Loo! mama yangu alipata shida jamani, tumekulia katika huzuni kubwa sana, chakula kilikuwa kipo japo watoto wa nyumba ndogo walikuwa wanapata nyamanyama, sisi mboga mboga mama anachuma kwenye bustani maharage mtindo mmoja na maombi kwa sana.
Mama yangu alikuwa bi mkubwa, alikuwa mweusi mfupi, bi mdogo alikuwa mweupe mrefu, jamani alikuwa ana matusi mwanamke yule siwezi kumsahau ila nimesamehe. alikuwa anapenda ugomvi, anamtukana mama yangu, anamkimbiza ili wapigane mwee R.I.P mama yangu.
Baba nae alikuwa ametawaliwa na bi mdogo, yani bi mdogo alikuwa anaogopwa na baba kinoma, nyumbani hakuna amani hata chembe. mwe alitutesa alitutesa sana, Mungu amponywe maana bado lupo hai, ila naogopa hata kumwona
Hali hii imechangia familia yangu ya bi mkubwa kukumbwa na msongo wa mawazo, japo wote tumesoma hadi lavel za chuo, wengine diploma wengine form 4 tu lakini hakuna aliendelea kama watoto wa bi mdogo, kaka yangu mkubwa amekuwa mwalimu wa secondary kwa tangu ujana wake hadi uzeeni lakini kashindwa kusomesha watoto wake wawili wanahangaika tu
dada yangu mkubwa nae mtoto mmoja kasoma wengine wanaunga unga tu
dada yangu ninaefatana nae kapata kazi juzi na yupo kwenye 40s hajawahi pata kazi wala kunawili, kila mala alikuwa anaonekana kama analia hahaha, ndipo mimi nikaanza kumfundisha masomo ya kuachilia chuki, achilia hasira, achilia kila jambo linalokuumiza. Mimi pona yangu ni ibada na kusoma soma vitabu vya dini na meditation.
Watoto wa bi mdogo walisoma nao sawa sawa na natoto wa bi mkubwa, ila wao walikulia kwenye upendo hata kazi walipata mapema, maisha yao yalikuwa mazuri mpaka Magufuli alipoingia madarakani na wenyewe ndio maisha yao yaliingia dosali. Kuna waliopelekwa mahajamani kwa uhujumu uchumi, kuna walifukuzwa kazi sijui hata makosa yao.
Lala kwa amani mama yangu, nakukumbuka na nakupenda pia.