wewe endelea kupinga maana ndiyo jadi yako.
wanaposema hakuna mkate mgumu kwa chai ujue hakuna mme mbishi kwa mke anayejitambua tatizo unaenda kuolewa hata wajibu wako huujui utaishia kuwa mama watoto badala ya mke. Wee mwanamke gani unachojua ni kuzaa tu hata mapenzi kwako ni zero umebaki kujivunia cheti cha ndoa sasa kopo limepata mfuniko wake baki na cheti chako uone mziki wake shankupe wewe.
Umepata mshahara huwezi kununua hata pedi yako hela hadi za mmeo kila kitu sasa usaidizi wako ni nini?.
Mme hata zawadi yako haijui wewe pesa yako haijulikani matumizi yake. Nakwambia utaendelea kuitwa mama watoto mke hawi kama wewe.
Unamkuta mwanamke kitandani yuko vizuri, chakula kwa wakati, msafi wewe kwenye gari tu ukipanua miguu watu wanasimama kukuachia kiti kwa uvundo bado majibu ya ovyo nakwambia utaishia kuzaa watoto kwenye mafungu kama mchicha usipojitambua shankupe.
Mwanaume hazoeleki ukimzoea mme ni ishara ya kubipu talaka. Unakuta mke anayokufanyia hadi ukiwa bafuni pekee yako unainua mikono juu kumwambia Mungu ulimchelewesha wapi huyu malaika?.
Jamani wanaume hatupendi kelele kila siku mtu unafungua kesi kitandani hatuvumilii ujinga huo. Wanawake badilikeni.
 
Back
Top Bottom